Tanroads kama Tanesco .....yatakiwa kulipa fidia.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanroads kama Tanesco .....yatakiwa kulipa fidia..........

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 26, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Tanroads kama Tanesco Saturday, 25 December 2010 20:52

  Fredy Azzah
  WAKALA wa Barabara Nchini (Tanroads), imetakiwa kuilipa zaidi ya Sh966 milioni, Kampuni ya Ujenzi na Ushauri ya Norconsult AS ya Norway, baada ya kuvunja mkataba wa kuinua kiwango cha Barabara ya Geita-Sengerema-Sengerema-Usagara.

  Uamuzi huo ulitolewa Desemba 21 mwaka huu na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Kamataifa za Biashara.
  Julai 18 mwaka 2008, Kampuni ya Norconsult ilifikisha shauri lake katika kamisheni hiyo kupitia kwa wakili Kampuni ya IMMMA, baada ya Tanrods kuvunja mkataba kwa madai kuwa kampuni hiyo ilikuwa inajihusisha na vitendo vya kukwepa kodi.

  Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Shirika la Umeme Tanzania,(Tanesco) kuamriwa kulipa fidia ya Sh106 bilioni kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited, baada ya kuvunja mkataba.
  Uamuzi huo uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara, Novemba 15 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake, Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker.

  Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwa Tanrods italazimika kuwalipa watalaamu washauri Sh250 bilioni, ikiwa kampuni zilifungua mashtaka, zitashinda.


  Baadhi ya barabara zinazohusishwa kuibua hasara hizo ni pamoja na ile ya Marangu-Rombo Mkuu na Mwika-Kilacha ambako Tanroads, iliingia mkataba wa Sh23.4 bilioni.

  Mgogoro uliopo katika ujenzi wa kuboresha barabara hiyo, unatokana na mkandarasi kufukuzwa katika eneo la ujenzi akidaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

  Mgogoro mwingine ni kati ya Tanroads na kampuni ya PRISMO-BADR, ulioko katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ukihusisha madai ya malipo ya awali na udhamini.

  Orodha ya migogoro pia inahusisha Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Tanroads, mgogoro ambao kwa sasa upo katika Mahakama ya Biashara na Tanroads inadai kurejeshewa malipo ya awali na dhamana kutoka benki hiyo. Hapa, Tanroad inadai Sh6.3 bilioni.

  Mgogoro mwingine unahusisha Shirika la China Estate Construction Eng. (CSCEC), ukihusisha kuboresha kiwango cha Barabara ya Kigoma-Lusahunga, deni likiwa Sh46.8 bilioni.

  Kampuni nyingine iliyoko katika mgogoro na Tanroads ni pamoja na Roughton International, Kundasingh, Shabbirdin & Associate na Grineker-LTA Ltd.

  Kampuni nyingine ni Konoike iliyoingia mkataba wa Sh103.47 bilioni na Tanrods. Mkataba huo ulihusu kubuni na kujenga Barabara ya Dodoma-Manyoni.

  Shauri la kampuni ya Konoike na Tanroads kwa sasa liko katika Mahakama ya Usuluhishi jijini London, Uingereza, na kampuni hiyo inatajwa kufukuzwa kwenye eneo la ujenzi baada ya kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.
  Shauri ambalo limetolewa maamuzi sasa ni lile la mkataba wa Sh1.39 bilioni kati ya kampuni ya Norconsult AS dhidi ya Tanroads
   
Loading...