Tanroads Mnachora "X" ONDOA halafu inapita miaka hawajaondoa, lengo lenu ni nini?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Sehemu nyingi naona alama za X Ondoa alafu inapita mwaka watu wanazidi kuchafua barabara na kuingia zaidi, baadhi ufuta kabisa hizi alama, sasa najiuliza huu wino mnaoutumia mnagawiwa bure? Na huyu anayepita kuchorachora kwenye vibanda halipwi chochote?

Kama mna madhumuni ya kweli mkishapitisha ondoa siku inafuata teketeza ili wengine wajifunze kuwa nyie amchezewi.Hawa machinga wamepewa rungu ya kupanga kokokote ili mradi eti haibi cha mtu, sasa hivi hadi road reserve wanajaza vitu jioni waendao wa miguuu wenye haki wanaanga kupishana na magari, wengine uvunjwa miguu kwa kuwaendekeza hawa wanaofanya biashara sehemu yeyote.
 
Hii kitu inaudhi na ni uchafuzi kibao kinaiwekewa x alafu kinakaa 3 yrs sasa si mngeondoa TANROADS mnazingua
 
Hii kitu inaudhi na ni uchafuzi kibao kinaiwekewa x alafu kinakaa 3 yrs sasa si mngeondoa TANROADS mnazingua
Yaaani ni sawa na kuja kwangu kuniuliza, niko na mpango gani ni ndizi iliyoiva pale shambani kwangu ambayo imeegemea kwenye mpaka wako.

Hizo alama za X, ni kukumbusha tu kuwa, uko sehemu isiyosahihi, hivyo basi siku watakapo kuja, usije lalama kuwa hukuwa unajuwa.

Pia kumbuka kwamba, sio wote wanaojua mipaka ya Tanroads kwenye barabara zinazopita kwenye maeneo yao. Jamaa mmoja alishawahi kuuziwa road reserve along moro road maeneo ya kimara. Kipindi hicho ilikuwa bado hawajaanza kuweka zile beacons.

Tuchukue tahadhari tunapo endeleza kwenye road reserves. Watakapo yahitaji maeneo yao, basi tusianze kulalamika kuwa tumeharibiwa sehemu zetu za biashara na miataji.

Invest wisely.

Sent using [Iphone XS Max]
 
Ndugu yangu uliza athari za wao kuondoa baada ya onyo hilo . Think twice mkuu
Wana JF,

Sehemu nyingi naona alama za X Ondoa alafu inapita mwaka watu wanazidi kuchafua barabara na kuingia zaidi, baadhi ufuta kabisa hizi alama, sasa najiuliza huu wino mnaoutumia mnagawiwa bure? Na huyu anayepita kuchorachora kwenye vibanda halipwi chochote?

Kama mna madhumuni ya kweli mkishapitisha ondoa siku inafuata teketeza ili wengine wajifunze kuwa nyie amchezewi.Hawa machinga wamepewa rungu ya kupanga kokokote ili mradi eti haibi cha mtu, sasa hivi hadi road reserve wanajaza vitu jioni waendao wa miguuu wenye haki wanaanga kupishana na magari, wengine uvunjwa miguu kwa kuwaendekeza hawa wanaofanya biashara sehemu yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom