Jana tarehe 20 Oktoba TANROAD wamezua taharuki kwa wakazi wa Morogoro baada ya kupita kimya kimya bila ya kuongea na mtu wakipiga X nyekundu na kuandika Bomoa kwenye kuta za nyumba.
Nyumba hizo ambazo ni za makazi na nyingine zimepangishwa kama fremu kwa wafanyabiashara zipo eneo la katikati ya barabara inayotumika kwa sasa na ile ya zamani.
Ni barabara kuanzia Kwa Chambo kupita mizani ya zamani ya Kihonda, Mkundi Mwisho kuelekea Makunganya. Baadhi ya wananchi walisikika wakidai kwa nini X ziwekwe wiki hii ya mwisho ya kampeni wakati wanajua hawawezi kubomoa leo wala kesho.
Wananchi kadhaa walisikika wakidai kuwa watumishi wote wamemchoka Magufuli na CCM yake walichofanya TANROAD wanafanya hata wakubwa wa idara mbalimbali kumchonganisha na wananchi ili kuwajaza hasira wasimchague tena.
.