Tanzania Bara iwekeze kwenye elimu kwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Bara iwekeze kwenye elimu kwanza.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Barubaru, Sep 3, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wana ukumbi.

  Kwa hivi sasa kuna mengi sana yanayotokea huko Tanzania Bara na kwa mwenye akili ataona kikubwa kilichopo ni kukosa Elimu kwa watu wengi na kuingia kwenye Ushabiki pasi na kujua mwisho wake.

  Mimi nashauri ni vizuri Serikali ya Tanzania Bara iwekeze zaidi kwenye ilmu ili kuwafanya vijana wake wawe sio tu wasomi lakin pia wenye uelewa wa kuelewa mwelekeo wa dunia ya leo. Hii itawafanya sio tu wawe makini na uzalendo wa kutetea nchi yao lakin pia kuwapa ujasiri na uthubutu wa kulinda mali zake.

  Mfano mdogo ni nchi ya Zanzibar ambayo imewekeza sana katika Elimu na kujenga vyuo vikuu vitano ambavyo kwa mwaka wana graduate wanafunzi wa undergraduate 3500 mpaka 5000. Sasa ukitazama kwa nchi ndogo kama hii ambayo ina wakaazi wasiozidi milioni moja na nusu kupata matunda kama haya ni ukombozi wa hali ya juu sana.Hili limepelekea vija wa kizanzibar kuondoa tofauti zao za kisiasa na kutetea maslhi ya Taifa lao kwanza.


  kama Tanzania Bara itajikita na kuwekez katika Ilmu basi nafikiri ushabiki wa sasa na uwogo uliopo kwa jamii kwa Serikali na kuburuzana na vyama vya kisiasa.

  Kuwekeza kwenye ilmu ni bora zaidi kwa vijana kuweza kulinda, kutetea na kuhishimu mamlaka ya nchi na jamii nzima. Nashauri wa tanzania Bara mlione hilo.
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu nitajie walau chuo kimoja tu ambacho kiko zanzibar kinajulikana nje ya wakazi wa zanzibar
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Madrasa navyo huitwa vyuo na vinajulikana sana huko afghastan na iraq........aah! Kimefunguliwa chuo kipua kinaitwa UAMUSHO zanzibar wamesoma hao..ila bara hatujasoma hatujui kiarabu na koran.
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Pengine ungeanza onyesha wapi wamefanya ushabiki pasipo kujua,halafu uje na ushahidi kuwa ni kukosekana kwa elimu.Halafu ndipo ulete ushauri wa elimu.

  Ni vyema pia ukajua kuwa mpaka sasa Tanzania hakuna mauhusiano ya elimu na kuelimika.Na hii si Bara tuu hata zenj.Kwani wasomi wa zenj ndio walewale waliotosa zanzibar.Ni walewake wanaoangalia na hata kupika machafuko yasiyoisha zanzibar.Machafuko hayo yamekuwa yakijibadili jina tuu,siku zote zanibar si shwari.Ushwari wake labda utakuwepo tuu katika masuala ya wizi wa mali za raia.Hapo zanzibar wameweza thibiti,ingawa pia inawezakuwa imechangiwa na hofu ya ushirikina zaidi ya kujua sheria.


  Pia mwandishi inabidi ajue kuwa itachukua muda kwa vyuo vya zanzibar kuwa na ubora,kwani katika kipindi hiki vitakuwa vinaathiriwa sana na matabaka na ubaguzi ulioota miziziz zanzibar.wanaoitwa watoto wa wakubwa, wanaoitwa wapemba na waunguja.Na tabia ya kulalamika kudai tuu, bila kujali kuwa kuna sehemu kila mtu nahitaji compromise kiasi fulani ili jamii ipanuke.
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhhhhhh!
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Barubaru,

  ..umejikita mno katika siasa.

  ..elimu itolewe ili wananchi waweze kuwa na ujuzi na utaalamu ktk fani mbalimbali.

  ..tuwe na mfumo unaowezesha sisi kama nchi kuweza kutambua vipaji vya watoto wetu, na kuviendeleza.

  ..kama mtoto ana kipaji cha ufundi basi apewe nafasi ya kusomea fani hiyo. kama kuna mwenye kipaji cha lugha asomee lugha, mwenye kipaji cha sayansi asomee sayansi etc etc.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Elimu bora haipimwi na idadi ya vyuo hata kidogo, Tanganyika vipo vyuo vingi saana tena vinavyotoa elimu katika ngazi ya degree,,,,,tatizovyuo vingi vimeanzishwa kisiasa,kishabiki na kwa kushindikana vyuo vyote vina matatizo ya msingi kama ifuatavyo,, havina walimu,, vifaa vya kufundishia, ufinyu wa budget wa kuviendesha,,,,,ufinyu wa majengo, uhaba mkubwa wa vitabu nk

  Wahitimu wanaotoka zanzibar naamini itawachukua miaka mingi kushindana na wenzao wanaotoka Kenya,Uganda kwani vyuo vikuu vilivyopozanziba NI VYUO KWA MAJINA TU KIUHALISIA HAVINA HADHI YA KUITWA VYUO HATA KIDOGO,, naadnika kitu nachokijua na kitu ambacho nimekiona

  Vyuo vya zanzibar havitambuliki popote waligomea hata TCU sasa sijui hao graduate unaojivunia nani atawaajiri?
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wizara ya elimu bado ipo nyuma cjui ni ufinyu wa bajeti au sera mbovu lkn pia sasa hakuna uzalendo hakuna anaejali next generetion itakuwa na sura gani ni huruma kwakweli
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .

  Kama ungekuwa na skuli hata ya Degree ya kwanza basi ungejua nini maana ya Chuo kikuu na ni wapi vinapata usajili.

  Ninavyozungumza kuna vyuo vikuu vitano vimesajiliwa na TCU ambacho ni chombo cha muungano katika kuhakiki ubora wa ilmu na mazingira ya vyuo vikuu huko Tanzania.

  Je ni nani asiyeijua State university of Znz , Znz university etc. Hivi ni vyuo ambavyyo vimetoa wanafunzi wengi sana na wengi tu wapo sehemu mbalimbali katika mashirika na taasisi za Muungano hususan katika fani za Uchumi, sharia na ualimu etc.

  Kumbuka kufahamika kwa University sio mbwembwe bali ni kwa zile product wanazozitoa nazo zimeshaanza kwa kasi sana kutoa matunda.

  Vile vile kukosa mahusiano ya ilmu na kuelimika ndio yanayowaletea wengi matatizo huko tanganyika. Kwani hata ukitembea barabarani utaona wale madereva wa daladala na bajaji wanavyo sababisha foleni kwa ima kukiuka taratibu na kanuni za udereva au kupuuza kutokana na kukosa ilmu.

  naamini wazi kama wote hawa wangeelimika kusingekuwa na foleni za kipumbavu huko tanganyika.

  Kuna mengi sana ambayo vijana wa KiZnz kwa ilmu iliyowekezwa na SMZ wameweza kujifunza na kufanya maisha kuwa rahisi sana hususan katika nyanja za siasa na kwengineko.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  State university of Zanzibar. na kuongezea kingine Zanzibar University. Pitia katika tovuti zao utajifunza mengi humo ikiwemo kuvijua zaidi na zaidi.
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Wewe utakuwa unaongelea toka Oman
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  kumbuka Dunia ni kama kijiji. Hakuna siri kila kitu hadhwarani.

  Msingi mkuu ni kuwekeza katika ilmu tu na sio siasa. Tz bara angalieni hilo kwanza kabla kufikiria mambo mengine.
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Okay kwa vile nyiye mshewekeza katika CUF
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Sidani kama nahitaji hiyo degree kujua hizo procedures za kuandikisha university+kujua ubovu wa mamlaka za viwango.

  Nadhani unahofia sana jina university, wakati nao pia wana hata mamlaka inayoandikisha meli zinazoua wazanzibar kila kukicha.Nao wanapiga kelele kuwa wana viwango.

  Sitaki waingilia hao jamaa wa TCU.Ila kutoaminiana kwa vyuo hadi kuwekea mizengwe kwa graduate wa chuo kimoja kwenda kingine ktk TZ ni kukubwa sana.

  Kuna vyuo kibao Tz havina lecturers wa viwango,wameagaliwa marks bila kujua wamezipata vipi.Matokeo yake vichekesho katika hivyo vyuo,wanafunzi wanajua walimu gani wababaishaji na wangapi kidogo wanaweza piga domo.Walimu wa vyuo vikuu wengi wanachojidai ni kuwa wanatoa reference +assignments+wanatangaza test,wanajua wanafunzi watakimbizana na kuleta majibu.Wengine ukiwapa hizo test na kuwapatia mwalimu wa nje jamaa hawapiti.Unaweza shangaa ila mika ya chuma walimu wa primary walisapewa mitihani ya wanafunzi wao ikawashinda.

  TCU hawapo hapo kama TBS wasivyo katik mfumo mzima wa production/manufacturing ila wanatokea katika final product.Pengine hata hizo sample wanaletewa zile za maonyesho.

  Sipendi Bishana na wewe ila jaribu pitapita katik walimu wa vyuo tena wa taaluma za computer halafu uangalie powerpoint presentations zao, zilivyo za ubora wa chini,halafu uniambie kama anaweza fikisha ujumbe sahihi kwa wanafunzi darasani.Achilia mbali uwezo wa kitaaluma katik kutumia vifaa vya kazi pamoja na kuwa mwepesi na huru kujibu n akujieleza darasani.Nadhani utaona kuamini kuwa TCU hawajafikia kuangalia elimu katik kila stage.Ndio maana tuna wasomi WA AKILI NDOGO KUENDESHA KUBWA.
  Mi sijui kama kuna zaidi ya chuo kikuu kimoja zanibar.Ndio unaeleza hapa.Naomba list vyote basi.
  teh teh..sitaki kupinga wala kuwa kikwazo katik juhudi zako za kueleza habari njema toka kisiwani.Ila tatizo ni kuwa umekuwa influenced na mitazamo fulani ya wasomi wa Zenj."Wanajitamani wenyewe" wanajiangalia katika vioo na kujipa viwango, halafu wanatafuta udhaifu mdogo kwa wengine wanautumia kujipa matumaini.Ndugu yangu zenj mna mmabo mengi sana yaliyo nje ya elimu yanayofanya elimu yenu isiwe reliable sana.Naamini mengi unayajua ila haupo tayari kuyasema.Elimu inaweza unganishwa na utalii ila elimu si utalii by itself,so utangaze kwa makini.
  Ndugu yangu foleni na daladala ndizo zimekufanya uone hivyo?Mbona kuna daladala nyingi za wapemba na unguja na madereva ni waho pia?Mbona mimi nimeona Uchafu unaweza kuwa ndio kukosa elimu kuliko na hayo yapo zaidi visiwani.Pamoja na udogo za Zenj ,hata mitaa yenye ukaribu na mji kabisa watu hawana vyoo?Daladala inaweza kuwa ni ukorofi tuu kwa vile tamaa,ubinafsi, shida za watu mwisho wa siku ndizo ziwafanyazo wajikute hivyo.Ila kukuwa na choo na kujihahatarisha kwa magonjwa ni ujinga zaidi.

  Sijui ni mitizamo tuu au ndio kuwa na mitizamo ambayo ni too confined, na kuwa na uelewa mdogo au ni kudharauliana bila sababu.Kwa mategemeo ya wengi kuwa PhD holders watakuwa na uwelewa wa kuridhisha,ila wabara huwa wanawashangaa sana wanaotoka visiwani,wanawaona kama vile misukule fulani.Pengine na wao wakirudi huko huja na mijisifa kibao kuwa wanakubalika na mengine,hivyo kuwafanya watu mliobanwa huko kutamani baki visiwani na mara mkitoka jicho lenu huwa kama vile wale jamaa wa ubishi wa dini huwa wanasoma vipande vya mistari kwa staili ya kuwasaidia ubishi"negatively".

