Tanzani inahitaji uhakiki wa vyama vya siasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzani inahitaji uhakiki wa vyama vya siasa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bakari Maligwa, Feb 26, 2012.

 1. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Tangu mwaka 1992; pale, mfumo wa vyama vingi vya siasa (maarufu kama, demokrasia ya vyama vingi vya siasa) uliporuhusiwa kwa Sehria Na. 4 ya mwaka 1992, vyama vimekuwa vikianzishwa na au "kuchipua" kama "uyonga wa mkonge"...na leo tuna chama kilichopata usajili wa kudumu hivi "majuzi" yaani, CCK [Chama Cha Kijamii]. Demokrasia (demokrasi, siyo domo-kaya) ni nzuri kwa vile inawapa nafasi watu kuchangua miongoini mwa vile nafsi (za watu) vinapenda na kuweka kwenye "mamlaka" ya uongozi wa dola na au uwakilishi kwenye vyombo vya uongozi wa nchi (kama vile Bunge, Baraza la Wawakilishi, na Mabaraza ya Madiwani).

  Pamoja na ukweli huu; kuna haja ya kufanya upitizi wa demokrasia ya vyama na mchakato wa demokrasia ya vyama vingi tukizingatia mazingira tuliyonayo. Na kwa jinsi hiyo hapa naomba niweke, japo kwa uchache, nukta za kuzifanyia kazi (uhakiki na tahakiki). Nukta hizo ni:
  1. Vyama ni vingi kuliko uwezo wa siasa ya demokrasi ya vyama vingi;
  2. Vyama vingine vimefanywa kampni binafsi za watu na au vikundi vidogo vya watu;
  3. Vyama vingine vimekuwa vikitumika kueneza propaganda ya kuua demokrasia halisi; na
  4. Vyama vingine vimepoteza uhalali wa kuwa ndani ya ulingo wa siasa.
  Kwa jinsi hiyo ni vema na haki kwa msajili wa vyama vya siasa nchi (Mh. John Tendwa) kufanya yafuatayo:
  • Kuhakiki uhalali wa vyama vya siasa juu ya kiwango cha wanachama chama ilichonach na kama kinakidhi utashi wa sheria;
  • Kuhakiki sera na madhumuni ya kuanzishwa kwa vyama vya siasa na kubaini kama kweli vyama vinaendeleza sera na madhumuni yake;
  • Kuhakiki harakati za vyama vya siasa na kutambua uhalali wa harakati za kisiasa za vyma hivyo; na
  • Kuhakiki uwepo wa vyama vya siasa kwenye maeneo yote ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar).
  Kwa kufanya hivyo; nadhani demokrasia ya vyama vingi inaweza kuwa na "maana" halisi ya mfumo huo. Hatuwezi kuwa na vyama vya "msimu", vyama vya "uchaguzi" na "vyama ghusi" vinavyotumika wakati wa shughuli za "kampeni za siasa" ilhali ukweli wa kuwepo kwa vyama hivyo ni "hadaa" ya kuwa na vyama vingi ilhali sehemu ya vyama hivyo ni "vile' vilivyoanzishwa katika kujaza wingi wa vyama kwa manufaa ya "chama kimoja" kinachotumia nafsi hiyo katika kuendesha "propaganda" na hatimaye kugawa kura na au kuvuruga demokrasia.

  Nimetumia muda wa kutosha (kama miaka kumi [10] na ushei) kufanya utafiti binafsi (na sio rasmi) kuangalia mwenendo wa baadhi ya vyama vya siasa na kugundua nukta nne (4) nilizoziainisha mwanzoni mwa makala haya. Ni wakati sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (chini ya Mh. John Tendwa) kuacha "siasa" ifanye kazi ya uhakiki (political parties audit) na hata kuvifuta baadhi ya vyama vilivyopeteza sifa za kuwa vyama vya siasa. Najua hata yeye (Mh. John Tendwa) anajua kwamba kuna baadhi ya vyama vya siasa vimepoteza uhalali; na kwa jinsi hiyo asisubiri kusutwa na wakati...afanyekazi aache "domo-kaya" la kuitumikia siasa ya upande mmoja - hapa sheria lazima itumike; hata hivyo, uchunguzi wa kisayansi na mantiki vitumike katika kupata vyama makini vitakavyoweza kufikia utashi wa demokrasia ya kweli na si ubabaishaji.

  Mwisho, nawatakia tafakari jadidi; na lazima tupate muafaka wa kuwa na vyama makini na vyenye nia ya kweli na haki katika kujenga mustakabali wa demokrasia ya vyama vingi. TUSHIRIKIANE TUJENGE DEMOKRASIA YA KWELI!
   
 2. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 28,951
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, hebu fikiria vyama kama vile TADEA cha Mzee Chipaka, NLD, CHAUSTA, DEMOKRASIA MAKINI, NRA, NK, kweli vinajaza tu daftari la usajili...........
   
Loading...