Tanzania bado ni nchi ya amani

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,227
113,583
Nimeanza kuona na kusikia vijimaneno maneno hususan humu kwenye mitandao kwamba sasa Tanzania siyo nchi ya amani.

Mimi sikubaliani kabisa na hiyo dhana. Nakataa kabisa. Tanzania bado ni nchi ya amani.

Matokeo machache ya watu kupoteza maisha yao au kushambuliwa kwa risasi hakuifanyi nchi kwa ujumla wake isiwe na amani.

Wote wanaodai kuwa Tanzania siyo nchi ya amani sijui wao wanaishi dunia gani maana nchi zisizo na amani zipo tele tu.

Huko kwenye hizo nchi watu hufa kwa mafungu mafungu. Unakuta watu 200 wanauliwa kwa kulipuliwa na mabomu kanisani au msikitini, mara usikie watoto 100 wa shule za chekechea wameuliwa kwa mpigo, mara sijui bomu limelipuka katikati ya mji wa Baghdad na kuua watu 90 papo hapo, na kadhalika, na kadhalika.

Sasa ni lini hapa kwetu mmewahi kusikia mambo kama hayo?

Nani kati yenu ana wasiwasi na usalama wa mwanae kesho hapo shuleni kwao?

Nani kati yenu ana hofu ya kwenda msikitini Ijumaa akiogopa usalama wake? Nani hatokwenda kanisani ifikapo Jumapili kisa tu anahofu na hali ya usalama?

Nani hatoenda sokoni kwa kuhofia huenda akauliwa akiwapo huko?

Nani kaahirisha mipango yake ya kwenda baa au sehemu zingine za starehe kisa amani hakuna?

Hata kwenye nchi zenye amani watu hufa. Na hufa kwa sababu mbalimbali.

Hata kwenye nchi zenye amani matendo maovu huwepo. Na ndo maana kunakuwepo na vyombo vya ulinzi na usalama.

Popote pale penye binadamu uovu nao huwepo.

Lakini yote hayo hayaifanyi nchi kwa ujumla wake isiwe nchi yenye amani.

Kama mnadhani Tanzania sasa amani hakuna basi hamieni Damascus huko. Au nendeni Kabul au Kandahar huko. Nendeni Lahore huko. Kama vipi mnaweza hata kwenda Somalia tu hapo kama huko kwingine mtapaona ni mbali.

Nendeni huko mkaishi kwa amani. Naamini mtakuwa salama zaidi huko kwani Tanzania sasa haina amani tena!
 
Amani ni hali ya raha na salama bila ugomvi; ni kinyume cha fujo au vita.

Mara nyingi hali za amani ya nje na amani ya ndani hutofautishwa.


Amani ya nje au amani ya kisiasa na kijamiiEdit

Amani ya kisiasa ni hasa kutokuwa na vita na mapigano kati ya nchi mbalimbali au kati ya vikundi ndani ya jamii. Kama kuna mgongano kutokana na tofauti ya upendeleo juu ya jambo fulani amani inatunzwa kama pande zote zinafuata sheria au kanuni za jamii bila kutumia mabavu.

Mara nyingi maana kuu ya "amani" ni hali ya kutokuwa vita kati ya nchi kwa sababu vita huleta uharibifu mkubwa kushinda aina nyingine za ugomvi.

Amani inaweza kutaja pia tendo la kumaliza vita kwa njia ya mapatano kati ya washiriki wa vita au pia kati ya washindi na washindwa wakikubali kumaliza uadui. (linganisha Amani ya Westfalia).

Tangu vita kuu za dunia kulikuwa na majaribio mengi kuhakikisha amani kwa njia ya mapatano kati ya nchi zote za dunia. Shirikisho la Mataifa lilianzishwa mwaka 1919 likashindwa kuzuia vita kuu ya pili ya dunia ikafuatwa na Umoja wa Mataifa ulio na shabaha ya kupunguza na kuzuia vita kwa njia ya ushirikiano.

Tunatakiwa kulinda amani ili kusonga mbele hata kiuchumi.
 
Matokeo machache ya watu kupoteza maisha yao au kushambuliwa kwa risasi hakuifanyi nchi kwa ujumla wake isiwe na amani.
Itapendeza vizuri zaidi Na itafaa zaidi Kama utachapwa risasi wewe utekwe na kupotezwa halafu utelekezwe pasipo kupewa Huduma yoyote unayositahili kupewa halafu uendelee kusema maneno haya ndipo maneno yako yatakapokuwa na maana zaidi kwa kuwa yanatoka kinywani mwamuhanga.
 
Itapendeza vizuri zaidi Na itafaa zaidi Kama utachapwa risasi wewe utekwe na kupotezwa halafu utelekezwe pasipo kupewa Huduma yoyote unayositahili kupewa halafu uendelee kusema maneno haya ndipo maneno yako yatakuwa na maana zaidi kwa kuwa yanatoka kinywani mwamuhanga.

Wewe ushawahi kutekwa na kutandikwa risasi?
 
Ngoja mtoto wako aje afe kwa risasi halafu polisi wa Tanzania watakwambia alikuwa jambazi sugu linalotafutwa ndio utaona amani ya nchi hii ilivyo.
Sasa mkuu vifo vingine ni mipango ya mungu tu... Nchi yetu hii democracy ndo ina shida
 
Naunga mkono hoja Tanzani bado ni nchi ya amani......najua mtakuja tu na mlivyozoea matusi siku hizi karibuni.
 
Nyani ngabu kwa akili yako ndogo uko sahihi kwani wenye akili za kuazima kama wewe hawajui maana ya amani na hutakaa ujue. Tunakusamehe bure huenda ipo siku kwa msaada wetu ukaja kujitambua.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom