Tanroad arusha mmekuwa kero tena kero kubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanroad arusha mmekuwa kero tena kero kubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GIB, May 10, 2012.

 1. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwa cha habari chahusika.
  Sisi watumiaji wa barabara ya moshi arusha tumeletewa kero tena kero ya mwaka. Maneja wa TANROAD arusha sijui kwa maslahi ya nani ameamua kuanzisha mizani bubu pale KIKATITI.
  Hii mizani bubu wengine wanaita mkeka ikiwa na watumishi wenye kiburi na majibu ya dharau kwasisi watumiaji wa hii barabara.
  Sehemu hiyo ya kikatiti ni nyembamba sana, hivyo kusababisha foleni ndefu isiyo elezeka. kwani tulisubiri kwanye foleni kwa zaidi ya saa moja , mabasi ya abiria na malori ya mizigo yote yanagombania kupima kwenye hiyo mizani moja.
  Cha ajabu zaidi inaonekana nimradi wa kukusanya pesa, kwani leo ni siku kama ya nne hakuna gari hata moja lililo kamatwa kwa kuzidisha mzigo. je hakuna magari yaliyo zidisha mzigo? ukweli nikwamba wanaendeleza utaratibu wa chukua chako mapema. Je hizo pesa zinazokusanywa zimaenda wapi?
  Mh. Dr, Mzee wa data, najua wajua kunamizani ngapi tanzania nzima pomoja na mahali zilipo. Je unaijua mizani hii inayobebla kwenye gari la TANROAD lanye namber STG 8?. Naje hizii pesa zinashokusanywa hapo unazo taarifa zake?
  Najua nimuhimu kulinda barabara zetu, je hakuna utaratibu au sehemu nzuri ya kupimia hadi pale katiti? hamuoni tatizo kusababisha kero hii? au mpaka tuandamane ?
  Hii mizani imekuwa kero sana tena sana. Meneja kumbuka kutoka katiti hadi njia panda ya himo kwenye mizani nyinginehakuna kilometer 150. je unazani gari likipima pale himo ni lazima lije kupima tena hapo katiti , jamani hii nikero tena kero.
  Nawakilisha.
  source : mimi mwenyewe
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, nilikutana nayo juzi! Yaani ni kero kwel kwel. Malori na mabasi yanagombania kupima na yanasababisha foleni kubwa huku trafiki wakizidiwa nguvu. Ni kero kubwa!
   
 3. T

  Turbulence Senior Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni maamuzi mengine ya kipumbavu yanayorudisha nyuma gurudumu la maendeleo. Ni juzi tu tulikuwa tunajadiliana kuhusu kupunguza mizani/roadblocks ili ku-facilitate trade. Tanzania tumeji-comit EAC kuwa tutapunguza visumbufu vya aina hiyo ambavyo vinachelewesha usafirishaji wa mizigo. Crazy crazy crazy!!!!! Halafu tunashangaa kuwa tunashuka kwenye Doing Business ranks. Inatakiwa kuanzisha utaratibu ambao watu wanaoleta maamuzi ya kipumbavu kama huo wapewe adhabu kali. Tujifunze kutoka China na Rwanda jamani. Daaah. Inaboa.
   
Loading...