Tangu niione clip ya harusi ya prof. Kapuya na kimwana wake namchukia sana mke wangu

Kati ya vitu ambavyo babu yangu aliniasa nilipoanza maisha tu. Aliniambia mkeo lazima muwe mnatofautiana miaka kumi yaani nimzidi kuanzia miaka kumi na kuendelea, lakini ukioa mnalingana kiumri huko mbeleni kuna hatari utamtesa mtoto was watu maana mwanamke azeeka upesi kwa hiyo mke mnaolingana kwa umri baada ya muda utamuona mzee utaanza kutafuta ving'asti kitu ambacho utampa maumivu mkeo akikugundua. Nikatekeleza ushauri wake mke wangu wa kwanza tofauti miaka kumi na huyu niliyenae maana wa kwanza tulishindwana tukaachana tofauti yetu in miaka 26.Nina miaka 57 utapiga hesabu mwenyewe
Mkuu mm nina 26 demu wangu ana 23 unamaanisha nimuandae kisaikolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mkeo mtulivu huwez kuwaza ivo ,Hivi huyo binti hana babu zake?
Mke wangu ni mtuivu sana. Tatizo ni huo u-ajuza wake ukilinganisha na mke wa babu yangu (le professor).
 
Prof. Kapuya ana umri wa miaka 76 lkn ameoa mke mwenye miaka 25, mimi nina miaka 39 mke wangu ana miaka 33.

Kitendo cha mimi kuwa na mke mzee kiasi hiki ambaye kiumri anaweza kuwa sawa na mama wa mke wa prof. Kapuya, kinanifanya nijione sina bahati na nina laana .

Kwa umri wangu prof Kapuya ni sawa na babu yangu, sasa kwanini nioe mama wa mkewe?

Kila nikimuangalia mke wangu, siipati tena furaha moyoni na akilini mwangu. Taswira inayojengeka ni uhenga uliokithiri wa huyu mwanamke dhidi ya yule wa prof.

Hali hii ikizidi nifanyeje wadau?
FUNGA NDOA TU INGINE NDIO UNCHOWEZA KUKIFANYA, MABINTI WA MIAKA 25 WAKO WENGI, HESABU RAHISI CHUKUA UMRI WA KAPUYA TOA UMRI WA MKE WAKE NA KISHA ANGALIA TOFAUTI KISHA CHUKUA UMRI WAKO TOA WA MWANAMKE UNAYETAKA KUWA NAYE ILA ULINGANE NA ULE WA KAPUYA, BAADA YA HAPO MTAFUTE OA, UKIFIKA MIAKA 76 UTAKUWA NA MKE WA MIAKA 25. NADHANI HUWEZI TENA MCHUKIA MKEO KILA UKIANGALIA CLIP ZA KAPUYA NA HUYO MKEO WA MAKA 25.
 
Tatizo lako unaishi kwa kuangalia maisha ya mtu mwingine kitu ambacho si kizuri, una muda gani kwenye Ndoa? Ina maana huyo Mke wako ulimuoa akiwa na miaka 33? Kama jibu ni ndiyo je ulilazimishwa?
 
Prof. Kapuya ana umri wa miaka 76 lkn ameoa mke mwenye miaka 25, mimi nina miaka 39 mke wangu ana miaka 33.

Kitendo cha mimi kuwa na mke mzee kiasi hiki ambaye kiumri anaweza kuwa sawa na mama wa mke wa prof. Kapuya, kinanifanya nijione sina bahati na nina laana .

Kwa umri wangu prof Kapuya ni sawa na babu yangu, sasa kwanini nioe mama wa mkewe?

Kila nikimuangalia mke wangu, siipati tena furaha moyoni na akilini mwangu. Taswira inayojengeka ni uhenga uliokithiri wa huyu mwanamke dhidi ya yule wa prof.

Hali hii ikizidi nifanyeje wadau?

Unahitaji maombi na dua. Kabla ya kapuya kuoa ulikuwa na hilo tatizo? Mimi ninachoona kwako ni kwamba unataka kuoa mke mwingine, na sasa unatafuta kiki ya kuhalalisha ukahaba wako. Nenda kamwombe msamaha mke wako haraka
 
Back
Top Bottom