TANROAD mkoa wa Morogoro kupiga X nyekundu Bomoa nyumba kando ya barabara Moro - Dodoma kata ya Mkundi, wiki moja kabla ya uchaguzi tuwaeleweje?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,328
2,000
Ukisikia tengeneza tatizo kwa makusudi kisha tatua ili majuha wakushangilie, ndiyo hiyo sasa!

Hapo wanajua Magu wakati anaenda Dodoma kumalizia ratiba ya kampeni, atasimama hapo na kusema "...hakuna kuwabomolea wananchi nyumba"!

Weka hii post sticky
Na hilo ndilo litakalofanyika
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,328
2,000
Fuata sheria! Usitake huruma ya uchaguzi, hata kama itakuwa miaka 50 ijayo kuna watu utawaponza. Waulize waliokuwa ubungo mataa na wana Kimara.

Usanii tu, soon Magufuli akipita hapo utasikia anasema, hataki wananchi wake wabomolewe nyumba zao!.

Hii ni Kampeni tu hii hakuna lolote watu tumeshamstukia!. Jiwe anajibu hoja za Lissu kwa kutumia ulaghai na umachiavelli

Ni kama issue ya walimu ngazi ya Cheti. Asubuhi anatengeneza tatizo, jioni anatoa suluhu kwa kusema kuwa waendelee na kazi na eti anawapenda sana

Jamaa ni msanii ajabu
 

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
2,662
2,000
Hivi kati ya hao wakazi na barabara nani alimkuta mwenzake? Je kama walikutwa walilipwa kupisha?

Kama walikuta ipo, kwanini walijenga karibu na Hapo Maana sheria zake zipo wazi. Ukiukuta mradi na kujenga, utavunjiwa na hulipwi hata senti tano
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom