Tanzania Bado Tuna Ujinga Mwingi.

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,502
19,341
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM), Mkoa wa Arusha, imemchangia Rais Jakaya Kikwete sh milioni moja kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais Oktoba ikiwa ni kumuunga mkono juhudi zake za uongozi bora. Fedha hizo zilikabidhiwa jana na Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James ole Millya, kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati , katika hafla ya kumsimika Kamanda wa Vijana wa Wilaya ya Longido, Michael Lekule Laizer .
Akikabidhi fedha hizo, Millya alisema hatua hiyo inaonyesha imani waliyonayo kwa mwenyekiti wao kutokana na kutambua uongozi wake tangu alipoingia madarakani.
Millya alisema mchango huo unaonyesha imani kubwa waliyonayo vijana kwa Rais Kikwete ambaye amesimamia vilivyo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM hivyo vijana kwa kutambua uwezo wake wameamua kumchangia fedha hizo kwa ajili ya kuchukulia fomu ili agombee kwa kipindi cha pili.
Mwenyekiti huyo, aliyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za UVCCM, katika hafla hiyo ya kumsimika Mbunge wa Jimbo la Longido, Michael Lekule Laizer, kuwa kamanda wa vijana wa wilaya hiyo.
 
Kwa vile ni uchaguzi wao wa ndani siwezi kuwalaumu sana lakini labda cha kuuliza kama si moja ya kampeni ambayo imekemewa na mwenyekiti wake kwani wamejuaje JK atachukua tena fomu ya kugombea au naye ameshatangaza nia maana karuhusu wabunge kutangaza nia lakini si kufanya kampeni ila yeye sijasikia kama katangaza nia au ni mazoea kuwa whatever the case atapewa tu kipindi kingine
 
kichuguu
huu ujinga wa waTanzania sidhani kama utatoka, pamoja na ahadi zote zilizoshindwa kutekelezeka hata nukta moja, lakimni bado watu wanchangishana kumpa kikwete
hamu sina
 
Vyama vingine navyo vikihamua kuwachangia viongozi wao nao watakuwa wajinga au....!?
 
Vijana ni CCM,pesa wametoa mifukoni mwao,waliomchangia ni mwenyekiti wao,kwa mapenzi yao na mtazamo wao kuwa anafaa kuendelea kuwa Rais.
Tatizo liko wapi?
 
Hao vijana wamejaribu kuwaiga Chadema

vijana wa chadema wao wanadumisha zidumu fikra za mwenyekiti
wa CCM wanadumisha adumu mfalme Kikwete

UVCCM wamecopy Chadema ila wameenda mbali zaidi LOL!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/45980-freeman-mbowe-award-from-bavicha.html

hii ishu ya vijana kujikomba kwa wenyeviti ina maelezo mengi sana, mwenye masikio na asikie neno hili ambalo hali halisi inawaeleza watu fulani

Hapa tunaongelea UVCCM kumchangia JK nauli ya kuingia ikulu hayo ya Chadema yanatoka wapi ina maana kila baya linalofanywa na CCM wanacopy toka Chadema na zuri linalofanywa na CCM huwa wanacopy wapi CUF, kila Chama kibebe mzigo wake kama ni mzuri mbaya watajijua
 
Hapa tunaongelea UVCCM kumchangia JK nauli ya kuingia ikulu hayo ya Chadema yanatoka wapi ina maana kila baya linalofanywa na CCM wanacopy toka Chadema na zuri linalofanywa na CCM huwa wanacopy wapi CUF, kila Chama kibebe mzigo wake kama ni mzuri mbaya watajijua

!!!!!, theory yako kila chama kibebe mzigo wake ni nzuri

wenye viti wa hivi vyama ni madikteta, na wafuasi wana njaa, ndio kujikomba hivyo, sasa kama Luteni wewe mpenzi tu uko hivi, je anayetegemea kula na kunywa kutoka kwa Mbowe na Kikwete atafanyaje?

ebu we piga picha tu!
 
Sijaelewa hapo ujinga ni upi.

As long as mfumo wa sasa upo in place, huezi ukapinga dalili badala ya chanzo cha dalili.
 
!!!!!, theory yako kila chama kibebe mzigo wake ni nzuri

wenye viti wa hivi vyama ni madikteta, na wafuasi wana njaa, ndio kujikomba hivyo, sasa kama Luteni wewe mpenzi tu uko hivi, je anayetegemea kula na kunywa kutoka kwa Mbowe na Kikwete atafanyaje?

ebu we piga picha tu!

Mimi ni mpenzi si shabiki ni mwanaharakati na mpenda maendeleo wa chama chochote kile kiwe cha upinzani kiwe chama tawala ndiyo maana hapa nimesema UVCCM hawajakosea kama katiba yao inawaruhusu vile vile huwa na wa support sana CUF hasa CUF zanzibar lakini wewe whatever Chadema Mbowe na Slaa wafanye huwa una wajudge negatively kitu ambcho huwa nakupinga wazi wazi sijifichi
 
JK ni kiongozi smart, mpeni nafasi nyengine apate kumaliza kazi aliyoianza ya kupambana na ufisadi :cool:
 
Back
Top Bottom