TANZANIA BARA sasa kuwa TANGANYIKA - RASIMU YA 2

mrelbattawy

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
564
112
Inafurahisha na kutia moyo sasa kuona kwamba ndugu zetu wa Bara kwa mujibu wa Rasimu hii ya 2 wamefumbua macho na kufahamu identity yao kurudi katika jina lao la awali TANGANYIKA badala ya Tanzania Bara., Hongera sana Warioba mengine yatajiseti kwenye Bunge la Katiba.,
 
kwani imeandikwa Tanzania bara au Tanganyika tujuwavyo watu wa bara tunajua kuwa tuna Tanzania ambayo inasimama kama Serikali ya muungano
 
Ikiwa Kuna Zanzibar Lazima Kuwe Na Tanganyika Kwa Maana Ya Tanzania Ili Kulinda Hadhi Na Matakwa Ya Washiriki Wa Muungano
 
Ikiwa Kuna Zanzibar Lazima Kuwe Na Tanganyika Kwa Maana Ya Tanzania Ili Kulinda Hadhi Na Matakwa Ya Washiriki Wa Muungano

Hakuna Zanzibar pasipo Unguja na Pemba wala Tanzania pasipo na Tanganyika na Zanibar....but still we can keep our Tanganyika na kubadili ramani ya Dunia..kama zamani.
 
Safi sana hii inaitwa pasu kwa pasu...ka kuna Zanzibar it is very obvious upande wa pili ni Tanganyika.
Hiyo Tanzania bara sijui ilitoka wapi..
 
Welcome back Tanganyika. Kujiita Tanzania bara siku muungano ukivunjika tutaadhirika
Yaani kufikiria kwako ndo mwisho wake hapo? Haya tuambie kama hilo jina "Tanganyika" litawafanya mafisadi wakarudisha mabilioni ya Uswisi ambayo mzee wa Kigoma na wengine wameshindwa hata kutaja jina moja! Au kama litatuondoa kwenye wimbi la umaskini wa kutisha huku tukiwa na rasilimali za kufa mtu. Mijitu mingine hata hamuoni zaidi za pua zenu, poor you!
 
hivi kwa Tanganyika: inatakiwa kuwa wimbo wa Taifa na nembo ya Taifa mpya tofauti na ilivyo sasa?
 
Malalamiko Muungano

Alisema kila upande wa Muungano una malalamiko mengi kuhusu muundo na kwamba tume hiyo imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane kwa upande wa Tanzania Bara.

Alisema kwa upande wa Zanzibar, malalamiko matatu makubwa ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la Serikali ya Muungano ambalo linaisaidia zaidi Tanganyika kuliko Zanzibar na kuifanya Tanganyika kuwa Tanzania.

Pili, mambo ya Muungano kuongezeka na kuathiri madaraka na kuishusha hadhi Zanzibar na tatu ni kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Alisema kwa Tanzania Bara, malalamiko makubwa ni Zanzibar kuwa nchi huru yenye bendera yake, wimbo wa taifa, serikali yake na imebadili Katiba yake ili ijitambue kama nchi, wakati Tanzania Bara imepoteza utambulisho wake. Katiba ya Jamhuri inasema Tanzania ni nchi moja lakini Katiba ya Zanzibar inasema ni nchi mbili.

Pili, Zanzibar imebadili Katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamhuri ya Muungano, kuelekeza sheria za Muungano zinazopitishwa na Bunge la Muungano zipelekwe kwanza kwenye Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika.

Tatu, wananchi wa Tanzania bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar, wakati wenzao wana haki hiyo Tanzania bara.

Muundo wa Muungano

Alisema katika kuchambua malalamiko ya Zanzibar, Tume imebaini kuwa muundo wa Muungano wa Serikali mbili umeifanya Serikali ya Muungano kushughulikia zaidi mambo ya Tanzania bara, hasa maendeleo na uchumi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977, Serikali ya Muungano ina mamlaka ya kusimamia mambo ya Muungano na yasiyo na muungano kwa upande wa bara... "Kwa msingi huo, Serikali ya Muungano inashughulikia sana kilimo, elimu, afya, maji, nishati na madini, ujenzi, uchukuzi, maliasili na utalii na mengine ya Tanzania bara yasiyo ya Muungano."

Alisema kutokana na hali hiyo, Tume haikuwa na njia nyingine kwa sababu Serikali ya Muungano haina madaraka ya kutosha juu ya mambo ya maendeleo na uchumi kwa upande wa Zanzibar na kwamba hata utafutaji wa rasilimali zaidi ni kwa ajili ya Tanzania bara kuliko Zanzibar.

Alisema Zanzibar inafanya mipango yake ya maendeleo, kwamba ili ipate rasilimali, kama mikopo na misaada, ni lazima ipitie Serikali ya Muungano jambo ambalo utekelezaji wake umesababisha matatizo mengi.

"Njia pekee ambayo ingeiwezesha Zanzibar kufaidi shughuli za Serikali ya Muungano wa maendeleo ya Zanzibar ni mambo yote kuwa chini ya Muungano kwa maana ya kuwa na Serikali moja, lakini hilo likifanyika kuna hofu ya Zanzibar kumezwa," alisema.

Alisema tume hiyo imefanya uchambuzi wa mambo 22 ya Muungano ili kubaini kama yanaingilia hadhi ya uhuru wa Zanzibar na kubaini kuwa siyo yote yanayotekelezeka. Mengi yamebadilishwa bila kubadili Katiba au kwa makubaliano ya pande mbili.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kodi, bandari, viwanda, usafiri na usafirishaji wa anga, utafiti, posta na simu, uraia, takwimu, mafuta na gesi na Mahakama ya Rufaa.


"Kama Katiba ya Zanzibar ikibaki kutakuwa na nchi mbili; zikiwa nchi mbili haitawezekana nchi moja iwe na hadhi na uhuru na nchi nyingine isiwe na hadhi na uhuru, kwa tathmini yetu, tunaona ukarabati huu ni mgumu. Serikali tatu ndiyo suluhisho," alisema.

 
I am very disappointed na huyu 'Jakaya Kikwete' he is a such useless president kila kukicha yupo njiani hivi kwanini watu wanataka kazi ambazo hawazijui. Huwezi kuja na sera za namna ya muungano bila ya wanasiasa wanaounga na wasiouunga mkono kutoa hoja za kisiasa na debate za kueleweka.

Hiwapo kweli hakuna makubaliano ya kisiasa na kuna maswala ambayo yameshindikana kupatiwa majibu ndani ya mungano. Suluhisho ni kura za maoni kujua watanzania wanataka nini watu wanarudi ubaoni na kurebisha vile watu wanataka, na sio kujiamulia tu kutokana na influence za draft drawers kama huyu babu Warioba pengine he has dementia halafu anatuletea mapendekezo uchwara.

The whole process was undemocratic na CCM imejionyesha jinsi ilivyo legelege hao CDM na CUF wala hawaeleweki vyama ambavyo vipo pro nationalistic kawaida havi cross border kwenye ulimwengu wa siasa ni wajinga wachache wanaviongoza na kuwatisha viongozi wa CCM wa sasa. Mwalimu huko aliko naona anajuta kutowafunza wanafunzi wake vilivyo kwa tamaa zake za madaraka na kupenda kuzungukwa na wajinga, it is a sad day for those of us who wanted to see further assimilation mshindi ni siasa za udini na ukanda (kuna watu wameshaanza kusema raisi ajae atoke wapi na awe wa dini hipi) ndio tumefikia hapa. Poor Tanzania, wenzenu walipigana kuungana.
 
Inafurahisha na kutia moyo sasa kuona kwamba ndugu zetu wa Bara kwa mujibu wa Rasimu hii ya 2 wamefumbua macho na kufahamu identity yao kurudi katika jina lao la awali TANGANYIKA badala ya Tanzania Bara., Hongera sana Warioba mengine yatajiseti kwenye Bunge la Katiba.,

Nimeisoma yote, ipo safi, Ma ccm hawana uso wa aibu, wapo Zanzibar kwenye mikutano ya hadhara wanaipinga! Rasimu inastahili kupita bila kupingwa labda kama kuna maboresho kidogo.
 
Kuhusu Madaraka Na Kinga Kwa Rais Alafu Mgombea Binafsi Bila Kusahau %50+ Kura Za Rais,rasimu Inaelezaje Wakuu?
 
hivi kwa Tanganyika: inatakiwa kuwa wimbo wa Taifa na nembo ya Taifa mpya tofauti na ilivyo sasa?

Ndio maana ake...Mungu ibariki Tanzania ndio inakua zilipendwa hivyo..track mpya Mungu ibariki Tanganyika
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom