TANROAD mnakwama wapi mpaka kushindwa kurekebisha barabara mkoani Shinyanga?

tatamajuva

Member
Sep 11, 2019
74
83
Barabara kutoka Kahama kupitia Msalala jimboni kwa Maige kupitia Mwakitolyo-Mhangu - Misasi wilayani Misungwi imekatika maeneo mengi, eneo la Mwanzugi wilayani Msalala barabara imebomoka na Tanroad wapo likizo hakuna kinachoendelea, huku watu wakitaabika, akina mama wajawazito wanajifungulia njiani kutokana na ubovu wa barabara, eneo la Mwakitolyo.

Wilayani Shinyanga nako barabara haipitiki kutokana na kuharibika maeneo kama manne hivi na wamebuni usafiri wa mitumbwi kuvuka eneo hilo, bidhaa zimepanda bei maradufu, huduma mbalimbali kama afya zimekwama,

Mheshimiwa Rais mpenda watu, mulika TANROAD Mkoa wa shinyanga .

Nina hakika kambi za jeshi zikisaidia kujenga barabara hii watatumia muda mfupi na watajenga madaraja imara chini ya usimamizi wa Tanroad
IMG_20200309_171910.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua bei ya vifaa vya kujenga barabara? Google bei ya vifaa ndio utaelewa kwa nini barabara ni shida kuzijenga.
 
TARURA....
Hata hivyo ni vema wananchi tukachukua route nyingine kwa kuwa mvua hizi nazo uchangia hasara hasa pale tunapojenga miundombinu kipindi chake.
 
Me nasema serikali iingie mkataba na sekta binafsi katika ujenzi wa barabara na igawane share na wahusika.

Mfano iseme serikali wachangie 40% ya gharama za ujenzi na watu binafsi wachangie asilimia 60% kisha hizi barabara zinawekewa kizuizi watu wapite kwa kulipia kulingana na uzito tofauti.... Utaona hizo barabara zitakazojengwa kila kona kwa mashindano......

Serikali haijui kucheza na akili za wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni yale matuta tu nikikatiza pale town Shinyanga kwenda Mwanza..aisee ni shida..
 
tatamajuva, Kama tanroad hawajapewa hela wanaenda kutengeneza na nini? Hela iliyobaki kwasasa ni ya kununua wapinzani na kampeni 2020.
 
Back
Top Bottom