  Hata wale jamaa wa UDSM na Muhimbili hawachoki piga domo kuwa elimu ya US ni ndogo kuliko ya Bongo,ila wenzao wanachana ubongo, wanabadili sura za watu, na mengineyo.


  By the way ukienda South East Asia,India,malaysia, indonesia, philipines, vietnam,thailand, pakistan etc tena katik miji mikuu kama Mumbai,Delhi,manill etc utaona jinsi gani sisi tuna afadhali ingawa hatuwezi shindana na hizo nchi kwa mambo mengi.

  Kukusaidia tuu ni kwamba masuala ya barabara na misongamano katika miji ni suala la mamlaka ya mipango miji.Miji iliyo na watu wengi wasio na hakika ya maisha, na walio katika hofu ya kutomiza malengo ya jioni ni kama kudondosha chakula somalia, hakuna atakayesubiri wapokee mmoja moja wakati hana hakina kuwa ikifika zamu yake atakuta kitu.
  Endelea amini hivyo ndugu yangu kwnai kuna faida kwa usalama wa nchi.Amini kama watanzania walivyokuwa wakiaminishwa kuwa legacy newspapers kama uhuru na mzalendo, sijui na daily news, ndio magazeti bora na yenye weledi..ila sijui hata rangi zake nasikia tuu watu walilalaa kuwa yanapiga story sana.

  Sijui unamaanisha nia ya SMZ ambayo siwezi pinga kwa vile siwezi isema.Ila kuna mengi wasomi wa Zenj wamewaangusha,wamewadhalilisha, wameitosa zenj,kupitia siasa na propaganda.Ila waulize hao viongozi kwanini wanapenda kula maisha dar?Uliza vizuri ubaguzi uliopo huko.Pengine utabisha kiushabiki au upo katika madhabahu na unakula vyema na wenye madhabahu.

  Zanzibar ipo na watu wa lost generation,zanzibar moral standards zimeshuka,huku wakiamini kuwa wapo juu.Pengine mzanzibar anaweza jivunia kwa kuwa na sheria mapema za haki za binadamu ila hawezi jua ni kwanini ziliwekwa tena chini ya watawala wasioheshimu haki za binadamu.Zanzibar wangekuwa jamii ya uwazi kama za ulaya pangekuwa na kashfa kuliko za ulaya(ushoga, ubakaji na udhalilisaji wa watoto).Unicef na mashirika mengine yalikuwa na report za kutisha kuhusu udhalilishaji wa kingono/ukabaki katika madrassat, na school hadi serikali haikuweza pinga sheria kuwekwa.Sijui kama story ilikuwa hivyo katika macho yenu?

  Nimekuwa zanzibar sana na nimeongea na watu, nimesikiliza watu wakiongea, nimesikia tafsiri zao za haki hata kwa wale wanaolia kuwa ni wapenda haki,nimesikiliza mitazamo yao juu ya watu wa bara, ..napata huruma.Ndipo napata picture kwanini viongozi wa Zanzibar wakiingia katik Muungano huwa wanajenga dar ili wakae mbali na watu wao.Kwa vile wanahisi hawawezi wabadili watu na ni bora wawatumie hivyohivyo, wawape habari wazipendazo kuzisikia.Nawalaumu kw ahilo kwa vile wanazidi waharibu na mwisho kuja waachia viongozi wajao watu wasioongozeka.
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nakupa changamoto kidogo . hebu pitia tovuti ya bunge lenu la Muungano na angalia CV za wabunge wote wa CUF uzione na ujaribu kuzilinganisha na wale wanaotoka Bara iwe CCM au hata Chadema uone wapi wapo juu.

  Nafikiri ukiliona hilo utaona umuhimu mkubwa wa kuwekeza katika Ilmu.

   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nicholas,

  Ahali yangu naona umeongea mambo mengi sana. Lakin kwa mtu makini anakuona kabisa unatoka nje ya mada. Mimi nimejaribu kufanya comparison ya Tanganyika na Znz katika nyanja ya Ilmu kwa kuweka vigezo sahihi kabisa toka nchini kwako. Nimebainisha kuwa vyou nilivyovitumia vyote vimesajiliwa na TCU. sasa kama wewe unaidharau TCU basi utakuwa mtu wa ajabu sana. Kwani hicho ni chombo kilichowekwa chini ya sharia za nchi yyenu kusajili na kuangalia ubora wa ilmu ya juu kwa nchi yenu. Hapa inajidhihirisha kuwa unaongea kwa kukata tamaa.

  Umebainisha vitu vingi sana ikiwemo pamoja na kuangalia uzuri wa majengo. Ndugu yangu kama ungepata kutembelea India au Pakistan au Singapore na malaysia kama ulivyozitaja. Labda nikupe ungepata nahati ya kuziona University za Delhi university, au old Delhi university, au haya Othmania ambayo ipo AP (Hydrabad ) au hata Bangalore university (Karnataka state)kisha ukatazama colleges zake nafikiri usingesema au kuandika unachoandika. Cha msingi ni kuangalia ubora wa ilmu inayotolewa kwani siku zote penye ilmu hakuna ubabaishaji. Mbabaishaji siku zote ni mwenye vyeti feki au mwenye kupata degree za kwenye chupi.

  Lakin vile vile katika miji hiyo uliobainisha pamoja na kuwa watu ni wengi sana na vyombo vya moto ni vingi sana lakin utaona madereva wake kwa kuwa wengi ni wasomi basi hata uendeshaji wao ni ule wenye kufuata sharia za barabarani. tembelea miji kama Lahore au islamabad Pakistan, Miji kama Hydrabad, Bangalore, madras, Bombay, au Delhi utaliona hilo.

  Mimi nakushauri kwani mimi ni mmoja kati ya watu niliopitia vyuo vingi iwe kwa kusoma au hata kutoa miadhara ya kitaaluma. Nimeliona hilo na nalibainisha bila kuuma maneno. Kuwa kuwekeza kwenye ilmu ni bora sana kwani kunaipambanua jamii iwe ni yenye kuelewa na kutetea maslahi yake.

  Lakin la mwisho nakushauri uache uvivu wa kutumia Computer yako na mtandao. Wewe tembeleo tovuti ya TCU angalia vyuo vilivyosajiliwa.

   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya mimi siamini sana CV ya mtu. Its just another piece of paper. Nimekaa katika panel za interviews nyingi (ikiwemo Zanzibar pia) na nimeshuhudia CV inavyoweza kukosa uhalisia wa mtu. Hiyo ya bunge ndio sitaki kuisikia kabisa
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Nia aibu kwa msomi kusema au kuandika maneno kama haya. Hii ni dalili ya uvivu wa kufikiri na kuwajibika na kujishughulisha kidogo.

  Kwenye moja ya bandiko langu la mada hii nilibainisha SIKU ZOTE MTU MWENYE ILMU YA KUUNGAUNGA NA ISIYO SAHIHI anakuwa na mbwembwe nyingi sana. Lakin wewe imenibidi nikujibu sababu umebainisha kuwa umeingia kwenye panel za interview nyingi.

  Kwa kukusaidia hapa nilitaka nikujulisha kuwa siku zote muomba anatanguliza kutuma CV kabla siku ya interview kupangwa na intervier wanatakiwa kupewa CV zile siku kadhaa kabla kukutana na muombaji. sasa kwa watu makini unatakiwa uifanyie kazi ile CV ikiwemo na kuhakiki usajili wa Vyuo alivyosoma kupitia tasisi maalum za kisharia za usajili wa vyuo hivyo nchini mwenu. Lakin pia hata kuwasiliana na vyuo kujua uhalali na usahihi wa cheti cha mwombaji. Ukisha jiridhisha na hilo ndio mtu anaitwa for the interview.

  sasa nafikiri wewe unafanya kinyume ndio maana unatamka kitu kama hicho. Nakuomba ubadilike na kufuata mfumo halali unaotumiwa na wengi duniani na kuamini kile kilichokubaliwa na wengi.

