Tangu Lini Majambazi wa Kawaida Wakatumia Gari Bila Number Plate? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tangu Lini Majambazi wa Kawaida Wakatumia Gari Bila Number Plate?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MgungaMiba, Jun 29, 2012.

 1. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Siku zote majambazi wa kawaida hutumia namba za bandia kwenda kufanyia uhalifu, kwani wakitumia gari bila namba, basi hata askari (Patrol) wasio na shaka watashtuka. Kwa hiyo waliomteka Dr Ulimboka, Kama ni kweli gari lao halikuwa na namba, ni dhahiri walikuwa na uhakika wa kutobughudhiwa na wanausalama wowote watakaokutana nao. Kwanini? Kama sio wenzao?
   
 2. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280

  La pili,

  Majambazi utesaji wao tunaujua nivipigo vya mapanga, kuoboa macho, kukata viungi n.k.....

  Lakini utesaji alioteswa Dr Ulimboka unaonekana kabisa ni "profeshono"..!!

  Ni watu waliosomea mambo hayo kwa kodi zetu leo wanatugeuka na kutufanyia sisi unyama walitakiwa kuwafanyia Al

  shabaab!!!!  ....
   
 3. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kova ni mshtakiwa na 1
   
 4. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Serikali imekwisha naiona Tanganyika mpya inakuja
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu inayoongozwa na CCM imeanza kugeuka kuwa serikali ya kidikteta dhid ya rai wake waiokubaliana nayo. Wabunge wa upinzani walikwata na mapanga, halagu serikali ikakaa kimya. Kuna wafguasi wa upinzani waliouwawa huko Igunga lakini serikali ikakaa Kimya. waandamanai wa upinzani waliuwawa na serikali hiyo hiyo. wananchi waliokuwa wakilalamikia maeneno yao kuingiliwa na wawekezaji huko Tarime waliuwawa na serikali hiyo hiyo.................................................................................................................................................................................................
   
 6. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Hivi kweli utoke leaders club na gari bila plate no mpaka mambwepande bila kukamatwa na trafik ? Maeneo hayo yana ulinzi mwingi kuliko maeneo mengine ya dar au wadau mnasemaje?
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe ulikuwepo? au umeambiwa hivyo?
   
 8. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Unaitwa Zombe??!! (No Wonder!)
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umeona jina lako? ni tusi, halafu nashangaa hawa ma moderator wa JF wanaliacha. Hawajui Kiswahili au wanafanya makusudi?
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Jambazi wa kawaida akitumwa kuja kukuua anakudunda risasi na kukuacha pale pale alipo kukuta.
  Majambazi huteka watu wenye fedha na kuwatesa ili waseme fedha ziko wapi??

  Hii ya kuteka kupiga kiumbwa umbwa huku wannatweta na kusema umetutesa sana wewe ni staili ya UWT na Polisi wa Tanzania. It is risk and costly it terms of mission kwa jambazi wa kawaida kuendelea kuzurura na mtu ambaye nia halisi ni kuondoa uhai wake.

  Hii kitu imeacha finger prints za UWT na Polisi.
  Huhitaji kuwa kachero wa kimataifa kunusa kwamba serikali ina mkono.
  Tulio wengi hapa ni hodari wa kujadili matokeo ya mwisho na kuacha kabisa kwenda hatua kwa hatua tangu mwanzo na ikiwezekana ku trail mwnendo wa kila kitu toka mgomo ulipo anza.
  Ukichukua majina 10 ya watu ambao ni watuhumiwa na kutrace simu zao utapata picha fulani.
  Ukichukua simu ya Dr Ulimboka ukatrace simu zinazoingia na kutoka ni wazi kwamba utapata picha fulani.
  Kila jambo ni lazima liache Traill za DNA zake nyuma
  Ukipanga tukio kwa tukio ni wazi kwamba utapata sura ya tukio zima.
  Uzuri kwamba Dr Ulimboka yupo hai na amekwisha ongea.
  Usije ukafanyika Uzembe wa aina yeyote na kutoa mwanya wa serikali kufanya jaribio jingine dhidi ya maisha ya Dr Ulimboka.

  Naomba vijana walio majembe ya kazi pale Bungeni kuanzisha hoja kuhusu misitu inayozunguka ukanda wa Dar.
  Misitu kama Pande na jinsi ambavyo imekuwa ikitumika kutupa watu waliokufa au waliohai lakini wameumizwa vibaya ili wafe huko kama alivyofanyiwa Dr Ulimboka.
  Sijawahi kufika huko Pande lakini kuna wakati nilifika Misitu ya Kanzagale nje kidogo tu ya Kibamba, nakwambia huwezi amini jinsi msitu ulivyo shona kisawa sawa.

  Nadhani kuna haja ya kuongelea nini kifanyike kuzuia misitu hii isiendelee kuwa maeneo ya kuficha uovu wa Polisi na UWT, I dont like their new name TISS it sounds like a hiss of snake
   
 11. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kazi ya Dhaifu hiyo; mumiani mnywa damu za watu.
   
 12. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hebu tuweke Mawazo yetu pamoja kwa Pande zote,pia tukumbuke ' Watu Kibao wameshatekwa,kuteswa na Hata kupigwa Risasi Majumbani mwao na Kwingine Kusikojulikana.
  Ukweli Upo na Utakuwa Bayana,Lakini Povu litutoke kwa ajili kusimamia sijui iundwe tume ni Upuuuuzi.
  Zitaundwa tume Ngapi kuchunguza watu waliopigwa mapanga,walioteswa na Hata kupigwa Risasi apa Tanzania?

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Hao ni majambazi wa dhaifu.
   
Loading...