Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,293
- 8,204
Tangu ulipoondoka mambo yamebadirika miluzi imeongezeka
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika,
Watu waliookoka, wote wameshapotoka,
Twarudi tulikotoka, taifa linaanguka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, mafisadi wanacheka,
Uchumi umeanguka, keki inapukutika,
Rangi zinabadilika, vinyonga waongezeka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, mbwa wengi wanabweka,
Simba wameshatoweka, fisi wanaongezeka,
Uoto umetoweka, kijani kinafutika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, chama kinawatalaka,
Upendo umetoweka, taifa linachepuka,
Wazalendo tumechoka, wezi wameongezeka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, rushwa imeongezeka,
Haki iyanizidi rika, utu unarukaruka,
Furaha meimarika, unyonge unaondoka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, nia tumeshaizika,
Dira imetuponyoka, ghala limeshatoboka,
Bendera inachanika, tunu yetu menyofoka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, hasara zinasomeka,
Vifungo vinatoweka, habari zinasikika,
Na sauti zinatoka, na pingu zinakatika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, wachache twanung'unika,
Wengi wanaburudika, hawanuni wanacheka,
Endapo ukifufuka, utalia hutocheka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, akili zimeondoka,
Imla uliyoandika, haiwezi kusomeka,
Kweli paka kiondoka, panya wanarukaruka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, hatuna mchakamchaka,
Semi zimebadilika, hapa kazi kadhalika,
Wachache waheshimika, wengi wadharaulika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, wameibuka vibaka,
Hazina wanaibaka, fafuyo inabomoka,,
Na keki uliyooka, bure inagawanyika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, bado tunakukumbuka,
Sijachoka kuandika, mema uliyoyaweka,
Hayawezi kuondoka, kichwani nitayaweka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, Bunge limebadilika,
Bunge linasikika, rangiye imechujuka,
Milango imedondoka, vitasa vimefunguka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Najua umeshafika, kwa Mungu na Malaika,
Neno lako nakumbuka, lile "tutakukumbuka"
Kweli tushakukumbuka, kwetu umeadimika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Mwisho jipu laumuka, haliwezi kutumbuka,
Dakitari katoweka, sijui tutatibika?
Huduma imeondoka, hujuma twaialika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika,
Watu waliookoka, wote wameshapotoka,
Twarudi tulikotoka, taifa linaanguka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, mafisadi wanacheka,
Uchumi umeanguka, keki inapukutika,
Rangi zinabadilika, vinyonga waongezeka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, mbwa wengi wanabweka,
Simba wameshatoweka, fisi wanaongezeka,
Uoto umetoweka, kijani kinafutika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, chama kinawatalaka,
Upendo umetoweka, taifa linachepuka,
Wazalendo tumechoka, wezi wameongezeka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, rushwa imeongezeka,
Haki iyanizidi rika, utu unarukaruka,
Furaha meimarika, unyonge unaondoka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, nia tumeshaizika,
Dira imetuponyoka, ghala limeshatoboka,
Bendera inachanika, tunu yetu menyofoka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, hasara zinasomeka,
Vifungo vinatoweka, habari zinasikika,
Na sauti zinatoka, na pingu zinakatika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, wachache twanung'unika,
Wengi wanaburudika, hawanuni wanacheka,
Endapo ukifufuka, utalia hutocheka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, akili zimeondoka,
Imla uliyoandika, haiwezi kusomeka,
Kweli paka kiondoka, panya wanarukaruka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, hatuna mchakamchaka,
Semi zimebadilika, hapa kazi kadhalika,
Wachache waheshimika, wengi wadharaulika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, wameibuka vibaka,
Hazina wanaibaka, fafuyo inabomoka,,
Na keki uliyooka, bure inagawanyika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, bado tunakukumbuka,
Sijachoka kuandika, mema uliyoyaweka,
Hayawezi kuondoka, kichwani nitayaweka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Tangu ulipoondoka, Bunge limebadilika,
Bunge linasikika, rangiye imechujuka,
Milango imedondoka, vitasa vimefunguka,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Najua umeshafika, kwa Mungu na Malaika,
Neno lako nakumbuka, lile "tutakukumbuka"
Kweli tushakukumbuka, kwetu umeadimika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.
Mwisho jipu laumuka, haliwezi kutumbuka,
Dakitari katoweka, sijui tutatibika?
Huduma imeondoka, hujuma twaialika,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika.