Muda huu mahindi ambayo yamelimwa kandokando ya barabara ya Kasulu yanafyekwa na TANROADS muda huu chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kitengo cha FFU.
Mahindi hayo ambayo yalikuwa yamekaribia kuvunwa yamefyekwa kwa amri ya kiongozi wa TANROADS hapa Kigoma na sasa wako maeneo ya Gungu stendi mpya.
Wakati hali ya hewa ni tata hapa Kigoma inasikitisha kuona TANROADS wakiharibu mazao hayo huku wahusika wakiachwa wakitoa machozi kuona kitendo hiki kikifanyika bila kujali hali tete ya hewa ambayo imeikumba nchi nzima.
Wadau hali hiyo inapaswa kuvumiliwa kweli bila hatua kuchukuliwa hatua kali dhidi ya bosi wa TANROADS Kigoma?