Tanil Somaiya kukutana na waandishi

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Tanil Somaiya anatarajia kukutana na waandishi wa habari hapo kesho.

Tutajitahidi kupata kinachoendelea katika mkutano huo.

Mh, tunakoelekea...!
 
Mengi amewasha moto ambao hawezi kuuzima! Busara za mtu kama Nyerere zinahitajika kwani naona huu mziki ni mkubwa kwa JK! Sijui tumwite Koffi Annani maana hapa nchini sijui nani wa kumnyooshea mwenzake kidole! Wote ni wizi mtupu!
 
CCM inawasukuma watu wake akina RA na hao wahindi wengine kusema lolote maana uchaguzi unakaribia na kila kigogo wa CCM anautaka ushindi mwaka 2010.The State and CCM has come between .Wacha tuangalie sasa .
 
Tanil Somaiya anatarajia kukutana na waandishi wa habari hapo kesho.

Tutajitahidi kupata kinachoendelea katika mkutano huo.

Mh, tunakoelekea...!

Mkuu huko tunakoenda ndio ukombozi wa mtanzania. Wacha yatokee yoyote hata kwa gharama fulani kwani mwisho wake watanzania walio wengi wataneemeka
 
Mengi amewasha moto ambao hawezi kuuzima! Busara za mtu kama Nyerere zinahitajika kwani naona huu mziki ni mkubwa kwa JK! Sijui tumwite Koffi Annani maana hapa nchini sijui nani wa kumnyooshea mwenzake kidole! Wote ni wizi mtupu!

Huu moto hauhitajiki kuzimwa maana unaunguza magugu tu. Tumshukuru Mengi kwa kuuwasha.

Tatizo ni kuwa unavyoendelea kuwaka ni nani kwenye uongozi wa sasa wa CCM atakayepona?
 
Haponi mtu hapa..na hamna mtu wa serikali atakaye ingilia...sophia simba ameshajichoma kwa kudandia bila kufikiria!!
 
Kazi ipo wakuu sasa sisi wenye nchi wazalendoo.....tumebakia hatuna chetu wanatamba wao tu kazi kweli kweli....
 
nakuunga mkono kufanya maandamano ya kumuunga mkono mengi.
tunahitaji kufanya maandamano.
 
nakuunga mkono kufanya maandamano ya kumuunga mkono mengi.
tunahitaji kufanya maandamano.

Yakifanyika yatazuiwa kwa nguvu kubwa na serikali huwezi amini!! Lakini yakifanyika yakumuunga mkono mheshimiwa sana mbunge wa Igunga Rostam kwa utetezi wake......yatasindikizwa na TOT huku John Komba akitumuiza!
 
Mengi amewasha moto ambao hawezi kuuzima! Busara za mtu kama Nyerere zinahitajika kwani naona huu mziki ni mkubwa kwa JK! Sijui tumwite Koffi Annani maana hapa nchini sijui nani wa kumnyooshea mwenzake kidole! Wote ni wizi mtupu!

Mkuu hapo umekosea;

Hakuhitaji kuuzima... alitaka uwake haswa na kila kitu kiwe wazi!!!

He did what he did intentionally and just to let you know that this chaos was necessary if we are to transform; kinachotokea sasa ni bora kuliko industrial revolution waliyofanya wenzetu zamani....

Yeye ni kama suicide bomber anayetumika kudeliver messages - HE IS A CHANGE AGENT MAZEE
 
SS alifikiria alichosema baada ya kumaliza ule mkutano
sidhani kama alifikiria, maana kesho yake live on TBC, aliyatamka tena maneno yale yale kwa lugha ya 'kishankupe' huku akiyatilia msisitizo wa kidole juu, mdomo akiubinjuwa. hapo kuna kufikiria kweli?.
 
Mengi amewasha moto ambao hawezi kuuzima! Busara za mtu kama Nyerere zinahitajika kwani naona huu mziki ni mkubwa kwa JK! Sijui tumwite Koffi Annani maana hapa nchini sijui nani wa kumnyooshea mwenzake kidole! Wote ni wizi mtupu!
Ndipo kila mmoja anapopataka wasipoongea hatutajua kitu wacha wajichanganye tupate pa kupitia. Asante Mengi kwa kufanya mabubu kuongea.
 
sasa basi Mengi inabidi aahirishe mkutano wake leo ili afanye baada ya kumsikia huyu fisadi papa mwengine. vita hii lazima wananchi tushinde.
 
sidhani kama alifikiria, maana kesho yake live on TBC, aliyatamka tena maneno yale yale kwa lugha ya 'kishankupe' huku akiyatilia msisitizo wa kidole juu, mdomo akiubinjuwa. hapo kuna kufikiria kweli?.
This made me laugh!

Na huyo ni WAZIRI... Kaazi kwelikweli
 
Sophia Simba na mwenzie Mkuchika mbona sijawasikia wakimjibu RA?....Double standards au ndo mambo ya ukipofu.....?
 
Mengi amewasha moto ambao hawezi kuuzima! Busara za mtu kama Nyerere zinahitajika kwani naona huu mziki ni mkubwa kwa JK! Sijui tumwite Koffi Annani maana hapa nchini sijui nani wa kumnyooshea mwenzake kidole! Wote ni wizi mtupu!

Nani kasema Mengi hawezi kuuzima? Kuwataja watu hao wa 5 alijua kabisa kwamba anaubavu nao ndio maana akafanya alivyofanya. Alikuwa na uwezo wa kuwataja wengine wengi tuu.

Kuhusu JK, sidhani kama atahusika sana na issue ambazo zinaonekana zipo kibinafsi hasa na hili lilithibitika jana baada ya RA kutoa shutuma ambazo zipo kibinafsi zaidi badala ya kutetea kwamba yeye sio FISADI
 
Back
Top Bottom