Tanzania bara kuna wagonjwa wa akili milioni saba!

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Kwa mujibu wa Mtaalam wa Afya ya Akili Josefina Kaponya aliyeongea katika kipindi cha DW saa saba mchana 22/10/2022, kuna watu milioni saba nchini Tanzania bara wenye maradhi ya akili! Maana ya takwimu za mtaalam huyo ni kwamba zaidi ya asilimia kumi (10%) ya Watanzania milioni 60 wana matatizo ya akili!

Binafsi nina wasiwasi kuhusu taarifa hii, kama ni kweli ni hatari sana kwa nchi na ni lazima lifanyiwe kazi kwa umakini sana. Lazima tujiulize kama hali hii ni ya kawaida au ni kwa Tanzania tu? Na kwanini iwe hivyo?
 
Kama Tanzania Bara kuna wagonjwa wa akili milioni 7! Zanzibar kuna wagonjwa wangapi?
 
Msikilize Waziri huyu anavyotaja takwimu ndo utaamini kwamba tunaotuongoza wako ktk hali gani
 
Kwa mujibu wa Mtaalam wa Afya ya Akili Josefina Kaponya aliyeongea katika kipindi cha DW saa saba mchana 22/10/2022, kuna watu milioni saba nchini Tanzania bara wenye maradhi ya akili! Maana ya takwimu za mtaalam huyo ni kwamba zaidi ya asilimia kumi (10%) ya Watanzania milioni 60 wana matatizo ya akili!

Binafsi nina wasiwasi kuhusu taarifa hii, kama ni kweli ni hatari sana kwa nchi na ni lazima lifanyiwe kazi kwa umakini sana. Lazima tujiulize kama hali hii ni ya kawaida au ni kwa Tanzania tu? Na kwanini iwe hivyo?
Naona 10% kama ndogo ,mimi nahisi kama 80% ndio wana matatizo ya afya ya akili.
 
Nazani wako wengi zaidi yaapo
Kama ulisikia sababu zilizokuwa zikitolewa hata katika mataifa ya jirani ni mambo yanayoigusa jamii kwa kiwango kikubwa sana
 
Back
Top Bottom