TANROADS hapa mmetumia akili niliyokuwa naifikiria

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
572
356
Nimeona jana maeneo ya Mbezi Temboni magreda yakitengeneza service roads mwisho mwa eneo lao la road reserve kama sehemu ya kuwazuia watu kung'ang'ania ndani ya road reserve baada ya bomoa bomoa ya Kimara Kiluvya. Hii ndio njia nzuri na salama ya kuwafanya watu waheshimu mipaka ya barabara. Wekeni hizo barabara za pembeni kama sehemu pia ya kuonesha mipaka yenu pamoja na yale mawe kwa maana ya kwamba mkimaliza mhakikishe mawe yote ya mipaka yanaonekana maana mengine yapo uwani na ndani ya nyumba za watu na wengine kwa ujinga wanayahamisha kimtindo ili wabaki ndani ya road reserve.

Lakini pia mhakikishe pia hamfanyi ubaguzi katika kuwaondoa watu kwenye road reserve kwani wakati hata makanisa, shell na maghorofa yamevunjwa tunaona bado kuna watu wanaendelea kuwemo ndani ya road reserve wakiendelea kuishi, kufanya biashara mfano za baa, kufyatua tofari na mbao wakati huo huo utakuta wanapita na magreda kuvunja vunja hata miavuli na vibanda vya mama ntilie. Hapo ndio huwa tunashindwa kuelewa hao wanaoendela kuishi humo, wenye mabaa, na wafyatua matofari waliomo ndani ya reserve wanamkataba na Tanroads?! Maana haiwezekani wengine wakawa wanatimuliwa mara kwa mara na vibanda vyao vibovu lakini wengine wanaachwa tu hata hawaguswi kama lengo ni kuondoa wote hao wengine ni akina nani? Mnapo waacha watu wanajiimarisha halafu baadaye mnakuja kuwavunjia mnawatia hasara sana.

Kwa wananchi wenzangu hebu tutii sheria bila shurti. Mtu umeshaambiwa ondoka unahangaika kufuta futa X kana kwamba nchi imekwisha hakuna pa kwenda. Wakati wenzako wanaondoka na kwenda kuanza maisha sehemu nyingine wewe unang'ang'ania hapo hadi siku wanakuvunjia huana hata kibanda cha kuishi badala yake unabaki kupiga piga kelele. Hebu jifunzeni sasa kwani hata serikali inabomoa majengo yake tena yenye thamani ya mabilioni!
 
Mpewa Muda wa kusherehea kwny Nyumba zenu kabla ya kugeuzwa kifusi cha kujengea
 
Back
Top Bottom