Tangu Ujiunge JamiiForums, Mpaka Sasa Umenufaika Kwa Lipi?

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,820
23,121
Habari wana Jamii Forums,..

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza,.

Binafsi nimepata kuelimika kwa mada mbalimbali na kufanikiwa kupata ushauri ambao umekuwa wa manufaa makubwa sana kwangu.

Hayo ni machache tu, kama nawe umenufaika kwa lolote na Jamii Forums karibu tushirikishane,..

Nawasilisha,...
 
Napata habar mbalimbali pia nimepata nafas ya kutambua tabia mbalimbali za walimwengu.mtu analeta thread nzur tu mwisho wa siku anaambulia matusi.wakat mwingine huwa nacheka mwenyewe kwa michango ya watu humu.yote kwa yote tunaelimika na kuhabarishwa kupitia jamii forum.
 
Inaongeza uwezo wa kufikiri,uelewa mpana,mtu anaweza kujitambu inaleta na ustaarabu kwa wengi sana
 
Nimejifunza mengi sana kuhusu kilimo na ufugaji.
Pia nimepata uwanja wa kuitangaza Business Accounting Software, BUSY kwa biashara ndogo na za kati. Natarajia nitakapo pata wateja nitaichangia JF.
 
Mkuu mambo .mengi sana kupata habari zinazotokea kila kona kwa mda.pili nimefanya sana biashara ya cm.kwa washikaji humu nk
 
kiukweli mengi ni faida tatizo wengi wetu hatutaki kuukubali ukweli na hasa pale unapoguswa kimtazamo au kimaslai
 
Lakini kuna wengi pia waliopata hasara na matumizi ya JF kwa sababu imewaanika na wameshakimbia tayari, mfano Zitto, Mbasha, nk. Wapo wengine wanaambulia matusi mwanzo mwisho kwa ujinga wao mfano Le mutuz!
 
nimejifunza mengi kama mwanafunzi maisha baada ya masomo na uzoefu wa watu walionizidi umri kuhusu maisha kupitia mijadala mbalimbali pia uelewa wa mambo mengi kuliko kushinda fb na vijana wenzangu tusio jua nini kinaendelea baada ya nasomo kiufupi jamii forum ni darasa tosha kwa maisha halisi ya kijana wa kitanzania
 
Lakini kuna wengi pia waliopata hasara na matumizi ya JF kwa sababu imewaanika na wameshakimbia tayari, mfano Zitto, Mbasha, nk. Wapo wengine wanaambulia matusi mwanzo mwisho kwa ujinga wao mfano Le mutuz!

umenifanya nicheke mkuu jf raha tosha, aiseee kwa zito Jf imechangia sanaaaaa, shoza na mwampamba, mwigamba ni mfano tosha, inteligensia ya jf ni zaidi ya tiss
 
Inanisaidia kupata habari mbalimbali nje na ndani ya nchi, lakini kama nimevurugwa iwe kazini au nyumbani huniondoa mawazo na kunipa furaha
 
Ukiwa na stress ingia Jf ni rafki wa kweli mwenye kuburudisha, kuelimisha, kukosoa, kufariji, kuchekesha na mengine kibaaaao, Long lyf Jf
 
Back
Top Bottom