Tanzania Bara iwekeze kwenye elimu kwanza.

Wana ukumbi.

Kwa hivi sasa kuna mengi sana yanayotokea huko Tanzania Bara na kwa mwenye akili ataona kikubwa kilichopo ni kukosa Elimu kwa watu wengi na kuingia kwenye Ushabiki pasi na kujua mwisho wake.

Mimi nashauri ni vizuri Serikali ya Tanzania Bara iwekeze zaidi kwenye ilmu ili kuwafanya vijana wake wawe sio tu wasomi lakin pia wenye uelewa wa kuelewa mwelekeo wa dunia ya leo. Hii itawafanya sio tu wawe makini na uzalendo wa kutetea nchi yao lakin pia kuwapa ujasiri na uthubutu wa kulinda mali zake.

Mfano mdogo ni nchi ya Zanzibar ambayo imewekeza sana katika Elimu na kujenga vyuo vikuu vitano ambavyo kwa mwaka wana graduate wanafunzi wa undergraduate 3500 mpaka 5000. Sasa ukitazama kwa nchi ndogo kama hii ambayo ina wakaazi wasiozidi milioni moja na nusu kupata matunda kama haya ni ukombozi wa hali ya juu sana.Hili limepelekea vija wa kizanzibar kuondoa tofauti zao za kisiasa na kutetea maslhi ya Taifa lao kwanza.


kama Tanzania Bara itajikita na kuwekez katika Ilmu basi nafikiri ushabiki wa sasa na uwogo uliopo kwa jamii kwa Serikali na kuburuzana na vyama vya kisiasa.

Kuwekeza kwenye ilmu ni bora zaidi kwa vijana kuweza kulinda, kutetea na kuhishimu mamlaka ya nchi na jamii nzima. Nashauri wa tanzania Bara mlione hilo.

Barubaru,
Nakubaliana kabisa na wewe. Bila elimu tunapoteza muda maana hakuna tutakachoweza kufanya na tunaanda bomu litakalolipuka baada ya muda mfupi. Ujinga ni balaa kubwa kwa nchi yeyote ile.
 
mkuu ni kutoweza tuu kupata picture ya kisemacho,sipendi sema unaanza thibitisha pia kuwa kifikra upo nyuma sana ya vyeti ulivyo navyo.

Hizo nchi na miji ni nortorius kwa chao za "barabarani" kule india Ng`ombe ana nafasi barabarani, bajaj, watembea kwa miguu, magari, tembo n.k. na wote wanafuata upenyo uliopo.Mifano yangu ipo sahihi sana tofauti na unavyoweza ikataa kirahisi tuu.Nimekuambia suala la magari barabarani,ni mamlaka na wala si la elimu ya darasani kwa raia.Hizo mamlaka ndio zinahitaji kuwa na watu wenye utaalamu wa mambo ya traffic flow.Raia wa kawaida ana mashinikizo ya maisha, ana majukumu na malengo ya kufikia kila siku,watu wa dar ni wa kutoka maeneo tofauti ya nchi na nchi jirani.Kwao lazima wafike na chakula nyumbani, wafikishe kiwango cha mwenye basi etc.Nimekupa mfano wa somalia,huweze enda wagawia chakula halafu useme kuwa wagawane kwa mpangilio.Kitakacho waongoza si elimu wala akili,il njaa na hamu ya kuchukua kingi kama akiba.

[/FONT]Majenngo? sidhani kama nimelinganisha majengo tuu..nimesema wametupita vitu vingi,nikitegemea utashi na elimu yako itakupelekea ku recaal couples ya uvijuavyo.Kma miundombinu, elimu(usitoe tuu mfano wa vyuo vya chini ila pia na vya juu ,kwani vya juu ubora wake hatuna Tanzania nzima).

Sijui unamaanisha nini kuhusu vyeti feki au pengine huelewi.Mi nafahamu feki ni kitu kisichotoka kwa mtengenezaji au mtoaji,ila kinaigiza kitu cha mtoaji halali.Kama unaaamisha feki kama cheti basi TCU inabdi waweke mashine ya kucheki vyeti.Vyeti feki ina maana huyo mtu ama hakusoma kabisa hiyo fani au hakufikia pata vyeti.Kama unataka leta nortion ya Feki kama elimu duni basi utakuwa umepota zaidi.

Elimu duni si vyeti feki, labda useme marks feki, au hata maksi zisizostahili.kama vile mtu kupewa maksi kza juu katika vyeti na katik kumbukumbu za computer kwa kutumia watu wa ndani.Haya yanaweza ambatana na feki.Hapo tutakaribiana kifikra kwani hapo ndipo ninaposema TCU hawajapashika.Hawan vipimo kuwa mwanafunzi alivujishiwa mitihani na walimu, au alipewa alama na mwalimu za bure katik assignments na hivyo kumjengea mazingira ya kupata madaraja ya juu pasipo kuwa na huo weledi.

Ukweli ni kwamba kuna shida sana katika mifumo inayotegemea marks za mwisho.Na hivyo kufanya thamani ya vyeti vitolewavyo na vyuo vingi kuwa hovyo. Na hii ipo kuanzia huko ulipo asia hadi Africa.Unachoongelea hapa ni kama kunishawishi niamini kuwa hela huweza nunua mapenzi kila mahali.

India ina spectrum ya ajabu sana, India in Polution kubwa sana inayokwenda kwenye billion, na ukubwa wa nchi unaifanya iwe kama bara(ni sub continent), kwa hiyo kuna kufanikiwa kwa ndani,yaani kampuni inaweza kuwa tajiri sana kwa kufanya biashara ndani ya india pekee.ratio ya matajiri na masikini kwa India ni ndogo sana, ila ktik hiyo fraction ukilinganisha idadi ya watanzania utaona ni watu wengi sana.Ila sehemu ya jamii iliyo na elimu kubwa si kubwa hivyo, na miji kama Mumbai inavuta wasomi wengi zaidi na hivyo kuifanya india ionekane kuwa ni ya wasomi ,ila kwa ujumla india kama taifa bado halijaelimika.Pakistani ndio taabu kabisa.

Hakuna anayekataa elimu ni ya msingi kwa afya na uhai wa any civilization.Ila hapa issue si hiyo hapa issue ni mlinganisho wako wa Zanzibar na Bara katika ratio ya vyuo .Ila katik ubora hujataka kubali ukweli kuwa Zanzibar wana mwendo mrefu hadi waweze ingiza elimu bora katik hayo majengo na taasisi za elimu.Ili watoe watu walio bora kama unavyotaka aminisha watu hapa.

Km wewe ni mmojawapo ya watu wanaoamini kuwa West waliiba elimu toka kwa waarabu,there is no doubt huwezi kuwa na fikra mbadal linapokuja suala za Zanzibar na Bara.Nilishawahai jiuliza kama taaluma zilitoka huko ulipo kwanini sasa wasiwe kwa kwanza kujua matumizi ya mafuta?kwanini basi wasiwe wa kwanza rusha rocket kwenda space?Ndugu yangu upo mbali sana na ukweli, naona umejisahau sana hadi kduharau watu kirahisi.

Usiwe naive ndugu yangu, katika hiyo mihadhara huwa unapewa platiform ambayo inakuwa one way traffic, huku watu wakiwa na shauku ya kukuona ,pia unaweza kuwa ulikuwa ukilindwa na timetable,kama kuna speakers wengine basi watu hawawezi ondoka kwani kwani kuna watu wengine wanafuatia.Pia ujue unaweza kuwa ulikuwa katik minajili ya dini na hivyo kuwafanya watu wasiangalie sana area nyingine.Hizo titles zako zilisaidia tuu watu wakusilikile ila si kwamba ulikuwa that credible.NAOMBA NEXT TIME INGIA KATIKA DIALOGUE NA WASOMI WENGINE halafu uone jinsi haukubaliki kihivyo.

Teh teh, niache uvivu gani tena wa computer halafu nitembelee website ya TCU?websiete yenyewe kwanza ni ya ubora wa chini sana.

Labda nikupe ukweli tuu ili taabu iishe, huko ungangani ulipo elimu yao ni mushkeli sana ndio maana sioni ajabu kuwa unaiona zanzibar ina elimu kubwa sana.Ni watu wangu wa karibu sana watoto wao wapo Tanzania wanasoma.Na wameweka wazi kabisa kuwa elimu yetu ipo juu sana kuliko ya huko ulipo.Na hii inatokana na watu misguided kama wewe.Mnajipigia debe na vyeti vyenu ,ahalfu mnakuja ongoza uongozi wa hizi taasisi.

Investment ya shule katik bara hasa kwa taasisi binafsi huwezi fananisha na zanzibar katik miaka ya karibuni.Labda wafungue milango wadau wengine wenye mitazamo tofauti waingie.Shida ni kwamba washauri kama ni aina yenu zanzibar aitabaki katik ndoto,na hawatajua wapi wamekosea.Watabaki kudhani wanafanyiwa hila.Nimeelezea shida nyingi za zanzibar naona umepiga kimya kwa vile hazina maslahi nawe katik hizi propaganda.Hizo shida ni baadhi tuu ya zinazoweza waletea wazenj uhuru wa kweli.

Kwa kweli umenichekesha sana. Siku zote tunaamini Mkataa kwao ni mtumwa.

Mimi naamini wazi ilmu ya Tz ipo juu sana kwani inamfundisha mwanafunzi mambo mengi sana ukilinganisha na western education. Tatizo ni mfumo unaotumika na kukosekana kwa vifaa bora na nyenzo bora za kufundishia. Na kwa hivi sasa huu udanganyifu na kukariri mitihani kunakofanywa na mamlaka zilizo na dhamana.

Kwa bahati mimi ni mmoja niliyesomea huko Bara kuanzia Mtendeni primary, Tambaza sec, Ilboru na UDSM. Zote nimesomea Tanzania lakin pia nimesomea Carleton University (Canada) na Sophia University ( Japan). Na ukisema mihadhara sio tu Oman au nchi za kiarabu lakin pia hata tanzania, Nigeria, USA, Uk Canada na kwingine kwingi tu. Hivi ninavyo ongea wiki mbili zijazo nitakuwa South Africa kwenye makongamano ya kitaaluma.

Nilichobaini kwako ni Dharau dhidi ya Mamlaka iliyopewa dhamana na nchi yako kisharia kusimamia suala la ilmu zote. Dharau hizo zimekufikisha kukata tamaa kimaisha na kuikatisha tamaa jamii yako. Nakumbuka last time nilikuja UDSM kwenye college ya Biashara nikawa naongea na mmoja wa sr lecturer ambaye alikuwa nyuma yangu nikiwa hapo. yeye aliniambia vijana siku hizi hawasomi kama enzi zetu ndio maana tunawashika sana. Nilifadhaika sana kwa hilo.

Nilimweleza kitu kimoja tu. Siku zote lecturer anapimwa kwa kiwango cha kufaulisha na sio kufelisha. kama wewe umewafundisha wanafunzi 40 na ulipotoa mtihani only 15 wakafaulu the rest wakafeli ujue kuwa haueleweki darasani hivyo huwezi kupandishwa cheo. Huo ni mfumo wa kisasa.

lakin kumbuka kuwa TCU ni taasisi iliyo makini na ipo na kufuata mitaala ya nchi za Madola. Ni chombo halali kisharia kilichowekwa na Serikali yako kupima ubora wa ilmu yenu na ndio maana ilmu yenu inakubalika katika nchi zote za madola.

sasa wewe kaa pembeni na kukejeli , pasi na shaka ndio wale wale wanaolalama bila kutoa suluhisho la problrms mlizonazo.

nakupa pole sana.

Lakinkumbuka Znz imewekeza sana na kuna vyuo vingine vitatu nafikiri baada miaka miwili vitakuwa njia moja kuongeza wasomi katika nchi hiyo ndogo yenye watu wasiopungua milioni moja na nusu. Je Bara mnajiweka vipi kwa hili la kuongeza wasomi ili muingia katika ushindani wa EAC.

 
Nia aibu kwa msomi kusema au kuandika maneno kama haya. Hii ni dalili ya uvivu wa kufikiri na kuwajibika na kujishughulisha kidogo.

Kwenye moja ya bandiko langu la mada hii nilibainisha SIKU ZOTE MTU MWENYE ILMU YA KUUNGAUNGA NA ISIYO SAHIHI anakuwa na mbwembwe nyingi sana. Lakin wewe imenibidi nikujibu sababu umebainisha kuwa umeingia kwenye panel za interview nyingi.

Kwa kukusaidia hapa nilitaka nikujulisha kuwa siku zote muomba anatanguliza kutuma CV kabla siku ya interview kupangwa na intervier wanatakiwa kupewa CV zile siku kadhaa kabla kukutana na muombaji. sasa kwa watu makini unatakiwa uifanyie kazi ile CV ikiwemo na kuhakiki usajili wa Vyuo alivyosoma kupitia tasisi maalum za kisharia za usajili wa vyuo hivyo nchini mwenu. Lakin pia hata kuwasiliana na vyuo kujua uhalali na usahihi wa cheti cha mwombaji. Ukisha jiridhisha na hilo ndio mtu anaitwa for the interview.

sasa nafikiri wewe unafanya kinyume ndio maana unatamka kitu kama hicho. Nakuomba ubadilike na kufuata mfumo halali unaotumiwa na wengi duniani na kuamini kile kilichokubaliwa na wengi.

Ndio maana hapo awali nilikwambia dunia ni kama kijiji kila kitu kipo hadhwarani. Vyuo vikuu karibu vyote vina tovuti na mail hivyo rahisi kuwasiliana navyo hata kikiwa uchina.

Jipambanue na ilimika kwa hilo. Ndio maana ninasema Ilmu ni muhimu sana kwa jamii.

kwa jinsi unavyopeteza muda kujitambuliasha kuwa umesoma na kuwaona wengine hawajui ni wazi kuwa.umeenda shule ila hujaelimika+ pride ndio kitu kinachokupoteza usijifunze na kuelewa mapya.

Hembu leta ushahidi wa kuthibitisha kwamba lazima ukisoma uelimike.Ndipo tuweke reference zetu sana.Yaani tufanya calibration.
 
Wewe kumbe hata hujui interview process yenyewe ikoje.Sasa mimi kama CEO unataka nipitie CVs za waombaji wote? Kweli? Hivi unajua ni applications ngapi hupokelewa mathalan kwa nafasi ya MHASIBU tu? Ni zaidi ya 100! Sasa hiyo due dilligence yako ikifanyika si itakuwa kazi? Hata hao finalist amabao napewa CVs zao bado ziwezi kusema ziko sawa kwa vile si wengi wanao ziandaa wenyewe kama waombaji. Again ntasimama kuwa CV haiwakilishi 100% uhalisia wa mtu.

Nafikiri ahali yangu unajichanganya.

Nilichobainisha hapo kwa stage ya juu. Kumbuka kuwa kuna watu ambao lazima wafanye hizo kazi za kuhakiki na ku short list wale walioweza kufaulu kwa vigezo vilivyowekwa. kama interviewer ni lazima apate CV hizo mapema ikiwa pamoja na uthibitisho wa Vyuo alivyosomea mwombaji kabla kuanza kumsahili.

haiwezekani kabisa kumsahili mtu kabla hajahakikiwa uhalali wa vyeti vyake kwani hilo linaweza kumwingiza pabaya yule interviwer pindi ikijulikana nae alishiriki kumwingiza kazini. Kama mtu ameajiriwa na vyeti feki basi hukma yake inaanzia kwa wote walioshiriki kumwajiri mtu huyo kuanzia utawala, interviwers etc.

lazima uwe makini kwa hilo.

 
Back
Top Bottom