Tangu vuguvugu la Mzee Lowassa hatuoni wala kusikia tena wimbi la wanaccm kuhamia CHADEMA. Tatizo nini?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,502
2,046
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyojieleza kabla ya uchaguzi wa 2015 ilikuwa kawaida sana kwa CHADEMA kupokea mamia ya wanaccm waliokuwa wakieleza wazi kuwa aidha wameichoka CCM au wamevutiwa na CHADEMA.

Hali hiyo kwa sasa haipo kabisa badala yake kila mara tunatangaziwa wanachama wa CHADEMA wanakihama chama hicho na kurudi CCM.

Hali hii inasababishwa na nini!?
 
Maskini wengi wa nchi hii ni wapinzani matajiri wengi wa nchi hii ni wapinzani
Viongozi wengi wa selikari ni wapinzani hata mwandishi wa juu Uzi ni mpinzani

Upinzani ni mawazo yaliyo tofauti na mwingne

Unao waona wanaenda kuungana na chama fulan sio malengo yao ila ni njaa zao za muda huo
 
Ni wapumbavu pekee tu watakaohamia chadema, Nani anataka kufukuzana na polisi kila dakika? Karibuni ccm tuitafune nchi, tz ni shamba la Bibi hakuna mwenye uchungu nayo ni mwendo wa kujichumia tu.
 
Back
Top Bottom