Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,526
- 19,381
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM), Mkoa wa Arusha, imemchangia Rais Jakaya Kikwete sh milioni moja kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais Oktoba ikiwa ni kumuunga mkono juhudi zake za uongozi bora. Fedha hizo zilikabidhiwa jana na Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James ole Millya, kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati , katika hafla ya kumsimika Kamanda wa Vijana wa Wilaya ya Longido, Michael Lekule Laizer .
Akikabidhi fedha hizo, Millya alisema hatua hiyo inaonyesha imani waliyonayo kwa mwenyekiti wao kutokana na kutambua uongozi wake tangu alipoingia madarakani.
Millya alisema mchango huo unaonyesha imani kubwa waliyonayo vijana kwa Rais Kikwete ambaye amesimamia vilivyo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM hivyo vijana kwa kutambua uwezo wake wameamua kumchangia fedha hizo kwa ajili ya kuchukulia fomu ili agombee kwa kipindi cha pili.
Mwenyekiti huyo, aliyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za UVCCM, katika hafla hiyo ya kumsimika Mbunge wa Jimbo la Longido, Michael Lekule Laizer, kuwa kamanda wa vijana wa wilaya hiyo.