TANU iliundwa Burma wakati wa WWII (1939 -1945)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,254
TBC imekuwa ikirusha kipindi, ''Kutoka Maktaba,'' kipindi hicho kikionyesha
mahojiano aliyofanya Ally Sykes na TBC 1 wakati wa uhai wake kuhusu
maisha yake akiwa Burma wakati wa WWII hadi kwisha kwa vita na kuanza
harakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika:



''Wakiwa pale Kurnegala, askari Waafrika walipata mafunzo ya kupigana msituni kwa miezi minne na kisha wakaondoka kwenda Burma kupitia Trincomalee.

Kutoka hapo wakaelekea Chittagong.

Wakati wote huo wakiwa katika msafara walisindikizwa na British Royal Navy, meli zao zikienda polepole kwa tahadhari, zikipita njia ambayo walihisi ni shwari kutokana na mashambulizi ya Wajapani.

Ilikuwa hapo Chitagong ambapo askari walipata kwa mara ya kwanza kuonja kile kilichokuwa kikiwangoja.

Kulikuwa na kitambo cha takribani kilometa kumi baina ya bandari na kambi.

Barabara ilikuwa mbaya na ilikuwa imejaa matope ambayo yalifika kina cha kifundo cha miguu kutokana na mvua kubwa za monsoon.

Kambi ilikuwa chafu kwa matope yaliyotapakaa kila mahali. Askari ilibidi abebe mzigo wake mzito wa vifaa na zana, bunduki na risasi.

Vilevile ilibidi wachimbe mahandaki siku hiyo hiyo kwa ajili yao wenyewe na kwa maafisa wao Wazungu.

Kambi iiliwapa picha kamili ya kilichokuwa kikiwasubiri hata kabla hawajasikia milio ya bunduki za Wajapani."

''Ilikuwa ni pale Anfal ambapo, huku vita vinafikia ukingoni, Abdulwahid na askari wenzake wa Burma walikaa kitako kutafakari mambo yaliyowasibu katika vita na kuufikiria mustakbal wa Tanganyika.

Iliamuliwa kuwa askari wa Burma kutoka Tanganyika waliokuwa 6th Battalion (Batalioni ya Sita) wawe ndio chanzo cha chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuuhamasisha umma.

Wote waliafiki wazo hilo.

Jina lililochaguliwa kukitambulisha chama hicho lilikuwa Tanganyika African National Union (TANU).

Ally Sykes anamkumbuka Abdulwahid kuliandika jina la chama hicho kilichokusudiwa ndani ya shajara yake.

Hawa askari wa Burma walikuwa wakifahamu vyema kuwa tayari huko nyumbani kulikuwapo na African Association, chama ambacho kilikuwa kikipigania haki za Waafrika.

Abdulwahid alitarajiwa afahamu hili zaidi ya wenzake kwa sababu baba yake ndiye aliyekianzisha chama hicho akiwa katibu wake wa kwanza.

Lakini suala la jinsi wangekiunganisha chama hicho kipya cha TANU na kile cha African Association halikujadiliwa.''

1154618

Kulia Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally katika uniform ya King's African Rifles (KAR)
Burma Infantry. Picha hii ilipigwa Burma mwaka wa 1942.


Kutoka: ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...''
 
Mkuu nashukuru kwa bandiko hili.
Nimemkumbuka mzee wangu ambae nae alikua mmojawapo wa askari wa tanganyika huko burma.
Yule mzee mpaka anafariki mwaka wa 2015 ile safari ya kutoka huku kwenda vitani na vile walivyopigana vita na kushinda kwa mwingereza vita hio,hakuwahi kusahau hiko kisa.
Alikua akitusimulia kiukamilifu matukio yote yalio watokea ila kwenye hilo la kuanzishwa tanu sikuwai kusikia akielezea, lakini alisema walikuwepo askari wengi sana kutoka tanganyika na afrika ya mashariki na hata nje ya afrika mashariki.

Nasikitika hayupo tena huwenda ningemuuliza asingekosa mawili matatu ya uanzishwaji wa chama cha tanu huko.

Ila angalau uwepo wako kwa namna moja ama nyingine tumeweza kujua kilichotokea, Asante.
 
Mara nyingi watu wanaokuwa maraisi wa kwanza kwenye nchi zao sio waanzilishi wa vuguvugu.
Tanzania kina Kleist Sykes,Plantan,Aziz Ali,Dosa Aziz,Zuberi Mtemvu,John Rupia,Lazaro Bomani na wengine wengi
Huko Kenya General China Warihui,Field Marshal Muthoni Kirima huyu alikuwa mwanamke pekee kufikia cheo cha field Marshall wa Mau Mau alikaa porini miaka11 akipigana bado yuko hai ana miaka88,Dedan Kimath,Harry Thuku 1895-1970
 
Back
Top Bottom