Mbekengason
Senior Member
- Sep 27, 2013
- 187
- 41
Hivi viwanda vilianzishwa na J.Nyerere ili kukabiliana na ajira sambamba na kuongezeka kwa watu enzi za TANU, miaka ya 60 na 70. Ilivokuja CCM mwaka 77 uroho ukaimaliza ndoto ya viwanda tz. Vilivyokuwa viwanda kuna mikono ya wahindi nyuma yake na kifo cha viwanda hivyo ndio utajiri maridhawa wa wahindi hao marafiki na wabia wa viongozi au waliokuwa viongozi. Aidha wanafadhili ccm au ni wabunge wa ccm. Viongozi wanapolewa utajiri huo wanaanza kuwazuga wtz. Eti ukosefu wa ajira ni bomu linalotaka kupasuka. Wanasahau kuwa wameliunda wao. Likipasuka wao wataponea wapi?