TANROAD mkoa wa Pwani na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bamba Kongowe, wanawadhurlmu Wafanyabiashara wadogo wadogo

Askari Mnoko

Senior Member
Oct 5, 2019
149
101
TANROAD mkoa wa Pwani, kwa kushirikiana na mwenyekiti wa Serikari ya Mtaa wa Bamba uliopo Kongowe, katika wilaya ya Kibaha. Wanaendekeza dhuluma dhidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo, wanaofanya shughuli zao katika eneo la hifadhi ya barabara, kwa kuwatoza Kodi Kila mwezi, kiasi Cha tsh 30,000/ na tsh 15,000/.

Kiasi hicho cha Kodi ukusanywa na mama Mmacha, ambaye anadai amemilikishwa eneo Hilo la hifadhi ya barabara na TANROAD mkoa wa Pwani, wakati Kuna alama kubwa ya mawe ya TANROAD. Baada ya kukusanya Kodi ndiyo mgao wa makusanyo hufanyika.

Wafanyabiashara wadogowadogo walijaribu kufuatilia uhalali wa mama Mmacha wa kukusanya Kodi, lakini waliambulia vitisho kutoka kwa uongozi wa Serikari ya Mtaa wa Bamba,"Kama mnataka kufanyabiashara lipeni Kodi na kama hamtaki kumlipa Kodi mama Mmacha acheni kufanya biashara".

Wanajamvi ninawaomba mtupe ushauri, hatua gani tuchukue kukomesha dhulma hii dhidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo.
 
Mkoa wa pwani kuna Mahakama,kituo cha polisi na TAKUKURU unazifahamu zilipo ofisi zao? Au we mnoko asiyejua kitu.
 
Mkoa wa pwani kuna Mahakama,kituo cha polisi na TAKUKURU unazifahamu zilipo ofisi zao? Au we mnoko asiyejua kitu.
Mkuu tunaomba ushauri,hili tujue malalamiko yetu tuyapeleke wapi? Tuanze kufungua kesi mahakamani? au twende TAkUKURU,au tukatoe taarifa polisi! Ingawa walinda usalama nao hawajambo wanapopenyezewa rupia,ukweli uwekwa kapuni.
 
Kwanza tuanze wewe unanafasi gani katika jamii unayoishi hapo?
Kiongozi au raia wa kawaida?
 
Mkuu tunaomba ushauri,hili tujue malalamiko yetu tuyapeleke wapi? Tuanze kufungua kesi mahakamani? au twende TAkUKURU,au tukatoe taarifa polisi! Ingawa walinda usalama nao hawajambo wanapopenyezewa rupia,ukweli uwekwa kapuni.
Je ni mhanga au msamalia mwema? Umetoa tu taarifa.
 
Je ni mhanga au msamalia mwema? Umetoa tu taarifa.
Mimi ni muhanga,ni Jambo linalonikera kumlipa pesa mtu Kodi,wakati si mmiliki wa eneo husika,pia hata rais aliruhusu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo,kufanya kandokando ya barabara biashara ,ili mradi wasivunje Sheria.
 
Back
Top Bottom