Tanzania, Afrika Kusini zawasilisha ombi maalum Umoja wa Afrika (AU)

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja Jamhuri ya Afrika Kusini zimewasilisha ombi maalumu kwa Umoja wa Afrika kuzitambua rasmi njia zilizotumika na wapigania uhuru kutoka Dar es Salaam kupitia nchi mbalimbali Kusini Mwa Bara la Afrika hadi Namibia kuwa urithi wa Kimataifa.

Ombi hilo limewasilishwa na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa katika Mkutano wa 34 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia mtandao na kuungwa mkono na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Tanzania pia imeuomba Umoja wa Afrika kuitambua lugha ya Kiswahili kama lugha ya asili na ya ukombozi katika Bara la Afrika kwa kuwa ndiyo lugha iliyotumika kwa ajili ya mawasiliano na mafunzo kwa wapigania uhuru ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni Sanaa, Utamaduni na urithi.

“Tumeuomba Umoja wa Afrika kuitambua lugha ya Kiswahili kama lugha ya asili na ya ukombozi katika Bara la Afrika kwa kuwa ndiyo lugha iliyotumika kwa ajili ya mawasiliano na mafunzo kwa wapigania uhuru ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni sanaa, utamaduni na urithi,” Amesema Prof. Kabudi.

Akiufunga Mkutano huo wa siku mbili, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Felix Tshisekedi amesisitiza kuwa umoja, mshikamano na amani katika bara la Afrika ndiyo nyenzo pekee itakayoliwezesha bara hilo kuendelea kiuchumi ili kuendana na rasilimali ilizonazo.

“Umoja, mshikamano na amani katika bara la letu la Afrika ndiyo nyenzo pekee itakatuwezesha sisi kuendelea kiuchumi ili kuendana na rasilimali tulizonazo kwa maslahi yetu mapana,” Amesema Rais Tshisekedi

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umejadili mambo mbalimbali ikiwemo uundaji wa Kamati mpya ya uongozi wa Umoja wa Afrika (the AU Bureau of Assembly) kwa mwaka 2021, uzinduzi wa Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2021 inayohusu “Sanaa, Tamaduni na Urithi katika kufikia azma ya Afrika Tuitakayo”

Mengine yaliyojadiliwa ni taarifa ya Maendeleo ya Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu COVID-19 Barani Afrika, taarifa ya Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika; na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitumia fursa hiyo kueleza utayari wake kuendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika na Nchi Wanachama wa Umoja huo katika kutekeleza jitihada zinazolenga kuiwezesha Afrika kujitegemea.
 
Miaka ya 70 ilipiganwa vita ya ukombozi wa nchi za afrika ambayo ilifanikiwa sana. Sasa yafaa vipiganwe vita vya ulinzi juu ya rasilimali za Afrika kutoingiliwa na mabeberu kwa njia ya kutupiganisha sisi wenyewe kwa wenyewe ambayo nadhani ndiyo itakuwa vita ngumu zaidi tunataka mali za Afrika zilinufaishe bara hili la africa kwa njia ya amani.

N.B Nadhani hili ndio lingekuwa point ya msingi zaidi na nashauri rais alichukue hili kama kauli mbiu na msimamo wake logic point.
 
Dokumentari kama hii imejaa uthibitisho wa wazee/ mababu hawa wa Namibia wakisimulia jinsi walivyopatiwa misaada ya mafunzo na lojistiki kambini Kongwa, Dodoma Tanzania jinsi ambavyo wanauenzi na kutosahau mchango wa Tanzania ktk ukombozi wa Namibia hivyo kutaka serikali ya Namibia kufanya juhudi vijana wa leo Namibia, Tanzania na Afrika tusipitwe na historia hii ya kujitoa muhanga bara la Afrika liwe huru tokana ukoloni na ubaguzi wa rangi:

THEIR BLOOD WATERS OUR FREEDOM | Namibian Heroes (Official 2020 Documentary)


Source : MICT Namibia
 

Students going into exile to Tanzania to join Umkhonto we Sizwe​


BAHA-1976-youth-in-exile_0.slideshow.jpg


Students going into exile to Tanzania to join Umkhonto we Sizwe (MK). Here four young students are interviewed by a Dar es Salaam journalist, Abdulla Riyami in Tanzania. From left to right; Miss Elsie Abrahams Biki (15), her brother Ernest Abrahams Biki (17), Michael Simango (17), and Richard Gardiner (16). The students took part in a demonstration and they said they were on the South African list of wanted.

Source : Students going into exile to Tanzania to join Umkhonto we Sizwe | South African History Online
 

First ANC National Consultative Conference - Morogoro, 26 April 1969​

The first National Consultative Conference of the ANC was held at Morogoro, Tanzania, from 25 April to 1 May 1969. The conference has become known as the Morogoro Conference. Oliver Tambo summed up the conference with these words: "Close Ranks! This is the order to our people; our youth; the army; to each Umkhonto we Sizwe militant; to all our many supporters the world over.

This is the order to our leaders; to all of us. The order that comes from this conference is: Close Ranks and Intensify the Armed Struggle!"

The Conference was attended by over seventy delegates from various centres representing ANC branches, units of Umkhonto we Sizwe - the ANC`s military wing - leader of the Indian and Coloured peoples and the revolutionary working class movement. The Conference was opened at a public session by GeorgeMagombe, Executive Secretary of the OAU Liberation Committee.

Other speakers at the opening session included: Mr A Swai, Administrative Secretary for External Affairs of TANU, Mr J J Nambuta of NUTA, Tanzania`s Trade Union Federation, Amadou N`diaye, Secretary of the All African Trade Union Federation and revolutionary leaders of FRELIMO (Mozambique), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia) and ZAPU (Zimbabwe).

Source: First National Consultative Conference - Morogoro, 26 April 1969 | South African History Online
 
Kongwa walitumia sana enzi hizo lakini serikali yenyewe imeshindwa kuwawekea njia ya lami tu kuwaunganisha kwa miaka 50 mpaka leo makorongo tu hawana njia kama watu hata hao SA ambao walitumia Kongwa kujifunzia wangewapa hata zawadi kuwaunganisha na barabara kuu kwa lami. Mkutano unaenda kujadili mambo hayana faida yoyote kwa watu, sasa wa kitambua kiswahili then what?
 
Watu wanawaza kwenda kuishi sayari nyingine sisi tunatafuta kutambua njia ambazo hazina msaada kwenye maisha yetu. Shame!
 
26 Jun 2012
Maadhimisho Miaka 50 ya FRELIMO

STV Watembelea makazi ya Eduardo Mondlane kiongozi wa kwanza wa chama cha wapigania uhuru wa Mozambique cha FRELIMO aliyeuawa na bomu lililotumwa na majasusi wa PIDE Taasisi ya Ujasusi ya Ureno ktk nyumba yake barabara ya Msasani, Oysterbay jijini Dar na Ofisi Kuu ya kwanza ya FRELIMO mtaa wa Lumumba Dar es Salaam Tanzania.

STV visita a casa onde Eduardo Mondlane foi assassinado



Source: mocambiqueTV
 

17 Sept 2019​

Eduardo Mondlane FRELIMO Leader in Britain | Mozambican Anti-Colonial Struggle | March 1968




Wednesday, March 6th 1968. Footage of Dr. Eduardo Mondlane (1920-1969), the President of Frelimo (Frente de Libertaqao de Mocambique), the Mozambican Liberation Front speaking at the Africa Centre in Covent Garden, London.

Dr. Mondlane, who was on a 10-day tour, was embarked on a campaign of winning British public support for the African nationalist movement against Portuguese rule in Mozambique. Source: Reuters News Archive. Note: 1.

He was the first African Mozambican to enter the University of Lisbon in 1950, however, he transferred to Oberlin College in the United States where he recieved his BA in 1953. He then obtained his MA and PhD in sociology at Northwestern University. In 1957 he joined the Trusteeship Department of the United Nations as a research officer, and from 1961 to 1963 he was a professor at Syracuse University.

After the independence of Tanganyika (later Tanzania), he went to Dar-es-Salaam to work for Mozambique's liberation. 2. On February 3 1969, Mondlane was assassinated by PIDE, the secret police of the Estado Novo; the Portuguese regime established by António de Oliveira Salazar. Mondlane's assassin was later identified as Casimiro Monteiro, the PIDE agent who also assassinated General Humberto Delgado.
Source : Adeyinka Makinde
 
Samora Moises Machel atunikiwa nishani ya Kilimanjaro daraja la kwanza May 22 1975 na Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Tanzania


0:14/1:34

FRELIMO Leader Samora Machel Honoured By President Julius Nyerere of Tanzania | May 1975


Published on 29 Apr 2020
Thursday, May 22nd 1975. Reuters Text: The President of Frelimo Mr. Samora Machel -- who will become Mozambique's first President when the country achieves full independence on 25 June -- was honoured by Tanzania's President Julius Nyerere on Thursday (22 May).

At a mass rally in Dar Es Salaam President Nyerere presented Mr. Machel with the Mt. Kilimanjaro Medal of the First Order. President Nyerere praised Frelimo for liberating their country and called on them to maintain their strength and unity.

He also said Mozambique's independence will not be complete if other African states are still being ruled by colonial powers. Mr. Machel thanked the Tanzanian leaders for the assistance they had provided for his country, including 1.4 million shillings (about 80,000 sterling) from the defence forces. Source: Reuters News Archive.

Adeyinka Makinde
 
Hawa yawapasa kwenye bajeti zao wawe wanatenga fungu la kutupooza kwa muda ambao tuliutumia kuwatumikia wao tu na tukaacha yetu yadorore
 
February 1969
Dar es Salaam, Tanzania

Tanzania yatoa mchango kwa wapiganaji wa Biafra wa Jimbo lilolotaka kujitenga Nigeria. Maandamano yafanyika Dar es Salaam kuunga mkono Biafra.

Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi 4 tu za kiAfrika waliounga mkono jimbo la Biafra la Nigeria kujitenga, juhudi za kujitenga ziliongozwa na Kanali Odumegwu Ojukwu aliyeasi jeshi la Nigeria.



Tanzania was one of 4 African nations which recognised the secessionist state of Biafra which at the time was fighting a civil war against Federal Nigeria. At the end of the rally, Abeid Karume (1905-1972), the Zanzibar leader who was the First Vice President of the nation presided over the end of rally ceremony during which Mr. Joseph Nyerere, the TANU Youth League Secretary-General handed over a cheque worth £13,000 Sterling and clothing to the Biafran Representative in East Africa, Mr. Austin Okwu. Source: Reuters News Archive.
Source : Adeyinka Makinde

July 19, 1967
Odumegwu Ojukwu, a former Lt. Colonel in the Nigerian Army gives a press conference as the leader of the breakaway Republic of Biafra.
 
Miaka ya 70 ilipiganwa vita ya ukombozi wa nchi za afrika ambayo ilifanikiwa sana,Sasa yafaa vipiganwe vita vya ulinzi juu ya rasilimali za afrika kutoingiliwa na mabeberu kwa njia ya kutupiganisha sisi wenyewe kwa wenyewe ambayo nadhani ndiyo itakuwa vita ngumu zaidi tunataka mali za afrika zilinufaishe bara hili la africa kwa njia ya amani
N.B Nadhali hili ndio lingekuwa point ya msingi zaidi na nashauri rais alichukue hili kama kauli mbiu na msimamo wake logic point
Nakazia
 

Eric Mtshali​

  • Synopsis
He was sent to the Union of Soviet Socialist Republics (USSR) and Cuba to receive military training. On his return Mtshali became Chief of Personnel in MK in Tanzania. During this time Mtshali worked closely with Moses Kotane transporting military hardware from Tanzania into the Zambezi valley in Zambia.
Source : Eric Mtshali | South African History Online
Sasa hawa wawa elimishe watu wa sasa huko afrika kusini nchi za afrika msaada uliyowapa
Siyo raia huko wazulu etc wanawaletea wageni wafrika wenzao mambo ya xenophobia

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom