TANROAD Dar mtalipa uhai wa Watu na magari kwa uzembe huu? Au Rushwa imewatoboa macho hamuoni?

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
887
500
Habari wana jukwaa,

Nimeanza na kichwa hapo. leo ni siku ya 4 mkandarasi amekata rami barabara ya Old Bagamoyo Road ili kufanya marekebisho lakini mashimo yalikatwa mengi na makubwa na yana sharp edge, na hakuna tahadhari au onyo yoyote iliyowekwa kuwa kuna ujenzi unaendelea. Juzi usiku kuna gari ilipasua taili mbili za mbele na kudondoka maeneo ya UNUNIO MABWAWA YA CHUMVI kwenye kona kali huku barabara ikiwa ni nyembamba. Leo asubuhi karo ndogo yenye taili low profile imepasua taili 3.

SWALI: Kwanini mkandarasi anakata mashimo na yanachukua muda mrefu bila matengenezo?

Uzoefu unaonyesha kuwa mkandarasi akipewa kazi anapeleka vifaa site then anachimba chimba harafu anaondoka miezi.

Kuna mkandarasi pale GAIRO- barabara ya Dodoma, na Kingolwira Morogoro wamechimba barabara kulia na kushoto urefu km 1 hivi na mashimo lenye urefu wa 70CM hivi. Mwaka 2018 kuna mashimomengi ya kutosha yalikatwa kati kati ya barabara eneo la chamakweza karibu na Chalinze siku moja magari zaidi ya 20 yalipasua matairi na kusababisha ajali. Mwaka jana 2019 kuna uzembe wa mkandarasi aliyekuwa anajenga daraja alisababisha ajari nyingi barabara ya Dodoma eneo la MBANDE nafikiri kuna kiongozi alipata ajari eneo hili kwani hapakuwa na tahadhari yoyote.

Kwanini TANROAD AU TARURA hawaoni matatizo ya wakandarasi hawa? kuna nini kiasi kwamba safety katika ujenzi haichukuliwi umuhimu?
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,486
2,000
Huwa hata sielewi ni nani anatakiwa kuwawajibisha maana unakuta unapita sehemu unashtukia bonge la shimo unaliingia mzima mzima.
 
Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
1,100
2,000
Hiyo road ya Dodoma ni hatari sana. Kuna sehem wametifua tifua wanaacha ala Ni darajani sana sijui wanakuwa na lengo gani
 
Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
5,463
2,000
Ni wapuuzi sana wangekuwa wanakata usiku na ku repair usiku usiku ,sio wanakata vipande karibia kilometer moja halafu wanayaacha tu.
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
21,529
2,000
Hapo Kingolwira Morogoro
Tangu Kitambo Mkandarasi Hafanyi Lolote Isipokuwa Eneo Kimekuwa Hatari Sana

Kibaya Sasa Hivi Askari Wa Kingolwira Wanasimamisha Magari Hapo Hapo Mpaka Hapapitiki. Gairo Napo Hatari
 
Usiku ni hatari zaidi, ukijichanganya ukiingia pembeni unadondosha gari kwa sababu kimo cha ngema ni zaidi ya mita moja kwenda chini. ikitokea ukabanwa ina bidi usiburi head on collision.
 
MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
887
500
Hili ni tatizo sugu!..tunaharibu sana magari!
Siyo kuharibu tu wanaua watu, ukiona kimya TANROAD hachukui hatua ujue kuna Rupia ilipenyezwa. Ukiuuliza utaambiwa ni contractor class one or two. Kama contractor wazawa hawatabadirika bora wapewe wageni kandarasi.
 
kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,498
2,000
Mwana juzi mi usiku nimekutana nayo, harafu wameyakata vizuri ,wakaacha wakaondoka,harafu sijui Kwanini hawamalizagi lile eneo
 
Silasy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
641
1,000
Kwakweli hii kitu ni uonevu kwasisi watumiaji wa barabara na walipa kodi last 2 weeks gari yangu imepasua tairi moja na mengine yote matatu yamevimba kwaajili ya kukita kwenye Mashimo km hayo Kilwa road na Chang'ombe ,gharama ya Tairi moja 180,000/= inaniuma sana ukizingatia yote bado ni mapya!
Huwa najiuliza kuna sehemu tunaweza kupeleka madai ya uharibifu wa mali unaotokana na uzembe wa watoa huduma tukalipwa?
 
Fidakasa

Member
May 14, 2013
83
225

Kuna jambo linatakuwa kufanyika katika kila taasisi ya serikali kuwe na indepent part ya kusikiliza malalamiko ya watu.
Sio mlalamikiwa ndio msikilizaji hapa haitakua sawa.
 
Bu'yaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,256
2,000
Leo asubuhi karo ndogo yenye taili low profile imepasua taili 3.
Makandarasi na waajiri wao TANRODS na TARURA ni majanga.

Lakini unapofunga vitairi vya low profile huku kwenye third world terrain usije kulalamika kwamba yamepasuliwa na barabara mbovu!
 
lordchimkwese

JF-Expert Member
Nov 16, 2015
960
1,000
Huku low profile na vigari vya chini hakuna rangi utaacha ona barabara nzima chache sana yani mtu ukiwa road gari inadunda dunda ka kitenesi doh barabara ka matuta ya viazi afu wanaita lami
Makandarasi na waajiri wao TANRODS na TARURA ni majanga.

Lakini unapofunga vitairi vya low profile huku kwenye third world terrain usije kulalamika kwamba yamepasuliwa na barabara mbovu!
 
Mario Kejob

Member
Apr 14, 2020
80
125
An area just passed Gairo(Mbande) I guess, toward Dodoma, I almost perished after running into unmarked bump and immediately followed by a huge pothole digged by those mucky mouse contractors.
The time has come to make a tough choice between the local contractors who does shoddy works and endangering the lives of the motorists (uzalendo) or hiring capable and qualified contractors who can do the job better and efficiently.
Just a reminder, Tanroad should do routine inspection and maintenance to make sure our roads are safe to avoid accidents and carnages.
The choice is ours.
 
Jikombe

JF-Expert Member
May 13, 2010
351
250
Habari wana jukwaa,

Nimeanza na kichwa hapo. leo ni siku ya 4 mkandarasi amekata rami barabara ya Old Bagamoyo Road ili kufanya marekebisho lakini mashimo yalikatwa mengi na makubwa na yana sharp edge, na hakuna tahadhari au onyo yoyote iliyowekwa kuwa kuna ujenzi unaendelea. Juzi usiku kuna gari ilipasua taili mbili za mbele na kudondoka maeneo ya UNUNIO MABWAWA YA CHUMVI kwenye kona kali huku barabara ikiwa ni nyembamba. Leo asubuhi karo ndogo yenye taili low profile imepasua taili 3.

SWALI: Kwanini mkandarasi anakata mashimo na yanachukua muda mrefu bila matengenezo?

Uzoefu unaonyesha kuwa mkandarasi akipewa kazi anapeleka vifaa site then anachimba chimba harafu anaondoka miezi.

Kuna mkandarasi pale GAIRO- barabara ya Dodoma, na Kingolwira Morogoro wamechimba barabara kulia na kushoto urefu km 1 hivi na mashimo lenye urefu wa 70CM hivi. Mwaka 2018 kuna mashimomengi ya kutosha yalikatwa kati kati ya barabara eneo la chamakweza karibu na Chalinze siku moja magari zaidi ya 20 yalipasua matairi na kusababisha ajali. Mwaka jana 2019 kuna uzembe wa mkandarasi aliyekuwa anajenga daraja alisababisha ajari nyingi barabara ya Dodoma eneo la MBANDE nafikiri kuna kiongozi alipata ajari eneo hili kwani hapakuwa na tahadhari yoyote.

Kwanini TANROAD AU TARURA hawaoni matatizo ya wakandarasi hawa? kuna nini kiasi kwamba safety katika ujenzi haichukuliwi umuhimu?
Tatizo la mashimo kukaa muda mrefu ni la Tanroads zaidi. Kwani mkandarasi akishakata shimo usubiri Tanroads waje wa approve ndipo aendelee na next stages. Sasa unakuta Tanroads haji kwa wakati labda kutokana na uchache wa manpower ama magari.
Issues ya Signs inaweza sababishwa madereva kutokuwa makini kusoma vibao vya signs kwani madereva walio wengi uwa wanajiachia tu nyakati za usiku. Pia kuna suala la kuiba hivyo vibao na maranyingi ufanywa na wenyeji wa eneo husika ili wanufaike na ajali ikitokea.
Tatizo siyo competence ya local Contractors kama wengi wanavyo hisi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom