Tangu tumepata uhuru tumekuwa tunafeli kupanga vipaumbele vya maendeleo

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Hili ni tatizo kubwa sana ambalo limeligharimu taifa letu ndio maana mpaka sasa tuna umaskini mkubwa sana. Maana nchi yetu haina wachumi wazuri wanaoweza kushauri vipaumbele vinavyoweza kubadili maisha ya Watanzania.

Mfano awamu ya kwanza ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ilijikita zaidi kwenye kupigana vita visivyo na msaada kwa raia wa kawaida. Tulitumia pesa nyingi kupigana vita Msumbiji, Uganda na hata Zimbabwe. Lakini sisi tukabaki masikini wa kutupwa hata barabara zikiwa vumbi tu.

Awamu hii ya tano imejikita kununua ndege ambazo hazina tija hata kidogo. Wananchi wana shida ya maji, madarasa na dawa za matibabu.

Hii yote ni sababu taifa halina watu wanaojua kupanga vipaumbele muhimu ili kutatua kero za wananchi. Tunaumia kila awamu ya CCM.
 
Bila ya CCM kuondoka madarakani hakutakua na mabadiliko ya aina yoyote nchi hii
 
1. Ebu fikiria, mtu mzima kabisa na 'mananii' yake anapanda jukwaani kufanya kampeni ya urais na kuifanya ajenda ya ushogeshwaji ni kipaumbele ktk mahitaji ya watanzania. Hivi mtu kama huyo angefanikiwa kuwa rais vipaumbele vyake vingekuwaje?

2. Hivi nyie chadema, kwa nini mnaona ujenzi wa ofisi ya makao makuu kuwa siyo kipaumbele cha muhimu? Miaka 25 ya uhai wa chama, miaka 16 ya uenyekiti wa mfalme mbowe, bado chama hakina hata kiwanja tu cha kujenga kiofisi cha makao makuu; hivi vipaumbele vyenu ni nini hasa?
 
85% ya majengo ya ccm walirithi kimabavu toka mfumo wa chama kimoja. Pitia ofisi walizirithi ccm kimabavu ukaone zina hali gani. Nitajie hata uwanja mmoja waliojenga ccm baada ya mfumo wa vyama vingi. Ukiwa na hayo majibu njoo utoe mrejesho.
 
1. Ebu fikiria, mtu mzima kabisa na 'mananii' yake anapanda jukwaani kufanya kampeni ya urais na kuifanya ajenda ya ushogeshwaji ni kipaumbele ktk mahitaji ya watanzania. Hivi mtu kama huyo angefanikiwa kuwa rais vipaumbele vyake vingekuwaje?
2. Hivi nyie chadema, kwa nini mnaona ujenzi wa ofisi ya makao makuu kuwa siyo kipaumbele cha muhimu? Miaka 25 ya uhai wa chama, miaka 16 ya uenyekiti wa mfalme mbowe, bado chama hakina hata kiwanja tu cha kujenga kiofisi cha makao makuu; hivi vipaumbele vyenu ni nini hasa?
Niambie CCM iliwahi kujenga ofisi yoyote kwa fedha za Chama? Mlichofanya ni kupora majengo ya serikali na kupaka Rangi. Hiyo Lumumba ya Dar lilikuwa ni jengo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kule Dodoma lile jengo la CCM zimetumika fedha za serikali kulijenga na ninyi mkapaka rangi za kijani na njano mkahamia, Viwanja vya michezo vyote mlipora toka serikalini. Kipi mliwahi kukifanya kwenye miundombinu na majengo kwa fedha yenu?
 
Back
Top Bottom