Tanroads mko wapi? Barabara ya sekenke na mawe ya hifadhi ya barabara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanroads mko wapi? Barabara ya sekenke na mawe ya hifadhi ya barabara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mama Mdogo, Sep 23, 2012.

 1. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wiki chache zilizopita nilikuwa safarini kutoka Ushirombo/Bukombe kuja Dar kwa bus. Muda mwingine nikiwa macho nilikuwa naangalia mandhari nzuri ya njiani na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nchi nzuri. Hata hivyo kuna kero mbili nilizoshuhudia zinazohusiana na hawa wadau wetu TANROADS.

  Kwanza, barabara ya Mlima wa Sekenke iko katika hali mbaya, imechimbika na kubomoka. Ni miaka minne tu tangu imekamilika na kukabidhiwa serikalini lakini hali ndivyo hivyo. Je imejengwa chini ya kiwango na hao wajenzi wa Kichina au mizigo inayopita pale inazidi kiwango??

  Pili, katika kipande cha barabara kutoka Chalinze hadi Vigwaza sikuona vile vigingi vya alama ya hifadhi ya barabara, je vimengolewa na wananchi wenye hasira kali? vimehujumiwa? Au Tanroads bado hawajaviweka. Je katika maeneo hayo mtu akijijengea banda lake hadi mita tano kando ya barabara ni nani wa kulaumiwa.

  Kwa haya machache namuomba Injinia Mfugale (CEO wa Tanroads) afunguke!!! Nawasilisha
   
 2. m

  mecy JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 424
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka barabara hyo haifai tena,serkali hi ni mbovu,kuna watu wamehongwa kuikubali barabara hyo ili ikabidhiwe serkalini,hvyo bsi tanroad singda iwajibike pia,hyo barabara irudiwe,sasa sijui tutakuwa tunapita wapi,eti serkali sikivu! Yani hlo neno linaniudhi,
   
Loading...