Tani 1.5 ya pembe za ndovu toka TZ zakamatwa Hong Kong

Bila shaka atakuwa yeye maana anahaingaika sana CCM ishinde ili chama hicho kiendelee kumpa cover.
 
what?? KInana huyo na meli yake anasema hajui cargo zinazobebwa na meli yake. Its very sad tunasema Tanzania masikini wakati wachache ndo vinara wa kutupeleka kwenye hilo jina.
 
Tatizo la Tanzania ni usimamiaji wa utekelezaji wa sheria za nchi, ni kama hakuna serikali. Hizi pembe za ndovu (stockpiles) ni tatizo zikiuzwa na ni tatizo zisipouzwa. Hakuna good option.
Zisipouzwa na kuendelea kuwepo kwenye mabohari: Wezi wanajua zipo kwenye maghala na zitakuwa zikiibwa kidogo kidogo kwa hiyo biashara ipo pale pale. Poaching huko kwenye mapori hatuwezi kuzuia. Tunashindwa kusimamia sheria ndogo ndogo kama za kuzuia watu kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa; hatuwezi kudhibiti maelfu ya kilomita za mraba ya mapori tunayoyaita mbuga zetu.

Zikiuzwa: Biashara itachanua. Itakuwa vigumu kujua zipi ziliuzwa kihalali na ni zipi zinatokana na tembo wanaoendelea kuuliwa kwenye mapori yetu. Yaani wafanya biashara hizi haramu watakuwa wamepata upenyo.

Zikichomwa Moto: Hasara kuchoma moto mali inayoweza kuuzwa. Lakini vile vile hakuna ushahidi kuwa kuchoma moto kutamaliza poaching inayoendelea.

Suluhisho - Serikali lazima isimamie sheria zilizopo, kama haiwezi ni juu yetu wananchi kuichukulia hatua serikali kwa kuiondoa madarakani na kuweka serikali mpya. Ikishindwa nayo tunaiondoa hadi tutakapopata serikali yenye uwezo wa kusimamia utawala wa sheria.
 
Ni kweli kama wakiziuza hiyo pesa haiwezi kumaliza matatizo yetu yote. Lakini kama zikitumika vizuri, zinaweza kuboresha sana hali ya askari kule porini na hivyo kuimarisha ulinzi [anti-poaching]. Kwa ufahamu wangu wa sector hii ya wanyamapori [I am a stakeholder], bila kuwajali askari wa wanyamapori [game scouts], ujangili hautakoma. Hali yao inavyozidi kuwa mbaya, ndio wanashawishika kuua Tembo ama kuwezesha ujangili kufanyika.

Sasa wewe mtaalamu unayejua "A,B,C, D ya biashara ya pembe za ndovu" nisaidie, kuzichoma pembe za ndovu moto ni "dawa" ya nini? It's like you are saying, the solution to the governance problem within the government and wildlife sector in particular is to set fire to the valuable ivory stockpile.

Problem: Poor governance.

Solution: burn the ivory so that everybody loses.

Really?

Kwa hiyo kwa mtazamo wako askari wa game wakilipwa mshahara mkubwa ujangili utakoma? Huoni kuwa inawezekana kabisa huyo huyo anayetoa orders kuhakikisha kuwa hakuna ujangili unafanikiwa ndiye huyohuyo anayeweza kutoa orders kwamba upande fulani wa mbuga kutakuwa na wazalendo wanawinda, hakikisheni hawasumbuliwi ili nanyi msipate usumbufu kwenye ajira zenu? Tena ukizingatia unono wa mishahara ni nani atakaye kubali kuharibikiwa?

Pale serikali ilipopigania kuuza bidhaa hizo haramu wataalamu wa mambo wakasema hapana. Vinginevyo tembo wangeendelea kuuawa na biashara kufanyika legally kwa kigezo cha kuuza stock iliyokamatwa. Usithubutu kumpa upenyo mswahili.
 
Mwanakijiji, wateketekeze fedha? Dollar? Wakati hata fedha ya kumlipa Askari wa Wanyamapori posho hamna? Vitendea kazi hamna? Na kuna ushahidi gani kuwa Serikali ikiteketeza shehena yake ya pembe za ndovu basi biashara hii itakoma? Ni kama vile umefanya hitimisho kuwa shehena hii iliyokamatwa Hong Kong imetoka kwenye maghala ya serikali. Ulimaanisha hivyo?


Mbona wanatekeza Bangi? Kwa nini tusiuze bangi tujenge Mashule?
 
Bse ata wakiziuza izo pembe ata hela itakwenda kwa wajanja then kuzitia moto ni vyema zaidi.
Kwa ukata walio nao CCM huu ndo mda wa kupata another source of fedha via selling izo pembe.
To me this is just another EPA.
Ila CCM ni wabishi kutoka madarakani ila ipo SIKU
 
ndio maana kwa mara ya kwanza niliungana na kenya kupinnga tz kutaka kuuza ule mzigo, tena bila aibu wanaenda kwa watu wenye akili timamu kujinadi kua serikali inataka ifanye biashara ya magendo? yaani kutoka kuwaachia wazungu migodi ya dhahabu mapaka kutaka kuuza pembe za ndovu si mastaajab ya mussa haya! hii inaonyesha jinsi serikali isivyo makini hasa wizara ya maliasili thanks heaven hata yule mwangunga kapigwa chini kwenye kura za maoni na tusimuone kabisa bungeni can you imagine alivyokua anashikia bango kuuza izi nyara, mara akawa anashikia bango kupitisha lami serengeti katikati ambayo ingestop the great migration of wild beast in africa utadhan karogwa!
 
No wonder walikuwa busy two weeks back kuwakonfyuzi WaTZ na mambo ya nani kaiba mke nai kaibiwa mke.....majini nk.....na media zetu dooo....hakunailiyoandika hii....thanks for the info
 
Inauma sana jamani hii nchi vipi?

kwanini tusijiulize sisi wenyewe jamani haiwezekani.?
Nafikiri bado hatujawa HURU tusimame imara tudai UHURU kweli watoto wetu watatuliza maswali mengi sana kuhusu nchi yetu na tutakosa majibu itakuwa aibu sana baba unakosa jibu la kumjibu mwanao kweli...

Tafakarini jamani Nyerere angekuwepo nafikiri angeomba kurudi IKULU aikomboe NCHI.

Kweli sie tumlaaniwa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Hii nchi nawaambiwa kama ccm watarudi madarakani basi tuombe mapinduzi ya kijeshi!

Mkuu genekai, mapinduzi yapi hayo? Jeshi letu ni thithiemu na wanasubiri kupiga kura!! Wale ndo wapiga kura tegemezi!! Sasa usishangae akiwa Rasi mpinzani basi nahisi mapinduzi ya kijeshi yanaweza tokea. Tanzania vyombo vya dola, majeshi, you name all ni serikali yenyewe!
 
Biashara ya ccm hiyo

Kwa hiyo una maana pesa ya kampeni imepungua kwa sababu ya moto wa Slaha na EPA hakuchoteki mpaka wakamua kuuza nyara zetu ili wanunue kanga, T-shirt na kofia kwa wanavijiji wetu waliojichokea kwa umaskini!!
 
CCM inatafuta hela za kampeni kwa kila hali.
Chagua CHADEMA CHAGUA SLAA kuepukana na dhuluma hii ya maliasili yetu
HONG KONG (AP) — Hong Kong customs officers have seized over one and a half tonnes of smuggled elephant ivory worth 10.9 million Hong Kong dollars (1.3 million US) shipped from Tanzania, they said Friday.


The 384 ivory tusks -- weighing 1.55 tonnes -- were found Thursday inside two containers labelled as "dried anchovies" at the Tsing Yi container terminal, the Ports and Maritime Command said in a statement.


Two men, aged 46 and 48, have been arrested as part of a continuing investigation, the statement said.


The international trade in elephant ivory, with rare exceptions, has been outlawed since 1989 after elephant populations in Africa dropped from the millions in the mid-20th century to some 600,000 by the end of the 1980s.


Anyone found guilty of importing unmanifested cargo into Hong Kong faces a fine up to two million dollars (260,000 US) and imprisonment for seven years.


In addition, those guilty of importing, exporting or possessing an endangered species for commercial purposes face a fine of up to five million dollars (640,000 US) and two years in jail, the statement said.


Kenya seized two tonnes of raw elephant ivory bound for Asian markets in August, saying it represented the country's largest recovery of elephant ivory in the recent past.
At least 4,000 elephants are killed each year across Africa to supply the illegal ivory trade, according to the conservation group WWF.
ALeqM5jlrWUqSf-bNMoRkJqEqbSxakjvnA


Nyara zilizokamatwa!

My Take:
Nilizungumza wakati ule TZ inalilia kuruhusu pembe hizi ziuzwe kihalali. Nilisema kwamba kwa vile wamekataliwa lazima itatatufwa namna tu lazima ziuzwe! Now here we are! Wameuza mbuga zetu, wameuza madini yetu, sasa na pembe zetu za ndogu wanauza kwanini wasizitekekeze kama wanavyofanya Bunduki?
 
Back
Top Bottom