Tani 12 za cocaine zakamatwa Colombia, zaweka rekodi ya kiasi kikubwa zaidi


real G

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Messages
5,257
Likes
5,110
Points
280
Age
43
real G

real G

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2013
5,257 5,110 280
Polisi nchini Colombia wamekamata tani 12 za cocaine katika kisa ya kukamatwa kwa kiwango kikubwa zaidi cha madawa ya kulevya katika historia ya Colombia.

Madawa hayo yalipatikana yamezikwa kwenye shmba moja la ndizi kaskazini mwa nchi, karibu na njia zinazotumiwa kusafirisha cocaine kwenda Marekani.

Rais Juan Manuel Santos alisema kuwa hicho kiwango kikubwa zaidi kuwai kupatikana katika oparesheni moja ya polisi.

Oparesheni hiyo ilikuwa ni sehemu ya kulikabili genge lenye nguvu la Gulf Clan, ambalo linahusika na ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Polisi walisema kuwa madawa hayo yalikuwa ni ya Dairo Úsuga, anayejulikana pia kama Otoniel, kiongozi wa genge la Gulf Clan, moja ya magenge hatari zaidi nchini Colombia.

Vikosi vya usalama vimejaribu kumkamta Otoniel kwa miaka kadhaa.

Polisi walisema kuwa pia waliwakamata watu wanne na kukadiria kuwa madawa hayo yalikuwa ni ya thamani ya dola milioni 360.

Katika kipindi cha miezi mwili iliyopita, vikosi vya usalama vimemakama tani 20 za cocaine huko Antioquia.

Genge la Gulf Clan liliibuka kutoka kwa makundi ya mrengo wa kulia ambayo yalitawanyika mwaka 2006 kufuatia msamaha wa serikali.

Serikali inasema kuwa zaidi ya wanachama 1,500 wamekamatwa mwaka huu na kamanda wake wa cheo cha pili kuuwawa


Chanzo: BBC Swahili
 
pangalashaba

pangalashaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Messages
1,225
Likes
1,108
Points
280
pangalashaba

pangalashaba

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2011
1,225 1,108 280
Nakumbuka kitu iliitwa Hacienda Nápoles (Naples Estate) ya mzee mzima Pablo Emilio Escober Gaviria.
 
The Proudly African

The Proudly African

Senior Member
Joined
Jun 22, 2017
Messages
139
Likes
164
Points
60
The Proudly African

The Proudly African

Senior Member
Joined Jun 22, 2017
139 164 60
Hahahaha. Nilipenda hoja yake kuwa hakufanya kosa lolote as he was exploiting flowers.
 
W

wolfpack

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2013
Messages
279
Likes
168
Points
60
W

wolfpack

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2013
279 168 60
PABLO HATUNAE TENA,
EL-CHAPO YUKO NDANI,
WHO IS NEXT??
:rolleyes:
 

Forum statistics

Threads 1,250,919
Members 481,523
Posts 29,750,780