TANLAP: Kilimanjaro, Mbeya na Njombe kuna changamoto za ukatili wa kijinsia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Imeelezwa kuwa Mikoa mitatu ikiwemo Kilimanjaro,Mbeya na Njombe bado zina kabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto hivyo elimu na msaada wa kisheria unahitajika.

Hayo yameelezwa Juni 29.2021 na Mchereli Machumbana, Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa kutoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP) akiwa Kata ya Mwika Kaskazini, Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mtando huo umefika kuwapatia wananchi elimu ya msaada wa kisheria bure ikiwemo kuwawezesha wanawake kufikia haki zao kwa wakati, ukatili wa kijinsia,Mirathi,migogoro ya ardhi, kuwawezesha kiuchumi na kuwawezesha kushiriki katika vyombo vya kufanya mamuzi kwa ngazi zote.

Alisema kuwa mikoa hiyo mitatu ilipendekezwa na mtandao huo kwa kushirikiana na Serikali ngazi ya Mkoa ambapo ilipendekeza Wilaya na Kata na kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro maeneo yaliyopendekezwa na serikali ni Wilaya ya Moshi na Rombo.

“Maeneo haya yaliyo chaguliwa ni baada ya majadiliano na vipaumbele vya serikali katika kuona maeneo hayo kuendelea kuwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia hasa Wilaya ya Rombo na Moshi kwa Mkoa wa Kilimanjaro, Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya ni Wilaya ya Mbarali na Rungwe na Mkoa wa Njombe ni wilaya ya Ludewa na Makete ambazo bado zina tatizo la ukatili wa kijisia hasa kwa watoto na wanawake”alisema Machumbana.

Alisema kuwa tatizo la kuendelea kuwepo ukatili wa kijinsia ni kutokana na utamaduni wa watu,mila,desturi na mitazamo hivyo bado elimu inapaswa kutolewa zaidi kwani vitendo hivyo haviathiri tu wahusika bali ni taifa kwa ujumla katika kupambana kukomesha vitendo hivyo kwa kutumia rasilimali zake.

Machumbana aliongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa Wanawake wengi bado wananyanyasika ukilinganisha na wanaume pamoja na watoto kunyanyasika kuliko wanaume.

“Wanaume wanaonekana kutumia nguvu kimtizamo na wakinyanyasika inaonekana kuwa ji fedhe ha kwao hivyo wanashindwa kujitokeza,kesi za wanaume kunyanyasika tunazipokea na wanakaribishwa poa katika madawati ya jinsia na watoto katika wilaya zao” alisema Machumbana.

Kwa upande wake Mwananchi (Mwanamke) aliyefika kupata huduma hiyo kwa masharti ya kutokuandikwa jina lake ameshukuru mtandao huo wa TANLAP kwa kufika katika kata hiyo na kutoa elimu na usaidizi wa kisheria kwa madai kuwa wanawake ndio wanao taabika na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Tatizo linaanza pale unapo fiwa na kubaki mjane ndugu wa mume ndio wanachochea ukatili wa kijinsia kwa kumfukuza mjane au kuchukua mali za mjane na watoto kuachishwa shule,ukweli wanawake tunateseka sana hasa huku vijijini ukifiwa na mume tuu mwanzo wa kuingia katika dunia ya mateso unaanzia hapo” alisema.

Katika mkutano huo wa kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na usaidizi wa kisheria bure wananchi wameliomba shirika hilo kuwatembelea mara kwa mara hasa kwa kuingia vijijini zaidi kwani huko ndiko kwenye matatizo mengi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
 
Hata K lyn wamemfanyia ukatili baada ya kufiwa na mme wake.
Unaongea kirahisi sana lakini hujui ukweli.

Kinachofanywa ni kulinda heshima ya aliekufa na kuwasaidia watoto wake watakapo kuwa wakubwa. Ukimwachia mwanamke mali bado ataolewa au ataleta mwanaume mwingine aje azichezee.

Hii inatokana na wanawake wenyewe japo sio wote.
 
Mi nawatetea wanaume wa Rombo. Wanaume wa Rombo ndo wananyanyaswa maana wake zao hufuata michepuko upande wa Kenya kwa kisingizio eti waRombo hawana nguvu za kiume.
 
Imeelezwa kuwa Mikoa mitatu ikiwemo Kilimanjaro,Mbeya na Njombe bado zina kabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto hivyo elimu na msaada wa kisheria unahitajika.

Hayo yameelezwa Juni 29.2021 na Mchereli Machumbana, Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa kutoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP) akiwa Kata ya Mwika Kaskazini, Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mtando huo umefika kuwapatia wananchi elimu ya msaada wa kisheria bure ikiwemo kuwawezesha wanawake kufikia haki zao kwa wakati, ukatili wa kijinsia,Mirathi,migogoro ya ardhi, kuwawezesha kiuchumi na kuwawezesha kushiriki katika vyombo vya kufanya mamuzi kwa ngazi zote.

Alisema kuwa mikoa hiyo mitatu ilipendekezwa na mtandao huo kwa kushirikiana na Serikali ngazi ya Mkoa ambapo ilipendekeza Wilaya na Kata na kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro maeneo yaliyopendekezwa na serikali ni Wilaya ya Moshi na Rombo.

“Maeneo haya yaliyo chaguliwa ni baada ya majadiliano na vipaumbele vya serikali katika kuona maeneo hayo kuendelea kuwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia hasa Wilaya ya Rombo na Moshi kwa Mkoa wa Kilimanjaro, Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya ni Wilaya ya Mbarali na Rungwe na Mkoa wa Njombe ni wilaya ya Ludewa na Makete ambazo bado zina tatizo la ukatili wa kijisia hasa kwa watoto na wanawake”alisema Machumbana.

Alisema kuwa tatizo la kuendelea kuwepo ukatili wa kijinsia ni kutokana na utamaduni wa watu,mila,desturi na mitazamo hivyo bado elimu inapaswa kutolewa zaidi kwani vitendo hivyo haviathiri tu wahusika bali ni taifa kwa ujumla katika kupambana kukomesha vitendo hivyo kwa kutumia rasilimali zake.

Machumbana aliongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa Wanawake wengi bado wananyanyasika ukilinganisha na wanaume pamoja na watoto kunyanyasika kuliko wanaume.

“Wanaume wanaonekana kutumia nguvu kimtizamo na wakinyanyasika inaonekana kuwa ji fedhe ha kwao hivyo wanashindwa kujitokeza,kesi za wanaume kunyanyasika tunazipokea na wanakaribishwa poa katika madawati ya jinsia na watoto katika wilaya zao” alisema Machumbana.

Kwa upande wake Mwananchi (Mwanamke) aliyefika kupata huduma hiyo kwa masharti ya kutokuandikwa jina lake ameshukuru mtandao huo wa TANLAP kwa kufika katika kata hiyo na kutoa elimu na usaidizi wa kisheria kwa madai kuwa wanawake ndio wanao taabika na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Tatizo linaanza pale unapo fiwa na kubaki mjane ndugu wa mume ndio wanachochea ukatili wa kijinsia kwa kumfukuza mjane au kuchukua mali za mjane na watoto kuachishwa shule,ukweli wanawake tunateseka sana hasa huku vijijini ukifiwa na mume tuu mwanzo wa kuingia katika dunia ya mateso unaanzia hapo” alisema.

Katika mkutano huo wa kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na usaidizi wa kisheria bure wananchi wameliomba shirika hilo kuwatembelea mara kwa mara hasa kwa kuingia vijijini zaidi kwani huko ndiko kwenye matatizo mengi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Kwa hali hii ya hewa mtu akunyime lazima kipigo kihusike
FB_IMG_16251351158090947.jpg
 
Back
Top Bottom