Tanzania bila Mahakama ya Kikatiba, Uchaguzi ni bure

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,658
22,255
Tanzania Uchaguzi wa Rais hupangwa na watu walioapishwa na rais aliyepo madarakani na kutoa matokeo yanayokubalika na rais aliyeiapisha tume.

Ili uchaguzi uwe na tija tume ya uchaguzi iwe ni ajira binafsi na matokeo yatangazwe baada ya mahakama ya kikatiba kuridhika baada ya vigezo vyote visivyo na shaka kuridhiwa na wagombea wa vyama husika, hii italeta heshima kwa nchi.
 
Wabunge wa Chadema walitangazwa na tume gani?
Bila kutumia policcm kukwapua masanduku ya kura na kukimbia nayo, kupandikiza mamluki wa chama na wakurugenzi makada kusimamia uchaguzi ccm isingepata hata wabunge watano (5)
 
Sidhani kama Serikali ya Ccm itakubali kujitia kitanzi shingoni! Kama wanaogopa tu hata uwepo wa Mgombea binafsi, ndiyo wakubali uwepo wa hiyo Mahakama ya Kikatiba!
 
Duu hizi ndoto za mchana

Nafikiri Wewe ni moja ya vijana wanaojidanganya ccm imechoka kwa kuangalia comment kumi za jamii forum

Kumbuka maneno ya Bashiru dola yako ushindwaje uchaguzi?
Dr. Bashiru alisema kweli akiwa na maana kura yako siyo haki yako, uamuzi wa mshindi hutolewa na tume bila kuzingatia idadi ya kura kwa sababu hakuna mahakama ya kikatiba kuthibitisha mshindi.
 
Tanzania uchaguzi wa rais hupangwa na watu walioapishwa na rais aliyepo madarakani na kutoa matokeo yanayokubalika na rais aliyeiapisha tume.

Ili uchaguzi use na tija tume ya uchaguzi iwe ni ajira binafsi na matokeo yatangazwe baada ya mahakama ya kikatiba kuridhika baada ya vigezo vyote visivyo na shaka kuridhiwa na wagombea wa vyama husika, hii italeta heshima kwa nchi.
Ibara ya 125 ya katiba ya JMT inazungumzia kuwepo kwa special constitutional Court. We unataka mahakama gani ya kikatiba zaidi ya hii. Au umekaririshwa hujui unachotaka kuulizia?
 
Safari hii, Mzee wa Chato ataugua zaidi kuliko ilivyokuwa aliposemeshwa juu ya uwepo wa tume huru.
 
Duu hizi ndoto za mchana

Nafikiri Wewe ni moja ya vijana wanaojidanganya ccm imechoka kwa kuangalia comment kumi za jamii forum
Kwahiyo CHADEMA walipata kura 10

Ilikuwaje sasa mkapata 58% ya kura zote?
 
Tanzania uchaguzi wa rais hupangwa na watu walioapishwa na rais aliyepo madarakani na kutoa matokeo yanayokubalika na rais aliyeiapisha tume.

Ili uchaguzi use na tija tume ya uchaguzi iwe ni ajira binafsi na matokeo yatangazwe baada ya mahakama ya kikatiba kuridhika baada ya vigezo vyote visivyo na shaka kuridhiwa na wagombea wa vyama husika, hii italeta heshima kwa nchi.
Nadhani issue siyo kutafuta mahakama ya kikatiba, bali kinachotakiwa ni Katiba mpya itakayoruhusu pamoja na mambo mengine matokeo ya uchaguzi wa Rais kupingwa mahakamani kama ilivyo Kenya na Marekani
 
Sidhani kama Serikali ya Ccm itakubali kujitia kitanzi shingoni! Kama wanaogopa tu hata uwepo wa Mgombea binafsi, ndiyo wakubali uwepo wa hiyo Mahakama ya Kikatiba!
Kwani Tanzania haina Mahakama ya Kikatiba au wewe ndio hujui kuwa ipo!? Ebu isome Katiba ya JMT.
 
Sasa nani wa kupigia Kura upinzani hapa Tanzania labda misukule
 
Nadhani issue siyo kutafuta mahakama ya kikatiba, bali kinachotakiwa ni Katiba mpya itakayoruhusu pamoja na mambo mengine matokeo ya uchaguzi wa Rais kupingwa mahakamani kama ilivyo Kenya na Marekani
Sawa kupingwa mahakamani lakini mahakama gani, ya wezi wa kuku? Mahakama pekee ni ya kikatiba ambayo inazo tafsiri zote za sheria ya uchaguzi hivyo haiwezi kuipasia mahakama nyingine iisikilize kesi ya uchaguzi.
 
Ibara ya 125 ya katiba ya JMT inazungumzia kuwepo kwa special constitutional Court. We unataka mahakama gani ya kikatiba zaidi ya hii. Au umekaririshwa hujui unachotaka kuulizia?
IPO? Mgombea binafsi naye ni haki, yupo? Elezea jambo ambalo lipo si la ndani ya vitabu.
 
Back
Top Bottom