Tanzania : A nation full of bogus politicians/leaders. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania : A nation full of bogus politicians/leaders.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Nov 17, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hivi ndivyo ilivyo nchi yetu kwa sasa. Ukiangalia yanayoendelea Bungeni utajua ninachokisema. Hakuna tena wanasiasa makini nchini hasa baada ya kujaza Idadi ya wachumia TUMBO, SIFA na VYEO katika Bunge.
  CHADEMA wamesusia mjadala kwa sababu wanazoamini ni sahihi na muhimu kwa maoni yao. Baadhi ya watanzania wameelewa kinacholalamikiwa na baadhi wanaona CDM wanapenda fujo. Binafsi siumizwi kichwa na hilo maana mwenye akili anaujua ukweli na ataweza kutenga uongo/pumba.
  Jambo ambalo limeanza kunipa shaka ni uwezo wa viongozi/wawakilishi wetu katika kujua kipi kisemwe wapi na kwa wakati upi na lipi muhimu kwa wakati gani na lipi si muhimu kwa wakati fulani. Je kuna sababu ya kila mbunge anayesimama kuchangia kulaumu wabunge na CDM kwa kususia mjadala na hicho kinachoitwa kuidhalilisha Zanzibar wakati kuna muswada mezani unaohitaji kuchangiwa mawazo na hatimaye kupitishwa?
  Naomba kwa pamoja tutafakari fikra hizi katika mitazamo kadhaa ili tuone kama kuna hekima sana kwa wabunge wa CCM, CUF na wengine kujadili vitendo vya CDM kama kipaumbele katika michango yao wakati issue ni mswada.
  1. Je ni kweli kwamba katika maelezo yote ya Mh. Lissu hakuna lolote muhimu isipokuwa pumba tu kiasi cha watu kutokuwa na lolote la kuishauri serikali kutazama upya mtazamo wake katika baadhi ya vifungu? Je itakuwaje kama kuna mapendekezo mengine mazuri kwa watu wote lakini yamefunikwa na hasira za baadhi ya wabunge hao wanaoona CDM inatumiwa?
  2. Je wabunge wetu wapendwa, waliozoea mbinu chafu/njama za chinichini katika kutafuta madaraka wana uhakika gani kwamba CDM hawatumii udhaifu wao wa kutochambua vifungu kwa umakini unaostahili kuwatoa katika hoja ya msingi ili baadaye waonekane wamepitisha madudu na wao, CDM wapate nafasi ya kuwashtaki kwa wananchi kama walivyofanya kwenye ufisadi na kuwapora majimbo kibao na kura nyingi za urais?
  3. Kama CCM wamekuwa wanatumia mbinu chafu kushinda wakiwa watawala nini kinawazuia CDM kutumia kutotafakari kwa majority ya wabunge wetu kuwaumiza kwa mbinu za kuwa-misslead ili wajadili kauli za Lissu wakati Mswada unapita pasipo kujadiliwa kwa umakini unaostahili?
  4. Mh. Hamad Rashid ametafakari kwa makini na kujua CUF yake imefikaje serikalini huko Zanzibar kama si kutumia nguvu yao ya umma na kususia mambo mengi katika SMZ mpaka kilipoeleweka?
  5. Na wenzetu CHADEMA; Kama swala lenyewe ni wazi litapita Bungeni kwa kutumia wingi wa viti vya CCM na vyama rafiki wao, kwa nini msibakie Bungeni mkatoa michango yenu ambayo baadhi yetu tunaikubali zaidi? Ili ijulikane Mnyika alipendekeza nini na kikatolewa nje n.k.?
  Hali hii imenishawishi kuamini kwamba tunao wanasiasa wengi Ma-Bogus wanaoenda kwa mkumbo tu na hawatumii muda wao kusoma, kusikiliza na kutafakari mambo kabla ya kuchangia. Huwezi kuushutumu ubalozi wa kigeni kwa madai ya kuingilia mambo ya ndani wakati serikali yako inatengeneza sera kwa kuwasilikilza mabalozi hao hao zaidi hata ya wanataaluma wazalendo. Hapa Mh. Ndasa ama amepotoshwa au hajui anachokisema maana ukifuatilila maamuzi mengi ya serikali za CCM yamekuwa yanaamini watu hao hao wa kutoka nje kuliko wazalendo na ndiyo sababu tunazidi kuvurugikiwa kiuchumi.
  Naomba niishie hapa kwanza. Natarajia kuwa open to more discussion.
   
Loading...