Uchaguzi 2020 Tanzania bara vs Tanzania visiwani, muelekeo wa uchaguzi mkuu 2020

Tman Clever

Member
Dec 20, 2012
37
28
TANZANIA VISIWANI(ZANZIBAR)
Ninauona uchaguzi ukiwa mwepesi Sana kwa upande wa Maalim Seif,
Haijarishi atapata mpinzani wa Aina gani kutoka Chama chochote tofauti na anachogombea.

Pia kutangazwa kwa ushindi wake kwa awamu hii hakutotegemea maagizo kutoka juu kama ataamua kukisimamia alichoahidi.

Kuhusu hili, lipo wazi kwani Historia yake sote tunaifahamu, ni anaenda kuendeleza tu umwamba wake,

Na awamu hii tutarajie lolote kuhusu yeye.

TANZANIA BARA (TANGANYIKA)
Tutarajie uchaguzi mgumu, mgumu Sana.

CCM: Wao washapata mgombea anaejulikana.

Kwa mgombea huyu, mtu yeyote ukimwambia nenda kamnadi, Sera za kumnadi ni zilezile, zishajulikana na hazitobadirika hata kabla,wakati na baada ya kampeni.

Kwa mgombea huyu, hata aamue kuwe na tume huru, bado anauwezo wa kuchota kura nyingi hasa kwa makundi maalumu waliko jiwekeza vizuri (Makundi hayo yanafahamika, ila tutaandaa uzi tukumbushane), na mikoa fulani fulani na maeneo fulani fulani waliyojiwekeza tangu enzi (Mfn: Dodoma yote).

VYAMA MBADALA
Ninaviona vyama Mbadala vikiwa katika wakati mgumu,

kwanza ni kutokana na Aina ya siasa na uendeshwaji wa uchaguzi ambao kamwe haujawahi kuwa rafiki kwa vyama hivi.

Pili: Ni Namna vyama hivi vimejipanga kuingia kwenye uchaguzi mkuu hasa Ngazi ya Urais.

Tuzungumzie kidogo muelekeo wa vyama Mbadala(Opposition Parties) viwili CHADEMA na ACT.

Hawa Wote bado hawajamtambulisha mgombea wa Urais,

ACT:
Ninaona wakisubiri maamuzi na muelekeo wa BKM, ili ndio pengine aje kuwa Mgombea Wao wa Urais.
Jambo jema Halihitaji haraka.
Tuendelee kusubiri.

Wakifanikiwa kwa hili, ninaiona ACT ikijiimarisha zaidi, japo ukweli ni kwamba kuubeba Urais kwa awamu hii ni ndoto za mchana.

Na wasipo fanikiwa kuubeba Urais, je Hawa wahamiaji wakina BKM wataweza kuvumilia shuruba, machungu, figisu na vitimbwi kwa miaka 5 mbele wakiwa kwenye vyama Mbadala? Ama ndio watafanya kama walivyofanya watangulizi wa kuhama na kurudi walikotoka.

Tahadhari ni kwamba kwenye siasa lolote laweza kutokea.

CHADEMA:
Mchakato unaoneka wa kuvutia hasa tunapoona wameruhusu mgombea wa mwaka huu akienda kupatikana kidemokrasia kwelikweli(Kama kweli wataendelea hivi hadi mwisho wa mchakato).

Mgombea Yeyote kupitia Chama hiki ni dhahiri atakuwa na effects kubwa (madhara makubwa kwa mgombea wa Chama tawala) kwenye mbio za Urais,

Tuijuavyo CHADEMA, miaka yote uweka wagombea wenye madhara makubwa kwa Chama tawala. Tunaweza wadhania tuwaonavyo mwisho wa siku wakaja na Mgombea ambae hatukumtarajia.

BKM:
Huyu ndio kete ya turufu kwenye uchaguzi wa mwaka huu,.
Ni maamuzi yake yeye mwenyewe eidha asalie aliko, ama asaidie kuamsha na kuyachangamsha mabadiliko yanayosubiriwa miongo kadhaa tangu tupate uhuru kutoka kwa Wazungu .

Kuenda kwake ACT kutaipendeza na Kuinufaisha ACT pengine (Kumb: Pengine ) kuelekea kuwa Chama Mbadala kikubwa siku za mbeleni ( Sio baada ya uchaguzi huu)

Kuenda kwake CHADEMA kunaweza kuwa na matokeo makubwa zaidi na miujiza ikatendeka.

Lakini je, CHADEMA wako tayari kurudia waliyoyafanya 2015?
Tuwasubiri kwani Wana watu wenye mipango ambayo haitabiriki.

CHADEMA vs ACT vs BKM
Endapo watatu Hawa wakabahatika kuwa pamoja, tutarajie miujiza mikubwa zaidi.

Lakini, Endapo watatu Hawa wakajigawa na kuwa wawili tofauti tofauti,
eidha {CHADEMA + BKM}
ama {ACT + BKM}

Wataurahisisha zaidi uchaguzi huu kwa kuzigawagawa kura za raia wanaohitaji mabadiliko.

IKUMBUKWE: Si kila Raia anaehitaji mabadiliko ni wa vyama Mbadala.

Ikiwa hivi, Basi tutarajie ushindi mnono kwa mgombea wa Chama tawala ambaye tayari Sera zake zinajulikana na kila mmoja wetu.
 
TANZANIA VISIWANI(ZANZIBAR)
Ninauona uchaguzi ukiwa mwepesi Sana kwa upande wa Maalim Seif,
Haijarishi atapata mpinzani wa Aina gani kutoka Chama chochote tofauti na anachogombea.

Pia kutamgazwa kwa ushindi wake kwa awamu hii hakutotegemea maagizo kutoka juu kama ataamua kukisimamia alichoahidi.

Asante kwa uchambuzi mzuri na tujipange vizuri wapenda mabadiliko dhidi ya bao la mkono pia.
 
Back
Top Bottom