Tanroads msipoyafanya haya sasa mtayafanya baada ya msiba mkubwa mnaoupalilia

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,827
Nianze kwa kuwaomba chonde chonde mods msiunganishe uzi huu na nyuzi nyingine. Niombe pia mods msiufunge uzi huu ambao ningependekeza uwanja wa kuangazia barabara hii kwa picha.

Nime andika nyuzi kadhaa zenye maudhui kama haya kwa barabara hii ya rusahunga Rusumo njia ya kuelekea rwanda, Burundi na DRC.

Barabara hii kimsingi imesahaulika haswaaa na ajali zitokanazo na ubovu wake zinaendelea kuleta misiba, hasara na uharibifu ambao labda kutokana na upembezoni wake zimeendelea pasi na kuwa reported.

Ajali hizi katika picha ni latest na ndiyo yaliyo maisha ya kila leo huku.

Tanroads rekebisheni ubovu huu ulio mikononi mwenu au pangeni kuifunga hii njia labda kama vinginevyo ni nia yenu kutengeneza misiba isiyokwisha.
 
Attachments

  • IMG-20190802-WA0003.jpg
    IMG-20190802-WA0003.jpg
    68 KB · Views: 28
  • IMG-20190630-WA0002.jpg
    IMG-20190630-WA0002.jpg
    57.1 KB · Views: 27
  • IMG-20190731-WA0008.jpg
    IMG-20190731-WA0008.jpg
    74.1 KB · Views: 25
  • Accident 3.jpg
    Accident 3.jpg
    78.5 KB · Views: 25
  • Accident 5.jpg
    Accident 5.jpg
    65 KB · Views: 25
  • Accident 4.jpg
    Accident 4.jpg
    70.4 KB · Views: 25
  • Accident 1.jpg
    Accident 1.jpg
    100.3 KB · Views: 26
  • IMG-20190714-WA0001.jpg
    IMG-20190714-WA0001.jpg
    90.1 KB · Views: 26
  • IMG-20190731-WA0001.jpg
    IMG-20190731-WA0001.jpg
    37.3 KB · Views: 25
  • Accident 6.jpg
    Accident 6.jpg
    89.4 KB · Views: 21
  • IMG-20190630-WA0001.jpg
    IMG-20190630-WA0001.jpg
    84.6 KB · Views: 19
Jamani ukweli hii road ni shida wakuu maana ni hatari sana hasa pale ngazi saba na kwenye mteremko wa kutoka Lusahunga ukiwa unaelekea kitongoji cha kikoma kuna daraja alafu unapandisha tena mlima kwenda nyamaragara duuu ni taabu sana Tanroad mkoa wa Kagera mko wapi
 
Kwa mipango yoyote ya muda mrefu tanroads wanaweza kuwa nayo kuhusu barabara hii status quo ya barabara hii haikubaliki kwa hali yoyote ile.

Huku ni ajali kila siku.

Tutakuwa ya ajali katika barabara hii zinazosababishwa na ubovu wa barabara.

Tanroads wanawajibika moja kwa moja kwa maana ya njia hii.
 
Asante mkuu kwa kuleta uzi huu,kwa kweli hali ni mbaya sana maeneo haya.
Mwaka jana nusura nipate ajali maeneo hayo nikiwa na familia.
barabara ina mashimo makubwa yenye lami ya zamani iliyochimbika
ni afadhari iondolewe kabisa ubakie udongo mtupu mashimo yake
yatakuwa na unafuu.Naamini wahusika watachukua hatua.
 
Tanroads juzi kati wameonekana wakiweka mabango kuhimiza uwepo wa mteremko badala ya kuziba mashimo. Hii ni mara baada ya kufyeka pembezoni mwa barabara.

Unajiuliza na kiangazi hiki wafyeka nyasi zipi? Kwa nini huzibi mashimo?

Pana haja ya wenye kuathiriwa na ubovu wa barabara hii kuwashitaki na hata kuwadai fidia.

Eboo! Zibeni mashimo vinginevyo this time tutaumbuana. Hamuwezi kutuweka rehani hivyo kwa njaa zenu. Road Fund za hii barabara mnapekeleka wapi?
 
Kwanini msipitie Mbeya Zambia to congo na hayo maroli yenu. Kwanza nyie wenye maroli ndio mmehujumu reli zetu
 
Hiyo barabara imesababisha niwatelekeze ndugu zangu waliopo huko Ngara kwa sababu Mara ya mwisho nilipata taabu kweli na nikawaahidi tu waendelee kuwa wageni wangu hadi barabara hiyo itengenezwe.
 
