Tanzania bado kuna Ombwe la media kwenye eneo la mahojiano

ALFRED RINGI

Member
Nov 2, 2016
17
26
Uandishi wa habari ni sanaa(arts),ila mahojiano ni sayansi(science),katika kazi ya uandishi wa habari,changamoto kubwa tunayokutana nayo ni namna ya kumhoji chanzo kigumu(difficult source),mfano Marehemu Mchungaji Mtikila ama mzee Mkinga Mkinga!.

Chanzo kigumu anaweza kuwa mgeni ambaye

1.Anamajibu mafupi sana

2.Anaongea sana bila kukupa nafasi

3.Hajibu maswali yako,yeye ukimuuliza hili anakuja na majibu yake

4.Anakuja na ajenda yake mfukoni,mfano kumshambulia mtu,taasisi,kikundi cha watu ama serikali(ambaye anaweza toa kauli ya uongo,uchochezi ama udhalilishaji)

Kabla ya kwenda kumhoji ni vizuri ukawa umaandaa......
1.Basic questions,haya humfanya mgeni wako ayazoee mahojiano,humtoa hofu mgeni ayaone mahojiano kama sehemu salama kwake!.

2.Surprise questions,haya humfanya mgeni ashangae na kuamini unamfahamu kwa undani mpaka maisha yake binafsi!.Hapa unaweza muuliza mgeni swali kuhusu maisha yake wakati akiwa mfano mwanafunzi wa sekondari huku ukimtajia jambo ambalo alilifanya na yeye atabaki kujiuliza umejuaje?

Mfano:Wakati ukiwa mwanafunzi wa darasa la saba na picha yako ni hii,siku moja ulifanya vizuri sana na mzazi wako akaitwa kupewa pongezi,tukio lile limechangia vipi wewe kuwa hapa?

Au Maisha yako ya chuo kikuu yalikutambulisha kama kijana mkimya sana,lkn leo unatamba na ni maarufu,mgeni wako atajua kuwa wewe unamfahamu kwa undani na katu hataweza kukupa majibu ya uongo!.

3.Packaged questions,haya humfanya mgeni na watazamaji/wasikilizaji wakuamini kuwa umesoma na kufanya utafiti wa hali ya juu juu ya mada husika,aina hii ya maswali hujengwa na takwimu,rejea,ushahidi wa nyaraka na mifano halisi kuhusu mgeni wako ama mada!

Mfano,tarehe 22.March.2017,ulinukuliwa na gazeti la serikali ukisema ........Or Kwa mujibu wa utafiti wa,.....Ushahidi unaonesha kuwa wewe,hapa lazima uwe na nyaraka itakayokusaidia kumbana mgeni wako ili asikukwepe!.

4.Tough questions.,maswali haya huwa mafupi na huitaji majibu mafupi yenye kujikita kwenye hoja,aina hii ya maswali huitaji majibu ya moja kwa moja,hapa hutoa nafasi kwa mgeni kujieleza mnoo nan hata kuweka blabla!.

Mara nyingine maswali haya huandaliwa mapema na hulenga kumrejesha mgeni kwenye mstari na kuepusha mgeni kuja na mambo mengiiiiii yasiyo sehemu ya kipindi!.

5.Follow up questions,haya ni maswali ambayo wewe muongoza mahojiano huyaandai,huja kutokana na majibu ya mgeni wako,unatakiwa akili yako na masikio yako kwa asilimia 100,yawe kwa mgeni wako anasema nini?pale unapoona mgeni kaeleza jambo lenye utata na linahitaji ufafanuzi,usijikite kwenye maswali uliyoandaa,zakisha swali kutoka kwenye maelezo ya mgeni wako ili kuondoa utata wa maelezo yake!.

Mbinu ya kuuliza maswali hutegemea mazingira,waweza tumia!.

1.Shotgun,mbinu hii mara nyingi hutumika kumnyima mgeni muda wa kuzungumza sana,mbinu hii hutumika kwa mgeni mwenye blabla nyingi au ambaye ana ajenda yake mfukoni na anataka kuipenyeza hewani!.

2.Space,hii ni mbinu ambayo hutumika sana pale unapokuwa na mgeni ambaye unamwamini,hana blabla,hawezi toa matamshi hatarishi hewani ,mfano kutukana ama kumdhamilisha mtu hewani!.Hatakuwa na tabia ya kuhama kwenye hoja,majibu yake ni kutokana na unavyomuuliza.

NB,Mahojiano ninuwasilishaji wa Ukweli(facts),Takwimu(data),Ushahidi(Evidence).
 
Waandishi wa habari na watangazaji, kuchukueni dhahabu hiyo hapo ya bureee
 
Unena vema kabisa ktk mada yako. Nakubaliana na wewe na hapo ndipo napowakumbuka watangazaji kama Tim Sebastian wa Hard talk BBC au Christiane Amanpour wa CNN au Hata Larry King wa CCN ingawa amestaafu,Pascal Mayala wa Kitimoto live ITV enzi hizo n.k
 
Mfano kipindi cha dakika 45 cha ITV kimekosa mtu wa kukiendesha, huyu Sam Mahela wa kujipodoa ameshindwa kabisa.
 
Back
Top Bottom