Tanzania bila Katiba mpya ipo siku tutajuta

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
14,130
21,268
Habari wakuu,

Mimi binafsi naweza sema matatizo yote ya nchi yetu ni katiba, hata JPM isingekuwa katiba ya hovyo iliyopo asingekuwa na mamlaka ya kuendesha nchi namna ile.

Katiba yetu imempa madaraka makubwa sana raisi, yaani anaweza kufanya lolote analotaka, mbaya zaidi nchi yetu unaweza kulala leo, kesho unaamka ni rais.

Siku tukipata rais ambaye anajijua mwenye alivyo ndio siku ya majuto, hii haijalishi ni CCM, Chadema, CUF wala ACT- Wazalendo.

Msifikili kila awamu tutapata rais mstarabu ambaye anajua ubinadamu, kwa hii katiba ya akiamua lolote ni yeye hapingwi, ipo siku tu
Swala kila anayeingia anaanza upya na mambo yake mwenye binafsi kama anaongoza familia ni sababu ya katiba yetu ya hovyo, ipo siku tutajuta kama taifa.

Ndio kama hivyo ufisadi na wizi hadharani unaonekana lakini hakuna wa kulaumiwa wala kuwajibishwa, tunabiki tunaangaliana.

KATIBA, KATIBA, KATIBA
 
Hili Nyerere aliliona zamani sana, akaamini watakaofuata labda wataliweka sawa badala yake waliofuata madaraka yamewanogea wanaona Katiba mpya itapunguza raha fulani wakiwa madarakani, kuhusu kujuta nadhani mfano tumeupata awamu iliyopita, kama sio Mungu kuingilia kati hali yetu kama Taifa ingekuwa ngumu sana.

KATIBA, KATIBA, KATIBA

Naunga mkono huu Uzi.
 
Tuendelee kushangilia tu ripoti ya CAG hakuna kujuta wala nini, na next year tena tushangilie tu, taifa la raia wenye vichwa vinavyoyumbishwa na upepo kama majani ya miti.
 
Back
Top Bottom