TANROADS hiki kipande cha barabara huku Ununio mnataka mpaka watu wafe sio?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,094
2,000
Juzi kati kuna jamaa katoka huko nduki kafika hapo katumbukia mtaroni mwezi uliopita gari la Driving school lilitumbukia hapo.

Leo nimeshuhudia magari mawili tena yanakwaruzana hapo kila mmoja akigombea upande mzuri wa barabara. But why!?

Nini kinachokwaza ninyi kuziba hiki kipande ambacho ni mbadala wa kupunguza foleni New Bagamoyo road. Asubuhi panakuwa na foleni hapa sababu ya kipande kipana tu ambacho hamjawajibika.

TUNAWATAKA mtengeneze kipande hiki mara moja. Msisubiri matokeo hasi kwenu au watumiaji wa barabara.

Kipande nachozungumzia kipo jirani na UWANJA WA MICHEZO UNUNIO karibu na ST. ANDREA CATHOLIC CHURCH.

20200712_151435.jpg
20200712_151443.jpg
 

blance86

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,506
2,000
Hii kipande walikiboa bila sababu tu bora wangeacha vile vile tu,toka watu wanazikwa usiku mpk leo aisee huu ni uzembe.
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,094
2,000
Tatizo diwani wa kunduchi ana car wash yake hapo hapo na yeye anashindaga hapo hapo na kabenz kake kekundu lakini haoni kabisa hilo tatizo.

Huyu Diwani Urio ni bure kabisa!
Hapa wa kuwajibika ni agency husika iwe TANROADS au tarura huyo wacha aendelee kuosha bodaboda hapo watoto wapate ya nauli shule
 

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,754
2,000
Hapo ndiyo Ununio?? Hapo si kanisani Roman Catholic Bahari Beach!
Mpaka wa ununio na bahari Beach ni Kona ya Kwenda Ras ya Kilomoni.

Kipande Kimekaa vibaya sana kila upande wa site kungia kuna shimo kubwa ila pa kutokea hakuna shimo hivyo dereva atataka kupita site ya mwenzake ambapo hakuna shimo na kurudi site yake napo hakuna shimo hivyo inaweza kusababisha ajali.
 

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,485
2,000
Barabara za halmashauri zote zimekabidhiwa TARURA ,TANROAD barabara zao zile Kubwa >30m
Lakini kipande cha kuanzia JKT Mbweni pale kwenye daraja la mto unaoingia baharini, kupitia nyumba za National House kuelekea Mbweni Oceanic hadi Ubungo kutokezea Mbweni Mpiji, ile barabara inahudumiwa na TANROADS. TARURA itakua wameishia pale kwenye kona ya eneo la NSSF kwenda JKT darajani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom