juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,463
Kwanza niseme tu wazi kwamba Magufuli sikumpigia kura na wala sitakuja nimpigie kura hata hiyo 2020. Japokuwa nilijua atashinda na ninajua pia hata 2020 atashinda na safari hii nahisi atashinda kwa kishindo.
Ila kiukweli pamoja sikumpa kura yangu kuna mambo mawili tu nampongeza tangu aingie madarakani. Kuna vingi kafanya ,mfano kanunua ndege,kabana matumizi,kazuia safari za nje kwa wateule wake,kajenga airport huko Chato,mapato TRA yameongezeka,kazuia mianya ya rushwa na wizi.
Kaleta mahakama ya mafisadi japo haina wafungwa,kaondoa wanafunzi na wafanyakazi hewa,,aisee ni mengi kafanya. Ila mimi hayo yote hayanihusu maana sio mwajiriwa wa mtu wala wa serikali na sifikilii kuajiliwa.kwa hiyo hayo hayanihusu kabisa. Mimi alichonifurahisha ni
1: Kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa,kwa kweli nampa hongera raisi,kwa sababu hii mikutano inaleta uongo na kudumaza akili za watanzania,ni mikutano hiihii ilisema Lowassa ni mwizi na fisadi papa,na ni mikutano hiihii ikaja kusema Lowasa sio mwizi bali ni mwanamabadiliko. Kwa hiyo kitendo cha rais kuzuia hii mikutano ni cha kupongezwa na kila mweye akili timamu. Hii mikutano haikuwa na tija bali ni kupoteza muda tu na kusemasema wau
2: Kuzuia bunge live kwa kweli amecheza kama pele. maana ilifikia hatua wabunge wanatafuta umaarufu tu bungeni ila majimboni kwao hawana cha maana. Sasa safari hii wakae wafanye maedeleo majimboni, yale mambo ya kupata ubunge kwa sababu tu ya umaarufu wako hayapo tena. Maana kuna watu ni wabunge tu ila wanajulikana Tanzania nzima ova ni mbunge wa taifa. Sasa safari hii ubunge wataupata kutokana na maedeleo wanayoleta majimboni na sio kwa umaarufu tu. Na natamani rais asilegeze kamba,ashikilie hapohapo.