Nimeuliza hivyo kwakuwa nakumbuka nilipokuwa nasoma na hata katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inatamka nchi iitwayo Tanganyika ndiyo iliyoungana na Zanzibar kuwa Tanzania.
Sasa hii Tanzania bara tunaitoa wapi? Nauliza hivi kwakuwa hata wasomi wetu nao utawasikia wakisema Tanzania bara na hata rais wetu Kikwete leo kwenye maadhimisho katamka hivyohivyo. Sasa hamuoni historia na uhalisia tu kuwa mnaviharibu?
Baraza la mitihani (NECTA) mfano likatunga swali lisemalo; Jaza sehemu iliyoachwa wazi kwenye sentensi hii- 9/12/1961 ni siku ya uhuru wa nchi ya_________( Akajaza Tanzania Bara) atakuwa kapata ama kakosea? Vinginevyo mnatuchanganya na kuchanganya watoto wetu.
Mnamdanganya na kumfariji nani kwa kutaja Tanzania bara badala ya Tanganyika?