Tangu uhuru uongozi tanzania haonyeshi dalili za udini, fuatilia hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangu uhuru uongozi tanzania haonyeshi dalili za udini, fuatilia hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jan 3, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tangu nchi hii ipate huru hainyeshi kama udini upo hebu fuatilia uongozi wetu tangu uhuru

  HISTORIA YA BARAZA LA MAWAZIRI NCHINI TANZANIA  KILA wakati Baraza la Mawaziri linapotangazwa kunakuwa na sura mpya ambazo zinaingia na sura za zamani ambazo zinaondoka, lakini pia rekodi zikiwekwa kutokana na historia ya nchi, kuanzia nafasi ya rais hadi mawaziri wadogo.
  Tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961, kumekuwepo na watu tofauti walioshika nafasi ya rais, makamu wa rais, waziri mkuu na nafasi nyingine za uwaziri.
  Makala hii inajaribu kuangalia watu tofauti walioshika nyadhifa hizo tangu Tanganyika ilipopata uhuru na baadaye kuungana na Zanzibar mwaka 1964 ili msomaji aweze kupata picha ya nchi ilikotokea, ilipo na inakoelekea kila wakati baada ya uchaguzi.

  A. Marais

  1.Julius Kambarage Nyerere, muasisi wa taifa la Tanzania aliyeongoza nchi ya Tanganyika kuanzia mwaka 1961 hadi 1964 wakati ilipoungana na Zanzibar na kuongoza Serikali ya Muungano wa Tanzania hadi mwaka 1985.
  2. Ali Hassan Mwinyi, rais wa serikali ya awamu ya pili aliyeongoza mwaka 1985 hadi 19895.
  3. Benjamin Mkapa, rais wa serikali ya awamu ya tatu aliyeongoza nchi kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
  4. Jakaya Mrisho Kikwete, rais wa serikali ya awamu ya nne aliyeingia madarakani mwaka 2005 na kuchaguliwa tena mwaka huu.

  Nafasi ya Makamu wa Rais (wakiwemo makamu wa pili wa rais)
  1. Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa makamu wa rais mwaka 1964-1972
  2. Rashid Mfaume Kawawa, alikuwa makamu wa pili wa rais mwaka 1962-1965;
  3. Aboud Jumbe alikuwa makamu wa rais kuanzia mwaka 1972 hadi 1984
  4. Idris Abdul wakil alikuwa makamu wa Rais chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere
  5. Ali Hassan mwinyi alikuwa makamu wa rais kuanzia mwaka 1984 hadi 1985
  chini ya Mwalimu Nyerere)
  6. Joseph Sinde Warioba alikuwa makamu wa rais 1985 hadi 1990
  7. John Malecela alikuwa makamu wa rais 1990 hadi 1994
  8. Cleopa Msuya alikuwa makamu wa rais kuanzia 1994 hadi 1995
  9.Dk Omari Juma alikuwa makamu wa rais kuanzia 1995 hadi 2001
  10. Dk. Ali Mohammed Shein alikuwa makamu wa rais kuanzia 2001 hadi 2010

  C. Mawaziri Wakuu

  1. Julius Kambarage Nyerere alikuwa waziri mkuu wa kwanza mzalendo wa Tanzania kuanzia mwaka 1960 hadi 1961 na baadaye mwaka 1961 hadi 1962 wakati huo ikiwa ni Tanganyika. Kwa mujibu wa katiba ya 1961, Waziri Mkuu ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa serikali. Katiba ilipobadilishwa mwaka 1962, urais ndio ukawa cheo cha juu zaidi nchini, nyerere akishika nafasi hiyo.
  2. Rashid Mfaume Kawawa alikuwa waziri mkuu kwa mwaka mmoja 1962. Baada ya nafasi hiyo kufutwa na kurejeshwa mwaka 1972, Kawawa alikuwa tena waziri mkuu hadi 1977.
  3. Edward Moringe Sokoine, alikuwa WM kuanzia 1977 hadi 1980
  4. Cleopa David Msuya ambaye alikuwa WM kuanzia 1980 hadi 1983
  5. Edward Sokoine alirejeshwa mwaka 1983 hadi 1984
  6. Dk Salim Ahmed Salim alikuwa WM kuanzia 1984 hadi 1985
  7. Joseph Sinde Warioba, 1985 hadi 1990
  8. John Malecela alikuwa WM kuanzia 1990 hadi 1994
  9. Cleopa David Msuya Msuya alikuwa WM kuanzia 1994 hadi 1995
  6. Frederick Sumaye alikuwa WM kuanzia 1995 hadi 2005
  7. Edward Ngoyai Lowassa alikuwa WM kuanzia 2005 hadi 2008
  8. Mizengo Pinda alikuwa WM kuanzia 2008 hadi sasa.


  D. Mawaziri-Ofisi ya Rais (Ikulu)

  1. Ali Hassan Mwinyi alishikilia Ofisi ya Rais kuanzia 1970 hadi 1975
  2. Profesa Kighoma Ali Malima, alishikilia ofisi hiyo hadi mwaka 1990
  3. Amran Mayagila 1990 hadi 1995
  4. Fatma Saidi Ali alishughulikia utumishi wa umma
  5. Wilson Masilingi alishughulikia utawala bora 1995 hadi 2000
  6. Sofia Simba alishughulikia utawala bora 2008 hadi 2010
  7.Hawa Ghasia alishughulikia Menejimenti ya Utumishi wa umma kuanzia 2006-2010

  E. MAWAZIRI-OFISI YA MAKAMU WA RAIS
  1. Aboud Jumbe alikuwa waziri ofisi ya rais kuanzia 1970-1975
  2. Edward Sokoine alikuwa Waziri wa Nchi kati ya 1970 na 1975
  3. Muhammad Seif Khatibu alishikilia ofisi kuanzia 1988 kuchukua nafasi ya Salim Ahmed Salim.
  4. Muhammad Seif Khatib alishughulikia Muungano mwaka 2008 hadi 2010
  5. Dk. Batilda Burian (Masuala ya Mazingira)
  7. Dk. Husesein Mwinyi (Masuala ya Muungano) (2006-Februari 2008)
  8. Mark Mwandosya (Mazingira) (2006-Februari 2008)

  MAWAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU
  1. Peter Kisumo (Utawala wa Mikoa na Maendeleo ya Vijijini (1970-1975)
  2. Robert Ng’itu alikuwa waziri mdogo kati ya 1977 na 1980)
  3. Edward Lowassa alikuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuanzia 1990
  4. Dk. Batilda Buriani alishughulikia Sera na Utaratibu wa Bunge 2006 hadi 2008
  5. Philip Marmo (sera na Uratibu wa Bunge)
  6. Aggrey Mwanri
  7. Celina Kombani

  C. Mawaziri
  (a). Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
  1. Dk. Stirling (Waziri)
  2. Derek Bryceson alipewa wizara hiyo kabla ya uchaguzi wa mwaka 1965. Awali alikuwa Waziri wa Kilimo
  3. Lawi Nangwanda Sijaona alishikilia wizara hiyo kati ya 1970 na 1975)
  3. Dk Aaron Chiduo
  4. Prof Philemon Sarungi
  5. Prof David Mwakusya (2005-2010)

  B. Wizara ya Ardhi

  (i) Mawaziri wa Ardhi na Nyumba
  1. Lawi Nangwanda Sijaona alikuwa waziri mwaka 1965
  2. Austin K.E. Shaba (Mtwara), kati ya 1962 na 1965.
  3. Musobi Mageni alishikilia wizara hiyo kuanzia mwaka 1963
  4. John Mhaville, alikuwa kati ya 1970 na 1975
  5. Thabita Siwale
  6. Gideon Cheyo
  7. Mercel Komanya, mwaka 1990
  8. Edward Lowassa
  9. John Pombe Magufuli kuanzia 2006 hadi 2008
  10. John Chiligati, kuanzia 2008 hadi 2010


  Wizara ya Elimu
  1.Solomon Eliufoo, kuanzia 1962 hadi 1965
  2. Chediel Mgonja, kuanzia 1970 hadi 1975
  3. Abel K. Mwanga
  4. Nicholaus Kuhanga, kuanzia 1977 hadi 1980
  5. Padri Simon Chiwanga
  6. Thabitha Siwale
  7. Prof Philemon Sarungi, alikuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni
  8. Margareth Sitta, Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzia 2006 hadi 2008
  5. Profesa Jumanne Maghembe, Elimu ya Juu kuanzia Februari 2008 hadi 2010

  SAYANSI, TEKNOLOJIA, NA ELIMU YA JUU:
  A. MAWAZIRI
  1. Dk William Shija, alikuwa waziri wa kwanza wizara hiyo ilipoundwa
  2. Professa Peter Msolla, alishikilia wizara hiyo kuanzia 2008 hadi 2010

  Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi (sasa wizara ya Miundombinu)
  1. Mustafa Nyang’anyi
  2. William Kusila
  3. Dk Shukuru Kawambwa

  Wizara ya Fedha
  1.Mark Bomani, alikuwa Waziri wa Fedha na Uchumi na Mipango
  kati ya 1962 na 1965
  2. Abdulrahman Mohamed Babu, kuanzia mwaka 1970 ambaye alikuwa waziri wa Biashara na Viwanda
  3. Amir Jamal, kati ya 1970 na 1975
  3. Abdulrahman Mohamed Babu, kati ya 1975 na 1975
  4. Paul Bomani, kuanzia 1965)
  5. Amir Habib Jamal
  6. Edwin Mtei, kati ya 1977-1980
  7. Profesa Kighoma Ali Malima
  8. Cleopa David Msuya (Mwanga)
  9. Profesa Simon Mbilinyi
  10. Steven Kibona (1990)(Awamu ya Mwinyi)
  11. Daniel Yona, kuanzia 1995 hadi 2000)
  12. Basil Pesambili Mramba, kati ya 2000 na 2005
  13. Zakhia Hamdani Meghji
  14. Mustafa Mkulo, kati ya 2008 na sasa


  Wizara ya Ulinzi
  1. Abdallah Twalipo, kuanzia 1985
  2. Philemon Sarungi
  3. Profesa Juma Kapuya
  4. Dk Hussein Mwinyi

  (b) Manaibu waziri
  1. Seif Bakari, kati ya 1977 na 1980, akiwa waziri mdogo
  2. Abdallah Twalipo, kuanzia 1985
  3. Edgar Maokola Majogo, kuanzia 1995 hadi 2000)
  4. Emmanuel Nchimbi
  Dk. Hussein Mwinyi

  Wizara ya Mambo ya Ndani

  1. Job M., Lusinde, alikuwa waziri kuanzia 1962 hadi 1965
  2. Said Maswanya, kuanzia 1970 hadi 1975
  3. Ali hassan Mwinyi, alijiuzulu kutokana na mauaji ya Shinyanga
  4. Muhidin Kimario, kuanzia 1985
  5. Augustino Lyatonga Mrema, hadi mwaka 1995 alipoihama CCM, pia alichukuliwa kama naibu waziri mkuu
  6. Lawremce Masha


  Wizara ya Nishati na Madini
  1. Jeremiah S. Kasambala, alikuwa waziri kati ya 1962 hadi 1965 alipoangushwa kwenye uchaguzi
  2. Wilbert Chagula, kuanzia 1970 hadi 1975. Wizara ya Maji na Niashati ilikuwa mpya kwenye baraza la 1970. Awali ilikuwa chini ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, wakati Nishati ilikuwa chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda.
  3. Al-Noor Kassum, kati ya 1977 na 1980
  4. John Malecela, hadi 1985
  5. Jakaya Kikwete, kuanzia 1990
  6. Daniel Yona, hadi mwaka 2005
  7. Shamsa Selesia Mwangunga (2006-Feb 2008)
  8. William Ngeleja
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Angalia miaka ya enzi ya Nyerere kama anaonekana alikuwa mdini kwani naona watu wa dini zote wanaonekana
   
 3. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ndugu Sugu tunashukuru kwa kumbukumbu za viongozi wa nchi yetu toka uhuru. Wengine sisi ni wagumu kuelewa. Tunaomba ufafanuzi wa namna ulivyozitumia takwimu hizo kufanya hitimisho kwamba wakati wa Mwinyi ulianza udini na wakati wa Nyerere haukuwepo.
   
 4. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2017
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Prof. Ahmed Muhidin anachambua utawala wa Tanganyika vs Kenya na Uganda katika kujenga dola au jamii. Na mageuzi ya sasa ya kujenga taasisi baada ya kuvunja utawala wa kichifu uliokuwa na mizizi lakini serikali za sasa zimeshindwa kujenga taasisi na badala yake inajenga utawala wa ''mtu'' badala ya taasisi/mifumo kuziba pengo baada ya kuvunja tawala za kichifu/kikabila


  Source: Bilal Kenya
   
Loading...