Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,657
- 22,254
NSSF ni mfuko wa jamii na pesa zilizomo kwenye mfuko huo ni za jamii ikiwa na maana si za serikali ni za wanachama.
Tangu awamu hii ya tano NSSF imekuwa ikishindwa kuwalipa kwa wakati wenye pesa zao ambao ni wastaafu, licha ya wastaafu kuwasiliana na waliojipa jukumu la kuwahifadhia lakini shirika limekuwa likishindwa kutoa jibu juu ya kushindwa huko kunasababishwa na nini. Kinachoonekana sasa ni kuwa NSSF inategemea ikusanye pesa toka kwa waajiri ili iweze kuwalipa wastaafu!
Hivyo badala ya malipo kufanyika tarehe 24 ya mwezi yanafanyika kati ya tarehe 29 na 31 ya mwezi baada ya makusanyo!
Ni vyema shirika lijitokeze hadharani na kuwajulisha wastaafu kama waendelee kutegemea pensheni zao ambayo ni halali yao au lijitangaze kuwa limefirisika ili wastaafu waondokane na usumbufu wanaoupata wa kusota kila siku kwenye vituo vya malipo.
Inaonekana NSSF imetoka kwenye jukumu lake la msingi la uhifadhi wa pesa za watu na kuziona kama ni kodi hivyo kuzitumia kwenye majukumu mengine.