Picha zaidi. Ni kwa asiyepita njia hizi pekee anayeweza kubeza jitihada za kuwataka tanroads kuwajibika.

Hawa jamaa ni mzigo na wanaendelea kutugharimu maisha.

Pity.
 
Attachments

  • Accident 6.jpg
    Accident 6.jpg
    89.4 KB · Views: 20
  • IMG-20190630-WA0001.jpg
    IMG-20190630-WA0001.jpg
    84.6 KB · Views: 18
Nianze kwa kuwaomba chonde chonde mods msiunganishe uzi huu na nyuzi nyingine. Niombe pia mods msiufunge uzi huu ambao ningependekeza uwanja wa kuangazia barabara hii kwa picha.

Nime andika nyuzi kadhaa zenye maudhui kama haya kwa barabara hii ya rusahunga Rusumo njia ya kuelekea rwanda, Burundi na DRC.

Barabara hii kimsingi imesahaulika haswaaa na ajali zitokanazo na ubovu wake zinaendelea kuleta misiba, hasara na uharibifu ambao labda kutokana na upembezoni wake zimeendelea pasi na kuwa reported.

Ajali hizi katika picha ni latest na ndiyo yaliyo maisha ya kila leo huku.

Tanroads rekebisheni ubovu huu ulio mikononi mwenu au pangeni kuifunga hii njia labda kama vinginevyo ni nia yenu kutengeneza misiba isiyokwisha.
Tuko kwenye mchakato tunalifanyia kazi very soon,utapata majibu
 
Tuko kwenye mchakato tunalifanyia kazi very soon,utapata majibu

Mpaka mmalize huo mchakato si tutakuwa tumekwisha kufa? Give us a break hatupendi kuwekwa rehani na nyie.

Hatupendi kuuliwa na nyie kwa uzembe wenu na njaa zenu.
 
Si wawape tu strabag wapo hapo karibu tu wanamalizia kipande cha lusahunga-nyakanazi
 
Eng. Mfugale pamoja na mengi mazuri inabidi aongeze ukali hasa hizi barabara ambazo ni highways.

Kuna safari tunawahi ziara ya Rais Mtwara, eneo la kiranje ranje almanusura tupotee,kuna mibonyeo ya kutisha. Shukrani kwa poti mzoefu na ubora wa gari tulokuwa nayo.

Eneo lile linahitaji kutengenezwa upya kabisa.
 
Mkuu pana hatua za muda mrefu wa kati na mfupi.

Hawa mabwana ni wajibu wao kuona barabara zinapitika kwa salama au zinafungwa kupisha maafa.

Ukiiona hali ya barabara hii utajiuliza kama kweli pana haja ya kuwa na maofisa wa tanroads na ati kuwa wako maofisini na kuwa wanapokea mishahara na marupurupu pia.

Ifungeni njia hii au muitengeneze. Short of that hamtufai.
 
Asante mkuu kwa kuleta uzi huu,kwa kweli hali ni mbaya sana maeneo haya.
Mwaka jana nusura nipate ajali maeneo hayo nikiwa na familia.
barabara ina mashimo makubwa yenye lami ya zamani iliyochimbika
ni afadhari iondolewe kabisa ubakie udongo mtupu mashimo yake
yatakuwa na unafuu.Naamini wahusika watachukua hatua.

Mkuu wakichukua hatua tutawapongeza kwa dhati kabisa japo ni kazi yao.

Ni bahati mbaya sana pande hizi za makwetu zimefumbiwa macho si na viongozi tu bali hata wana habari.

Tupo kama nchi nyingine kwa wenzetu zajengwa airports, barabara za juu na hata barabara za njia 8. Achilia mbali yale madege tutakuwa vipi katika kadamnasi ya kuyapokea kama makwetu ni hivi?
 
Wamkusikia...

Cc: mahondaw

Hawa kusikia ni sawa na sikio la kufa. Uzi wa awali kuhusu hili:

Angalia comments pale zili range tokea hii barabara ina umuhimu gani kwa taifa hadi kama picha bado basi tunajadili uzuri wa demu gizani. Nini walifanya?

This time tutawakomalia sana maana wenzetu mwapita barabara za juu sisi je?
 
Back
Top Bottom