TANROADS, vipi ile kasi ya kumalizia barabara kuingia stand kuu ya Mbezi Luis na njia sita Kimara hadi Kibaha? Mbona hakuna kinachoendelea?

Kwasenga

Member
Feb 24, 2021
50
52
TANROADS, mbona barabara ya kuingia stand ya mabasi Mbezi Luis progress yake ni zero? Au ndo imeyeyuka hivyo? Je, hii ya njia sita mbona pia hakuna kinachoendelea?
 
Wanasubiri siku 21 za maombolezo zipite, au wanamhujumu Mama.

Ngoja tuone.
 
Kuna kampeni mpya dhidi ya rais wa sasa, sio? Naona ID zile zile toka asubuhi zipo kwenye pambano la propaganda zikibadilishana tuu cha kuanzisha kwa madai angekuwepo JPM hali isingekuwa ilivyo! Target kuonyesha SSH hatoshi?
 
Labda wanangojea fungu, nimedokezwa kuwa mifumo ya malipo yote imefungwa, pesa haitoki hadi maza akamilishe ukaguzi wake BOT. Inaonekana kuna watu walitaka kutajirika na kifo cha hayati.
 
Labda wanangojea fungu, nimedokezwa kuwa mifumo ya malipo yote imefungwa, pesa haitoki hadi maza akamilishe ukaguzi wake BOT. Inaonekana kuna watu walitaka kutajirika na kifo cha hayati.
Ok. Si vibaya. Acha mama ajiridhishe kwanza.
 
Hadi sasa ile kambi kubwa sana ya ujenzi wa barabara ya njia sita toka mbezi hadi kibaha iliyopo gogoni ni kama imefungwa! Pako kimyaaaa!!!! Huko nyuma mitambo ilikuwa inaunguruma pale masaa 24! Lakini sasa pako kimyaa!! Hapo kambini mpaka sasa kuna vifusi vya kufa mtu vya kokoto itakayomwagwa barabarani lakini kimyaaa!!! Barabarani hakuna harakati zozote zinazoendelea kuonesha kuwa kazi inaendelea kama huko nyuma, magari ya ujenzi wa barabara hiyo yalipokuwa yanapishana barabarani muda wote!!. Bila shaka wadau wanajipanga upya na tutegemee wakirudi watarudi kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya!! Ni hayo tu!!! Kazi iendelee !!
 
Back
Top Bottom