Tangu mchepuko wangu aanze vicoba, amekuwa na tabia ya kuniibia

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,385
98,851
Baada ya kipind kile kuleta Ujinga wa kuniomba Kodi ya fremu kwa nguvu bila utu kipind ambacho nmetoka kuibiwa dukan kwangu, ikapelekea kuua kabisa Lile wazo langu la kumfungulia biashara yake ya urembo wa kina mama.

Sasa Ni mwezi umepita aliponiomba nimfikirie tena niurejeshe Moyo nyuma nimfungulie ile biashara yake anayoipenda ya urembo na vipodozi vya kinamama, Akasema amekiri kakosa sana na kajifunza.

Nikamwambia
"kwaSasa huna akili ya kusimamia biashara wewe, akili yako bado waruwaru sana. Ntapoteza bure pesa zangu. Endelea TU na Kaz yako ya sheli, Cha muhimu unapata mshahara wako kwa wakati, unakula, unavaa unastarehe,unalala Basi inatosha iyo"

Akasema,
"Niamini mpnz wangu na Zamu Hii nataka nikuonyeshe kwamba naweza kwelikweli na nmekua. Naangalia maisha sahv. Nipe nafas ya mwisho mpenz wangu"

Nikasema
"sawa, ila vigezo na mashart ya mwanzo vitabadilika" akasema "vyovyote sawa"

Nikamwambia,
"Ili nikusapoti, Utapaswa kujilipia fremu Kodi ya miez 6 ya mwanzo kwa mshahara wako mwnyw, afu mzigo wa mwanzo utaugharamia mwnyw. Ukishaanza nikaona uko serious na unachokifanya ndo ntatoa sapoti yangu na Mimi"

Akakubali ikawa imeisha hivyo,

Sasa baada ya siku 2 akawa ameniingizia pesa mil. 1.6 kwny account yangu. Nikamuuliza yanini Hii pesa akasema nikija jion kwake atanifahamisha vizur. Nikasema sawa.

Iyo Jion nmepitia kwake,
anasema iyo pesa alontumia alikua anaweka akiba ya posho ya meza nnayomuachia na mshahara wake kazin kwa miez kadhaa. Kwaiyo ndo Kama nnavoona kafikia kiwango hicho. Nikasema " sawa wazo zuri ilo"

Akasema anaomba pesa nyngn anazopata awe anaweka kwangu, maana Kwny account yake anajikuta kazitumia.
Nikamwambia huo ujinga kuweka pesa kwangu Siutaki, kipimo kizur Cha kua mfanyabiashara Lazima uwe na nidhamu ya pesa, ukiona unashindwa kutunza pesa zako mwnyw Basi kwny biashara yako lazima ufeli. Jifunze Sasa kujitunzia akiba ya pesa zako mwnyw. Na kweli zile pesa nikazirudisha kwny account yake mwnyw pale pale. Ikawa imeisha hivyo.

Baada ya siku 3 akaja na wazo jingine,
Kwamba pale kazn kwao Kuna kikoba wenzie wakongwe pale wanacheza Cha kununua hisa, kuweka akiba na kukopeshana. Kila ijumaa anatakiwa kupeleka elfu 50. Ila anaweza weka zaid ya hizo ili kuweza kutunisha akiba yake kuweza kukopeshwa pale atakapohitaji mkopo.

Eti Kwamba kaona ndio Njia sahii ya yeye kutunza pesa zake zisipotee, maana Kwenye account yake yeye kashindwa kabisa kuzitunza pesa.

Akasema kila Mara anawashwa washwa azitumie na hata zile mil.1.6 nilizomrudishia sahv zishapungua zimebaki mil. 1.5
Basi nikaafiki japo Mimi sio muumini kabisa wa hizi Mambo hizo za vikoba. Na kwakua uyu ndo anaanza na naoan keshujua udhaifu wake kwny kutunza pesa.
Basi sio mbaya ngoja nimuache huenda itamsaidia.

KISA CHA KWANZA,
Kuna siku nmetoka ofsin na elfu 75 ya noti za elfu tano tano TU. nmeziweka kwny mfuko wa koti. nmeenda kwake, nmefika kwake kanivua koti na nguo vyote kavitundika kwny enga, tumefanya yakufanya tumemaliza, nmeoga, kanivalisha nguo zangu, nmemuachia noti 2 za elfu tano tano (yaani elfu 10) kisha nmeondoka zangu kwangu.

Asbh nmeamka nikaacha posho ya nyumban kwangu noti 3 za elfu tano tano (yaani elfu 15) Kisha nikaaga nikaondoka zangu.

Sasa nikiwa njian naenda kazin,
ikabid nipitie nikajaze mafuta ya elfu 50 sheli ya jirani.

Ile Kufika sheli nihesabu pesa nimpe aweke mafuta, najikuta ziko jumla noti 8 badala ya noti 10 za elfu tano tano(yaani elfu 40 badlaa ya eldu 50)
Kama nilivotarajia.
Yaani elfu 10 haipo.

Basi nikawa sina jinsi, nikaweka ya 40.
Ila nikahisi huenda nilihesabu vibaya wkt nafunga, Huenda nilichukua 65 badala ya 75 Kama nilivodhani. Ikawa imeisha hivyo.

KISA CHA PILI,
Kuna siku nyngn nafunga ofisi niondoke, nikabeba elfu 30 ya kula kwenye mfuko wa shati.
Sasa mda niko nasimamia vijana warudishie mageti.
Kuna dreva kirikuu mmoja akaniletea pesa 360,000 alzopeleka mzigo kwa mteja. Nazo nikaziweka kwny mfuko wa shati.
Nikiwa nishafunga Niko parking nmesimama nje ya gari namalzia kuongea na Simu ili niondoke zangu, akaja boda boda nae kaleta elfu 20 Kuna mzigo alipeleka kwa mteja. Nikazipokea nikaziweka kwny mfuko wa suruali.
Maana ake JUMLA Apo nikawa na sh. 410,000

Sasa nikaelekea kwa Mchepuko wangu Kama kawaida, nmefika tumefanya ya kufanya, tumemaliza nmeaga naondoka nikachomoa noti moja ya elfu 10 (yaani 10,000) nikaiacha mezani nikaondoka zangu kuelekea kwangu.

Kesho yake asbh,
Nikakuta pesa zote zimewekwa juu kwny droo ya kitandan, na nguo mpya zishanyooshwa tayar na wife.
Kwaiyo nikavaa Kisha nikaacha noti 2 za elfu 10 (JUMLA elfu 20) pale mezani nikaondoka zangu.

Sasa nmefika dukan,
Ikabid nichukue pesa zote zilizolala dukan nijumlishe na hizi nilizolala nazo nyumban ili nimpe kijana wangu azipeleke benki.
Katika kuhesabu nilizolala nazo nyumbani nikakuta nna JUMLA ya sh. 360,000 badala ya 380,000 maana Kwnyw 410,000 niliyoondoka nayo , nmetumia elfu 30 tu. Maana ake nnashoti ya elfu 20 haionekani.

Ikabd nimpigie wife aKasema alivyotoa pesa mifukoni kwny nguo chafu, aliziweka Kama zilivyo zote kwny droo hajatoa hata Mia.
Mchepuko nae nikampigia akasema hajatoa Ela yoyote ile Jana yake.
Nikasema sawa, huenda alivyonipa yule boda badala ya kuweka mfukoni huenda iyo 20 nilidondosha pale pale parking kwa ubize wa kuongea na Simu. Nikapotezea na maisha yakaendelea.

KISA CHA TATU,
Kuna wikend moja asbh saa 3 Nmetoka kwangu Nikiwa na LAKI (100,000) Mfukoni nmekwenda kwa Mchepuko wangu.
Nmefika Tumepiga Stori, nmekunywa supu pale. Kisha nikaaga naenda zangu saluni kunyoa. AKaomba anisindikize maana Hana Cha kufanya pale home MDA ule, nikasema sawa.

Tumefika saluni nmenyoa, nayeye kaomba kutengenezwa kucha na kuoshwa Nywele. Invoice ikaja jumla elf 25 nikailipa na tukapewa lisiti pamoja na chenji yetu nikaviunganisha na nikaweka pamoja pesa zingine mfukoni kisha kwenye saa 7 mchana tukaondoka zetu pale.

Tumeondoka pale tukaelekea baa moja kula na kulikua na bendi moja ya wazulu wanatumbuiza siku iyo, ikabd tukae pale kdg kuosha osha macho tukipiga bia kadhaa.
Sasa Katika kutumia pale vikoro-koro vyote invoice ilikuja jumla 32,500 na risiti walitupatia kabisa. Nikachanganya chenji na ile risiti pamoja na Ela nyingine zote pamoja nikatia mfukoni.
Kisha saa 10 nikamrudisha Mchepuko wangu nyumban kwake,

Tumefika,tumefanya ya kufanya, tumemaliza. nikamuachia noti Moja tu ya elfu 10 Kisha namimi saa Moja usiku nikaelekea kwangu.

Sasa nmefika nyumban chumbani nmebadili nguo,
Na Nmetoa kila kitu mifukoni(zile risiti na chenji zangu zote) ili nichambue niwape pesa nao wanyumbani wakanunue creti Moja la soda wanywe, nakuta nna balance ya 17,500.

Ikawa hainiingii akilini,
nikachukua zile risiti na kujumlisha nikakuta nnashoti ya elfu 15.

Hapo akili ikawaka kwamba Kuna mchezo mchafu unaendlea kule kwa Mchepuko wangu maana malipo yote nilipewa risiti za malipo.
Nikijumilisha na kutoa hesabu ya zile risiti zote natakiwa kubakiwa na balance ya 32,500 na sio 17,500 Kama nilivyoikuta mifukoni.
Na hatujasimama wala kununua kitu chochote kile uko njiani.

Basi Nikawapa watoto Ela ya soda elfu 15 waondoke zao, ila nikajipanga next time kwa Mchepuko lazima niweke mtego nijue mbichi na mbivu.

KISA CHA JANA,
Jana nikajipanga kumkamata mwizi wangu,
nikiwa natokea Safar dodoma, nikampigia mchepuko na kumwambia kwamba nitapitia hapo kwako unipe kimoja cha fasta kabla sijaenda kwangu. Akasema POA

Nikapitiliza bar, nikasukutua bia Moja mdomoni nipate harufu ya bia afu ntajifanya nmelewa kisha nifanye uchunguz huwa anachukuaje pesa zangu uyu mifukoni. Ili Nimkamate ready handled.

Basi nikaandaa noti za 120,000 nikazinakili namba nne za mwisho kwa kila noti kwny karatasi ya pembeni, pesa nyngne nkazificha kwenye Gari. Hizo zilizonakiliwa namba nikaziweka kwny suruali. Kisha nikaenda kwa Mchepuko.

Kweli nmefika nmejifanya nmelewa chakali, nayumba kwelikweli. Nmefika kanipokea na kwenda kubwaga kitandan chali.
Kisha akaanza nivua nguo zangu. Kamalizia kunivua nguo Kaenda kuzitundika kwny enga Kisha Akarud nakuanza kunipapasa uku na kule.
Nikajifanya nmelewa chakali sitoi hata ushirikiano.

AKainuka Kaenda ilipo suruali na shati kuanza kukagua mifukoni, nikawa nafumbua kidg kidg namchungulia anavokagua. Baada ya kuzipata pesa akawa anazihesabu zote Kisha akatoa noti mbili akaweka pemben kwny dressing table yake. Nyingine akazirudisha kwny suruali.

Sasa nikiwa najiandaa niinuke nimkamate ready handled, nikaona kaziacha pale anakuja uelekeo wangu wa kitandan na kisha kuinama uvunguni. Akatoa kibox Cha chuma vile wanahifadhia ela (sefu/vibubu). Apo Ikabd niwe mpole kwanza nichunguze nn kitaendelea.

Nikaona karud na kibubu mpk kwny dressing table kisha kachukua zile noti mbili, Moja baada ya nyngn anazikunja na kuzitumbukiza kwn kile kibubu Cha chuma. Kisha aarudi kitandani na akakiburuza kukirudisha kule uvunguni kilipokua.
Moyoni Nikajua kumbe uyu huwa anaficha uku.
Okay haina haja ya kupigizana nae kelele kwa Sasa. Ebu nitulie

Nikatulia pale Kama dkk 40 hivi Kisha nikajifanya namuomba anisindikize kwny gar niende zangu nyumban, kweli akafanya hivyo.
Kufika kwny Gari nikajifanya siwez hata kuendesha naomba aniendeshe. Kweli akafanya hivyo.

Akaniendesha mwnyw mpk kanifikisha mita chache karibia na nyumbn na kunambia niendeshe mwnyw sasa. Yeye anaishia hapo, atarud kwake na boda boda. Nikasema sawa.

Sasa leo Kulipokucha,
Nikampigia saa 3 akasema keshafika KAZIni, nikamjibu Mimi ndo naamka Niko nyumbn mwili wote unauma siendi kokote. Akasema sawa

Basi kwakua ninazo funguo za akiba pale kwake, nmekwenda kwake nmefungua na nmebeba kibubu kizima chenye pesa zake zote pamoja na zile noti mbili ndani nilizonakili tarakimu zake nne za mwisho.

Sasa Hapa namsubiria tu alalamike kwamba kibubu chake Cha pesa hakionekani mle ndani kwake ili nimlipue LIVE kabisa mkanda wake mzima wa kunisachi alokua anaufanya na ushahidi wa wazi kabisa ninao.

NGOJA TUONE,
TAYAR NMESHATEGA BOMU,NASUBIRI LILIPUKE , NTAWAPA MREJESHO
 
Baada ya kipind kile kuleta Ujinga wa kuniomba Kodi ya fremu kwa nguvu bila utu kipind ambacho nmetoka kuibiwa dukan kwangu, ikapelekea kuua kabisa Lile wazo langu la kumfungulia biashara yake ya urembo wa kina mama.

Sasa Ni mwezi umepita aliponiomba nimfikirie tena niurejeshe Moyo nyuma nimfungulie ile biashara yake anayoipenda ya urembo na vipodozi vya
Kajambazi hako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom