Tanzania 2015: Zaidi ya kula, kulala na kuvaa- Ni nani hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania 2015: Zaidi ya kula, kulala na kuvaa- Ni nani hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by B.Louis, Oct 3, 2012.

 1. B

  B.Louis Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Huwa nachangia mara chache ndugu zangu, lakini ni mhudhuriaji mkubwa wa mihadhara ya humu jamvini. Waungwana, tafadhali naomba niseme ninayoyaona ndani ya akili yangu. Naanza kwa kusema, ''Mwanadamu wa leo anashugulika ili ale, alale na avae kimsingi. Kama akihakikishiwa kula na kulala na kuvaa basi angeishi kama mbuzi ama ng'ombe.

  Tofauti ingekua kwenye kuvaa nguo tu''. Sio wote bali ni wengi. Wale wachache ambao wanaona zaidi ya kula, kulala na kuvaa wamefanikiwa/watafanikiwa. Kwa kua hili ni Jukwaa la siasa basi nielekeze hoja hii huko kwa kutizama wanasiasa wetu Tanzania na hata mataifa mengi ya ulimwengu. Wanasiasa wananadi kuhakikishia wananchi wenzao kua wakimpa mamlaka ya kutumia fedha zao (kodi) ili ahakikishe wamekula, kulala na kuvaa; kimsingi.

  Kwa utashi huu tutalaumu kila mtu atakayekua Rais au kiongozi yeyote yule. Kama ufanisi na ubora binafsi haupewi umuhimu na kuthaminika basi hapo tumefungulia wenyewe mlango matatizo yetu-kama Watanzania na kama wanadamu. Mimi si shabiki wa siasa ila nadhani ni chombo kinachoweza kutufikisha mbali sana zaidi ya kula, kulala na kuvaa. Ningependa sana kupata hoja zinazoshabihi mrengo huu kwa kuangalia mabadiliko katika utamaduni wa Mtanzania wa leo kuelekea Mtanzania bora zaidi wa miaka ya mbeleni atakaye thamini ubora binafsi na kujiamini katika ufanisi wa anachokifanya.

  Na ni kiongozi gani anayeweza kutufikisha hapo kwa matendo kiukweli. Hata kama anatoka chama gani kwa dhati ya utashi na tumpe taifa 2015. Tutende haya na kuyasimamie au la tukubali anguko kila kunapokucha. Tusiwekeze fikra kwa yale yanayosemwa bali kwa yaliyofanywa katika mafanikio halali binafsi na ya kitaasisi. Kwani taifa ni moja ya taasisi kubwa katika ulimwengu. Karibuni tushirikishane kuboresha muono huu ili kuwezeshana katika kufanya maamuzi sahihi 2015.
   
Loading...