Tanzania bado ina uhaba wa wahandisi wanawake

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Tanzania ina upungufu mkubwa wa wahandisi wanawake unaochangia kuongeza changamoto katika sekta ya uhandisi nchini, hali inayopelekea waliopo pia wasiwe na uwezo wa kupigania changamoto zinazoikumba sekta hiyo.

Hayo yameelezwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto wakati akifungua Kongamano la Mtandao wa Wanawake katika Sekta ya Nishati ambapo walikutana kujadili changamoto zao.

Kumbilamoto amesema Serikali inaongeza ufadhili katika masomo hayo hasa kwa wanafunzi wa kike ili kuleta uwiano sawa katika sekta ya Nishati na masomo ya Sayansi kwa ujumla.

Kwa upande wake Mhandisi Juliana Pallangyo ambaye pia amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, amesema Wanawake wahandisi wana uwezo sawa na Wanaume katika utendaji na wakiongezewa nguvu ya kupewa nafasi na uwezeshwaji kimitaji watafanya mambo makubwa zaidi.
 
Super womens mkuje huku, kuna jambo lenu.
Hivi wanadhan PCM/PGM ni matako kila binadamu anayo?
 
Tanzania ina upungufu mkubwa wa wahandisi wanawake unaochangia kuongeza changamoto katika sekta ya uhandisi nchini, hali inayopelekea waliopo pia wasiwe na uwezo wa kupigania changamoto zinazoikumba sekta hiyo.
Wanahandisi nini cha kike? Waliopo wakiume mmewatumia wote wakaisha? Hatusikii wakisema uhaba wa marubani wa kike
 
Back
Top Bottom