Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Yutong kule China kilikuwa ni kiwanda kikubwa kilichokuwa kikitengeneza zana za kivita, kiwanda kimebadilishwa sasa kinatengeneza mabasi na mitambo mingine ya kiraia, mabasi ya Yotong yamefika hata hapa kwetu TZ. Ni muda muafaka kwa Serikali kuiwezesha Nyumbu pamoja na zana za kivita, kiwanda kitengeneze magari kwa ajili ya matumizi ya kiraia, tutaokoa mamilioni ya dola tunazopeleka Japan kununua magari tena mitumba. Kiwanda hiki kinaweza kutoa mchango mkubwa sana katika pato la Taifa na hivyo kupunguza umaskini tulio nao leo. Kutakuwa na haja gani ya kuagiza magari mitumba toka Japan na kwingineko wakati yapo magari mapya hapa nchini ambayp bila shaka bei itakuwa nzuri tu.
Nyerere alikuwa na dira akaona haja ya kuwa na kiwanda hicho, Warithi ni kama vile wamekitelekeza sana, wakumbuke kuwa hakuna maendeleo popote duniani bila ya kuwa na mageuzi ya Sayansi na Tekinolojia.
Bila wauzaji kujua watanufaikaje na mauzo, hakuna kitakachouzwa.....lakini kama kweli tunataka kufika tunakokwenda, manufacturing lazima tuifufue upya, hakuna jinsi