Tangu Uhuru Tanzania ina Katiba 3 ambazo hazikushirikisha wananchi

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Tanzania ni nchi huru iliyopata uhuru wake mwaka 1961

Katiba ya kwanza iliandaliwa uingereza na kuleta tanganyika na kuanza kutumika baada ya kuonekana ina mapungufu.

Mwaka 1962 waliteuliwa wabunge 71 wakaifanyia marekebisho bila kupata maoni na mapendekezo ya wananchi.

Mwaka 1977 waliteuliwa wanachama wa tanu na Afro-shiraz 20 Zanzibar 10 na bara 10 wajumbe hawa wakiongozwa na Pius Msekwa na Sheikh Thabiti Kombo ndio waliotengeneza katiba ya CCM baada ya kuviunganisha vyama vya tanu na Afro-Sshiraz na baadaye wakatengeneza Katiba ya Jamhuri ya Muungano na wananchi hawakushirikishwa kutoa maoni na mapendekezo yao.

Tunaposema tuna taka katiba ya wananchi tunakuwa tunaamini tanzania haijawahi kuwa na katiba iliyotokana na maoni na mapendekezo ya wananchi. Katiba iliyopo ni ya CCM na ilitengenezwa na wanaCCM na haikushirikisha wananchi.

Baada ya nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi busara kubwa ingetumika kuandaa katiba ya wananchi kwani katiba iliyopo iliandaliwa wakati wa mfumo wa chama kimoja lakini hilo halikufanyika.

Kamati yenye maoni na mapendekezo ya wananchi inatakiwa

Katiba mpya
 
Baada ya nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi busara kubwa ingetumika kuandaa katiba ya wananchi
Mzanzibari anasema anajenga uchumi kwanza. Mbona nchini kwake walibadilisha kariba mwaka 2010??? Uchumi wa Zanzibar ni mkubwa kuliko wa bara?
 
Back
Top Bottom