TANROADS yaanza kumwelemea Magufuli; Adaiwa kujali sifa binafsi si matatizo ya wizara. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANROADS yaanza kumwelemea Magufuli; Adaiwa kujali sifa binafsi si matatizo ya wizara.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 10, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  *

  WAKATI hali ya mambo ndani ya Wizara ya Ujenzi ikiendelea kuwa tete, waziri wa wizara hiyo, Dkt. John Magufuli amerushiwa
  lawama kwa kile kilichoelezwa kuwa kutotilia maanani matatizo ya ndani, badala yake kuweka kipaumbele kwa majukumu ya kisiasa yanayompa sifa binafsi.

  Chanzo cha kuaminika ndani ya wizara hiyo kimeliambia gazeti hili kuwa imani waliyokuwa nayo wafanyakazi hao inazidi kushuka siku hadi siku kutokana na Dkt. Magufuli kushindwa kupatia ufumbuzi wa haraka kero zilizodumu kwa muda mrefu ndani ya wizara hiyo ikiwemo uteuzi wa wakala mbalimbali ikimewemo TANROADS.

  "Wizara ya Ujenzi chini ya mheshimiwa Magufuli imepoteza mwelekeo kwa kile tunachoona, ameweka kipaumbele zaidi kwa shughuli zinazompa sifa binafsi, anatafuta 'cheap popularity' kwa wananchi na kujisahau kutekeleza vipaumbele vya majukumu muhimu ya Wizara yake," kilisema chanzo hicho na kuongeza;

  "Inashangaza waziri kutembelea mikoani na kuwaamrisha wakuu wa mikoa na wilaya kuwaweka ndani makandarasi bila kufuata taratibu. Jambo hili analifanya kienyeji sana 'unprofessional.' Kuna utaratibu wa mambo yote kwenye mikataba na hatua za kuchukua kama mkandarasi anashindwa kufanya vizuri.

  "Tatizo ni kwamba waziri hajui na hataki kujua labda kuponzwa na sifa anazomwagiwa na wananchi, ndio maana anaacha huku wizarani mambo yamelala wala haoni umuhimu wa kuwateua watendaji wakuu mapema."

  Majira lilidokezwa kwamba tangu Dkt. Magufuli arudishwe wizarani hapo, kurugenzi na wakala zote za wizara zimeendelea kuwa na watendaji wakuu waliokaimishwa kwa muda usiojulikana.

  "Hii imetuchanganya kwani tuliamini Mheshimiwa Rais Kikwete ametuletea Magufuli akiamini kwamba ana uwezo wa kudhibiti hali mbaya ya wizara na wakala zake. Badala yake Mheshimiwa Waziri yuko moto kutoa amri nzito zinazompa sifa binafsi, hata wakati mwingine kuvuka mipaka bila kushirikisha wakuu wake wa kazi."

  "Kwa mfano amri za bomoabomoa nchi nzima na amri za kuwatisha makandarasi bila kufuata taratibu ni hatari katika kipindi hiki ambacho serikali inakabiliwa na changamoto nyingi juu ya kero za wananchi ambazo hazijazipatiwa ufumbuzi.

  "Kwa ujumla wizara imepoteza mwelekeo, badala ya kuwa wizara ya kujenga, imekuwa ya bomoabomoa. Ikumbukwe kwamba hata hayo mabango yaliyowekwa barabarani yaliwekwa kwa ridhaa ya serikali hivyo kuyaondoa ni vyema utaratibu ukafuatwa kuepuka kuiingiza serikali katika kesi za fidia kama ilivyojitokeza katika uuzaji holela wa nyumba za serikali, Dowans nk. Hivi sasa wizarani hakuna anayejua afanye nini zaidi ya kusubiri utekelezaji wa Waziri Magufuli."

  Chanzo kingine ndani ya Wizara hiyo kilisema hatua ya Dkt. magufuli kuchelewa kupanga miundo na watendaji wakuu wizarani na kwenye wakala imechangia kupunguza kasi ya utendaji wizarani hapo.

  "Nashindwa kuelewa kwanini anachelewesha jambo hili au hajapata anaowataka yeye? Waziri Magufuli anasifiwa sana na wananchi wa kawaida ambao wao hawaoni kasoro hizi. Huenda amejisahau kwa sifa hizo na kusahau majukumu yake mengine ya ndani ya wizara. Aangalie matatizo yaliyo ndani ya wizara na kuyashughulikia haraka."

  Vyanzo hivyo vilimshauri Dkt. Magufuli kutumia muda mwingi zaidi kupanga safu za wizara yake bila upendeleo ili kukabiliana na majukumu mazito yanayoikabili wizara na kuleta mafanikio kwa serikali na taifa kwa ujumla.

  Majira lilipomtafuta Dkt. Magufuli simu yake iliita bila kupokelewa. Lilipotuma ujumbe wa maneno kuomba apokee simu, lilijibiwa kuwa "Unayemtafua yuko Kagera."

  Lilipompigia simu msaidizi wake aliyefahamika kwa jina moja la Samike, alisema katibu mkuu ndiye mwenye jukumu la kutoa ufafanuzi wa masuala yote yanayohusu wizara hiyo kwa kuwa ndiye mtendaji mkuu.


   
 2. M

  Matarese JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  wazushi tu hao, magufuli piga mzigo tu!
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio wameconfirm kuwa hata Tangazo la juzi la Pinda ni kutuliza hali ya sasa, maisha magumu, hali mbaya, serikali iko kwenye wakati mgumu, hivyo bomoabomoa ni kupunguza makali,

  Huyu anasema Magufuli kukemea wakandarasi na bomoabomoa havijazingatia hali ya sasa ya nchi

  Hata Dowans imewashwa ili kuzuia maisha yasipande sana....tukarudi kulekule

  Compromise...compromise...we are comprimising with situations

  Kuwa kumbe kuna watu wanaweza wakaiba, halafu kipindi cha njaa tukarudi kwao kuomba na tukawapigia magoti wezi

  waliohusika kutoa viwanja isivyo halali wawajibishwe hata kama vibali vilitolewa mwaka 1950! ndio uwajibikaji ambao HAPA HAUPO yet we are crying for development!
   
 4. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  huku vijijini wanasema magufuli na chadema.
   
 5. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Pombe twende baba kaza buti bora sifa kwa wananchi kuliko kwa mafisadi
   
 6. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ipo kazi, sikujua kupambana na mafisadi ni gharama kubwa hivi; magufuli go-go-go!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ukipenda Chongo uita kengeza!, badala yake mnambomoa badala ya kumjenga bado tunataka nyumba zetu
   
 8. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  magufuli ana chuki na makandarasi fulani fulani hivyo anataka kuwaumuza wote
   
 9. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kazi za Wizara ni zipi kama siyo hizo za kujenga?
   
Loading...