  Ndio maana hapo awali nilikwambia dunia ni kama kijiji kila kitu kipo hadhwarani. Vyuo vikuu karibu vyote vina tovuti na mail hivyo rahisi kuwasiliana navyo hata kikiwa uchina.

  Jipambanue na ilimika kwa hilo. Ndio maana ninasema Ilmu ni muhimu sana kwa jamii.
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Wewe kumbe hata hujui interview process yenyewe ikoje.Sasa mimi kama CEO unataka nipitie CVs za waombaji wote? Kweli? Hivi unajua ni applications ngapi hupokelewa mathalan kwa nafasi ya MHASIBU tu? Ni zaidi ya 100! Sasa hiyo due dilligence yako ikifanyika si itakuwa kazi? Hata hao finalist amabao napewa CVs zao bado ziwezi kusema ziko sawa kwa vile si wengi wanao ziandaa wenyewe kama waombaji. Again ntasimama kuwa CV haiwakilishi 100% uhalisia wa mtu.
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280

  mkuu ni kutoweza tuu kupata picture ya kisemacho,sipendi sema unaanza thibitisha pia kuwa kifikra upo nyuma sana ya vyeti ulivyo navyo.

  Hizo nchi na miji ni nortorius kwa chao za "barabarani" kule india Ng`ombe ana nafasi barabarani, bajaj, watembea kwa miguu, magari, tembo n.k. na wote wanafuata upenyo uliopo.Mifano yangu ipo sahihi sana tofauti na unavyoweza ikataa kirahisi tuu.Nimekuambia suala la magari barabarani,ni mamlaka na wala si la elimu ya darasani kwa raia.Hizo mamlaka ndio zinahitaji kuwa na watu wenye utaalamu wa mambo ya traffic flow.Raia wa kawaida ana mashinikizo ya maisha, ana majukumu na malengo ya kufikia kila siku,watu wa dar ni wa kutoka maeneo tofauti ya nchi na nchi jirani.Kwao lazima wafike na chakula nyumbani, wafikishe kiwango cha mwenye basi etc.Nimekupa mfano wa somalia,huweze enda wagawia chakula halafu useme kuwa wagawane kwa mpangilio.Kitakacho waongoza si elimu wala akili,il njaa na hamu ya kuchukua kingi kama akiba.

  Majenngo? sidhani kama nimelinganisha majengo tuu..nimesema wametupita vitu vingi,nikitegemea utashi na elimu yako itakupelekea ku recaal couples ya uvijuavyo.Kma miundombinu, elimu(usitoe tuu mfano wa vyuo vya chini ila pia na vya juu ,kwani vya juu ubora wake hatuna Tanzania nzima).

  Sijui unamaanisha nini kuhusu vyeti feki au pengine huelewi.Mi nafahamu feki ni kitu kisichotoka kwa mtengenezaji au mtoaji,ila kinaigiza kitu cha mtoaji halali.Kama unaaamisha feki kama cheti basi TCU inabdi waweke mashine ya kucheki vyeti.Vyeti feki ina maana huyo mtu ama hakusoma kabisa hiyo fani au hakufikia pata vyeti.Kama unataka leta nortion ya Feki kama elimu duni basi utakuwa umepota zaidi.

  Elimu duni si vyeti feki, labda useme marks feki, au hata maksi zisizostahili.kama vile mtu kupewa maksi kza juu katika vyeti na katik kumbukumbu za computer kwa kutumia watu wa ndani.Haya yanaweza ambatana na feki.Hapo tutakaribiana kifikra kwani hapo ndipo ninaposema TCU hawajapashika.Hawan vipimo kuwa mwanafunzi alivujishiwa mitihani na walimu, au alipewa alama na mwalimu za bure katik assignments na hivyo kumjengea mazingira ya kupata madaraja ya juu pasipo kuwa na huo weledi.

  Ukweli ni kwamba kuna shida sana katika mifumo inayotegemea marks za mwisho.Na hivyo kufanya thamani ya vyeti vitolewavyo na vyuo vingi kuwa hovyo. Na hii ipo kuanzia huko ulipo asia hadi Africa.Unachoongelea hapa ni kama kunishawishi niamini kuwa hela huweza nunua mapenzi kila mahali.
  India ina spectrum ya ajabu sana, India in Polution kubwa sana inayokwenda kwenye billion, na ukubwa wa nchi unaifanya iwe kama bara(ni sub continent), kwa hiyo kuna kufanikiwa kwa ndani,yaani kampuni inaweza kuwa tajiri sana kwa kufanya biashara ndani ya india pekee.ratio ya matajiri na masikini kwa India ni ndogo sana, ila ktik hiyo fraction ukilinganisha idadi ya watanzania utaona ni watu wengi sana.Ila sehemu ya jamii iliyo na elimu kubwa si kubwa hivyo, na miji kama Mumbai inavuta wasomi wengi zaidi na hivyo kuifanya india ionekane kuwa ni ya wasomi ,ila kwa ujumla india kama taifa bado halijaelimika.Pakistani ndio taabu kabisa.
  Hakuna anayekataa elimu ni ya msingi kwa afya na uhai wa any civilization.Ila hapa issue si hiyo hapa issue ni mlinganisho wako wa Zanzibar na Bara katika ratio ya vyuo .Ila katik ubora hujataka kubali ukweli kuwa Zanzibar wana mwendo mrefu hadi waweze ingiza elimu bora katik hayo majengo na taasisi za elimu.Ili watoe watu walio bora kama unavyotaka aminisha watu hapa.

  Km wewe ni mmojawapo ya watu wanaoamini kuwa West waliiba elimu toka kwa waarabu,there is no doubt huwezi kuwa na fikra mbadal linapokuja suala za Zanzibar na Bara.Nilishawahai jiuliza kama taaluma zilitoka huko ulipo kwanini sasa wasiwe kwa kwanza kujua matumizi ya mafuta?kwanini basi wasiwe wa kwanza rusha rocket kwenda space?Ndugu yangu upo mbali sana na ukweli, naona umejisahau sana hadi kduharau watu kirahisi.

  Usiwe naive ndugu yangu, katika hiyo mihadhara huwa unapewa platiform ambayo inakuwa one way traffic, huku watu wakiwa na shauku ya kukuona ,pia unaweza kuwa ulikuwa ukilindwa na timetable,kama kuna speakers wengine basi watu hawawezi ondoka kwani kwani kuna watu wengine wanafuatia.Pia ujue unaweza kuwa ulikuwa katik minajili ya dini na hivyo kuwafanya watu wasiangalie sana area nyingine.Hizo titles zako zilisaidia tuu watu wakusilikile ila si kwamba ulikuwa that credible.NAOMBA NEXT TIME INGIA KATIKA DIALOGUE NA WASOMI WENGINE halafu uone jinsi haukubaliki kihivyo.

  Teh teh, niache uvivu gani tena wa computer halafu nitembelee website ya TCU?websiete yenyewe kwanza ni ya ubora wa chini sana.

  Labda nikupe ukweli tuu ili taabu iishe, huko ungangani ulipo elimu yao ni mushkeli sana ndio maana sioni ajabu kuwa unaiona zanzibar ina elimu kubwa sana.Ni watu wangu wa karibu sana watoto wao wapo Tanzania wanasoma.Na wameweka wazi kabisa kuwa elimu yetu ipo juu sana kuliko ya huko ulipo.Na hii inatokana na watu misguided kama wewe.Mnajipigia debe na vyeti vyenu ,ahalfu mnakuja ongoza uongozi wa hizi taasisi.

  Investment ya shule katik bara hasa kwa taasisi binafsi huwezi fananisha na zanzibar katik miaka ya karibuni.Labda wafungue milango wadau wengine wenye mitazamo tofauti waingie.Shida ni kwamba washauri kama ni aina yenu zanzibar aitabaki katik ndoto,na hawatajua wapi wamekosea.Watabaki kudhani wanafanyiwa hila.Nimeelezea shida nyingi za zanzibar naona umepiga kimya kwa vile hazina maslahi nawe katik hizi propaganda.Hizo shida ni baadhi tuu ya zinazoweza waletea wazenj uhuru wa kweli.
   
Loading...